Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Serikali ipi unayotaka iaminike?!

Huyo Kakoko mwenyewe ana tuhuma za wizi, na ndio maana kasimamishwa! Sasa unataka tumwamini mtu mwenye tuhuma za wizi?!
Sasa weka wewe mkataba basi tuuuone ili kumkata kabisa ngebe za kakoko na ili kusapoti hii mada yako.
 
Pole sana!!

Kwa mfano, ulitaka niseme kitu positive kipi?! Kununua ndege? Kujenga Chato International Airport?! Kipi hasa ambacho ulitarajia nikiseme?!
Kwa hiyo hayo tu ndio aliyoyafanya tangu awe rais?

Mkuu hivi ndio unataka tukusapoti kwenye hii mada yako kwa mitazamo hii kweli?
 
Mradi wa Bandari wa Bagamoyo ulikuwa na mambo makubwa matatu:-
1. Bandari yenyewe
2. Industrial Park
3. SGR kutoka Bagamoyo to the main SGR line!
Mradi una mambo matatu, umejuaje?

MWONGO MKUBWA!

Umejuaje contents za mkataba bila mkataba?

TUNATAKA KUUONA MKATABA!
 
Mradi una mambo matatu, umejuaje?

MWONGO MKUBWA!

Umejuaje contents za mkataba bila mkataba?

TUNATAKA KUUONA MKATABA!
Toka kule juu page ya kwanza watu wamedai aweke mkataba hapa ila anajibu blaa blaa
 
Muongozo mkuu wa miradi ni Mkataba, bila mkataba kuhusishwa hata ukiandika maneno matamu kiasi gani bado yanakuwa hayana maana.
 
Kwa hiyo hayo tu ndio aliyoyafanya tangu awe rais?

Mkuu hivi ndio unataka tukusapoti kwenye hii mada yako kwa mitazamo hii kweli?
Hapa chini ni hoja niliyotoa miaka 3 iliyopita kuhusu SGR!

Mkuu JokaKuu, ahsante kwa mwaliko kwenye mjadala murua kama huu.

Kwanza nitangulie kusema jambo moja. Binafsi, mradi kama mradi nauunga mkono ingawaje sina hakika sana kama unakoelekea mradi (Central to North East Corridor) ni right direction.

Ningetamani niseme mengi katika hili lakini wacha nijikite kwenye hoja zako.

To start with, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana, kwamba, at least in the short run, SGR itaua sana ajira na sio kuongeza kama wanavyodai!

By short run, kwa project kubwa kama hii namaanisha angalau miaka 5!

Ndani ya kipindi hicho, SGR itaua sana ajira rasmi na zisizo rasmi.

Effect of economic multiple impact itakuwa negatively higher kwa sababu, kama ulivyosema, sekta ya usafiri wa barabara ina-stimulate sekta nyingi sana za kiuchumi at distributive/multiplication level.

But of all that, bado naunga mkono SGR kwa sababu I believe in the economy that produces though I also doubt ikiwa ninachofikiria mimi ndo hasa wanachofìkiria Decision Makers.

I believe tukiwa visionary, basi economic impact ya SGR ni kubwa kuliko road transportation system tuliyonayo ambayo inachochea sana usafirishaji wa transit goods and related sectors.
Again, pole sana kwa hayo mawazo yako kwamba mtu akimpinga jambo la JPM basi ana chuki na JPM!!!

Lakini siwezi kuwa mjinga wa kuunga mkono ununuzi wa ndege!

Siwezi kuwa mjinga wa kuunga mkono ujenzi wa Uwanaja wa Ndege wa Kimataifa eneo ambalo halina sifa hizo!!

Hata alipojenga hospitali ya rufaa Chato, hoja yangu haikuwa ujenzi wa hospitali bali kwanini asingejenga Geita iliyo katikati ya mkoa na kwenda kujenga chato ambayo ipo pembezoni kabisa mwa mkoa!!

Na hata lilipokuja suala la CRDB Chato miaka 3 iliyopita, hoja yangu ilikuwa hii hapa:-
Ukifuatilia afanyayo JPM unaweza kuzeeka haraka!

- Chato ni Wilaya pekee yenye international airport nchini!

