Nimeshasema huna hoja, so stop wasting my time!! Huwezi kushindwa kujadili mada eti kisa hakuna mkataba wakati tangu umezaliwa hujawahi kujadili mada yenye mkataba hapa JF!!
Na ikiwa unashindwa kujua hata mambo madogo kama hayo ambayo yameshawekwa wazi tangu zamani, si itakuwa kupotezeana muda tu kuendelea kujadiliana na mtu wa aina yako!
Mtaleta hoja nyingi zenye kila aina ya rangi lakini hicho unachokitetea hakina tija. Weka kataba wake hapa sio kuleta porojo za utafiti feki na makala zilizojaa hisia binafsi kutokana na maslahi uliyokuwa nayo
Nimesoma hii kitu usiku wakati usingizi umekata, strong points which need strong minds kuijadili, bila facts huna sababu ya kupinga hoja za mdau lakini pia bila facts za mkataba hatuwezi kufanya objections zozote kwa sasa.
Kwahiyo unataka nianze kujadili yooote aliyofanya JPM, ninayoyaunga na nisiyoyaunga mkono?! Nimekutajia miradi ya JPM ambayo watu wenye chuki nae tumekuwa tunaipinga... mbona unashindwa kuelewa?
Halafu acheni kujificha kwenye mkataba kwa sababu tu hamna hoja!!!
Nimekuuliza, Kakoko aliyewaambia Wachina wanataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, amekuonesha huo mkataba?
Ikiwa hata huko bungeni Wabunge wamekuwa wakililia kupewa mikataba na hawapewi, halafu unataka huo mkataba nikuwekee mimi JF?
Upo serious kujadili mada wewe?!
Hoja zangu zinajadilika bila kuona mkataba kwa sababu ni matokeo ya research!!!
Nimesoma hii kitu usiku wakati usingizi umekata, strong points which need strong minds kuijadili, bila facts huna sababu ya kupinga hoja za mdau lakini pia bila facts za mkataba hatuwezi kufanya objections zozote kwa sasa.
Nilichofanya mimi ni kupangua hoja za wanaopinga mradi!
Kwa mfano, Kakoko amesema Wachina wanataka wasemehewe kodi kwa miaka 30! Nimehoji, ni kodi ipi kwa sababu pale bandarini kuna kodi za aina nyingi!!
Aidha, kote duniani zipo kodi unazoweza kusamehewa, na zipo kodi ambazo katu huwezi kusamehewa kwa sababu ni mali ya serikali!!
Sasa huwezi tu kusema wanataka msamaha wa kodi bila kutaja ni kodi zipi!
Sasa kujadili hoja kama hiyo nako kunahitaji kuona mkataba?