- Chato ni wilaya pekee nchini ambayo soon itakuwa na hospitali ya rufaa ya serikali

- Chato ni wilaya pekee nchini kuwa ya kwanza kupata bohari ya madawa wakati kulikuwa na mikoa kadhaa hawakuwa nayo!

Ukishayatafakari hayo tu; hilo la CRDB wala haliwezi kukushangaza!

But to be honest, kuna uwezekano uwekezaji wa tawi la CRDB ukawa more profitable kuliko international airport!

Potential ya benki za biashara ni mikopo!! Na kama Chato hakuna NMB, basi wanaweza ku-influence civil servants wafungue bank accounts zao CRDB Chato Branch na hivyo ku-stimulate branch businesses!

Wakiwa more smart, wanaweza "kununua" mikopo ya civil servants iliyopo NMB ikahamishiwa CRDB Chato Branch na hivyo ku-stimulate lending business!

Therefore, wanaweza wasiwe good performing branch lakini pia wanaweza isiwe white elephant investment.

With microfinancing, tawi linaweza kufanya vizuri hata kama kwa kujivuta vuta!

Lakini International Airport... HAPANA!
Kwa mara nyingine, pole sana!!!

Hizo fikra zako za kudhani watu tunamchukia JPM zitakuzeesha kaba ya wakati wako kwa sababu, yale ambayo hatukukubaliana nae, watu tutaendelea kuandika, na wewe utaendelea kutoa povu!!!
 
MAPENDEKEZO

Reserved for later
Sawa sawa mkuu (nasikilizia mapendekezo yako)

ila binafsi, nasema kitu kimoja tu katika hili sakata:

maendeleo yawe kwa nchi (1) na wananchi (2)

kuna mijitu kila kona wapo! wale wa 'unanijua mimi ni nani?' kisa Mh. Rais anamsikia(na sio kumjua). huu ushamba uishe sasa.

kuna kampuni nyingi za kigeni ambazo zilikuja na kutaka kujikita kwenye maswala ya infrastructure zilisepa. they counted and weighed their losses wakaona ni uendawazimu. maana ofisi za mabalozi wanatangaza fursa hii wakati on ground ni utumbo mwingi na ukaangaji wa maini. kuna mabalozi wenye heshima zao walioneka bure kutokana na utendaji nchini pale mwekezaji anapoingia.

wajenge wasijenge, taratibu zifatwe na vyombo husika vichunguze kampuni na viongozi wa makampuni hayo na pale inaonekana kuna jambo sio sahihi, watu wawe bold kusema. bila kumuogopa mtu kwani ujenzi wa leo ni kwa manufaa na matumizi ya vizazi vijacho. maana kama jiwe alivyosema, unaweza kutaka kuchukua ng'ombe wako pale ambapo simba kashambana na ukajeruhiwa pamoja na kwamba ni mali yako!

miradi mingi ya Tanzania imekua kituko. Hebu angalia mwendo kasi, pale bonde la msimbazi, ni nini kile kama sio uchafu. na anayedhalilika ni kiongozi wa nchi kwani watendaji wake wakishapata chao, wao ni matumbo yao na familia zao. mwisho wa siku kiongozi unaonekana kituko.

bado watanzania (wengi) hatujastaarabika, kutoka viongozi mpaka wananchi! kila mnapoenda kwenye nchi zilizoendelea mnang'atuka meno na ku-admire ya wenzenu, wakirudi nyumbani mziki ni ule ule.

tubadilike! nchi isiwe shamba la bibi...

waweke mikataba wazi, vyombo kama takukuru wahusike!

it's high time our nation benefits and reaps from the fruits that she bares for the benefit of all not a few!
 
Hapa chini ni hoja niliyotoa miaka 3 iliyopita kuhusu SGR!


Again, pole sana kwa hayo mawazo yako kwamba mtu akimpinga jambo la JPM basi ana chuki na JPM!!!

Lakini siwezi kuwa mjinga wa kuunga mkono ununuzi wa ndege!

Siwezi kuwa mjinga wa kuunga mkono ujenzi wa Uwanaja wa Ndege wa Kimataifa eneo ambalo halina sifa hizo!!

Hata alipojenga hospitali ya rufaa Chato, hoja yangu haikuwa ujenzi wa hospitali bali kwanini asingejenga Geita iliyo katikati ya mkoa na kwenda kujenga chato ambayo ipo pembezoni kabisa mwa mkoa!!

Na hata lilipokuja suala la CRDB Chato miaka 3 iliyopita, hoja yangu ilikuwa hii hapa:-

Kwa mara nyingine, pole sana!!! Hizo fikra zako za kudhani watu tunamchukia JPM zitakuzeesha kaba ya wakati wako kwa sababu, yale ambayo hatukukubaliana nae, watu tutaendelea kuandika, na wewe utaendelea kutoa povu!!!
Nami nakuuliza kwa mara ya pili, kwa akili yako kubwa sana ni hayo tu ndio JPM kalifanyia hili taifa,,?

Tukirudi kwenye mada,..

Kwanini usitimize takwa la wengi kwenye huu uzi wako wa kisomi kwa kuweka mkataba hadharani na ili tuzidi kumdharau sana huyu JPM?
 
Nami nakuuliza kwa mara ya pili, kwa akili yako kubwa sana ni hayo tu ndio JPM kalifanyia hili taifa,,?

Tukirudi kwenye mada,..

Kwanini usitimize takwa la wengi kwenye huu uzi wako wa kisomi kwa kuweka mkataba hadharani na ili tuzidi kumdharau sana huyu JPM?
Kwahiyo unataka nianze kujadili yooote aliyofanya JPM, ninayoyaunga na nisiyoyaunga mkono?! Nimekutajia miradi ya JPM ambayo watu wenye chuki nae tumekuwa tunaipinga... mbona unashindwa kuelewa?

Halafu acheni kujificha kwenye mkataba kwa sababu tu hamna hoja!!!

Nimekuuliza, Kakoko aliyewaambia Wachina wanataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, amekuonesha huo mkataba?

Ikiwa hata huko bungeni Wabunge wamekuwa wakililia kupewa mikataba na hawapewi, halafu unataka huo mkataba nikuwekee mimi JF?

Upo serious kujadili mada wewe?!

Hoja zangu zinajadilika bila kuona mkataba kwa sababu ni matokeo ya research!!!
 
Mradi una mambo matatu, umejuaje?

MWONGO MKUBWA!

Umejuaje contents za mkataba bila mkataba?

TUNATAKA KUUONA MKATABA!
Nimeshasema huna hoja, so stop wasting my time!! Huwezi kushindwa kujadili mada eti kisa hakuna mkataba wakati tangu umezaliwa hujawahi kujadili mada yenye mkataba hapa JF!!

Na ikiwa unashindwa kujua hata mambo madogo kama hayo ambayo yameshawekwa wazi tangu zamani, si itakuwa kupotezeana muda tu kuendelea kujadiliana na mtu wa aina yako!
 
Kwahiyo unataka nianze kujadili yooote aliyofanya JPM, ninayoyaunga na nisiyoyaunga mkono?! Nimekutajia miradi ya JPM ambayo watu wenye chuki nae tumekuwa tunaipinga... mbona unashindwa kuelewa?

Halafu acheni kujificha kwenye mkataba kwa sababu tu hamna hoja!!!

Nimekuuliza, Kakoko aliyewaambia Wachina wanataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, amekuonesha huo mkataba?

Ikiwa hata huko bungeni Wabunge wamekuwa wakililia kupewa mikataba na hawapewi, halafu unataka huo mkataba nikuwekee mimi JF?

Upo serious kujadili mada wewe?!

Hoja zangu zinajadilika bila kuona mkataba kwa sababu ni matokeo ya research!!!
Kwa vile kakoko hajaweka mkataba akaja na blaa blaa..

Wewe hujaweka mkataba umekuja na blaa blaa..

Wote nyie ni wa kupuuzwa..
 
UTANGULIZI

Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!

Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
  • Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
  • Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).

Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!

Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!

Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:


Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.

Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!

Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!

Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.

Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!

Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!

Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.

Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).

Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!

Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!

Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!

Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!

Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!

Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!

Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!

Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”

Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.

Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.

Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!

Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!

Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!

Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”

Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!

Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.

Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”

Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!

Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:


Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.

Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!

Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!

Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!

Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!

Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!

JokaKuu
Mtaleta hoja nyingi zenye kila aina ya rangi lakini hicho unachokitetea hakina tija. Weka kataba wake hapa sio kuleta porojo za utafiti feki na makala zilizojaa hisia binafsi kutokana na maslahi uliyokuwa nayo
 
Back
Top Bottom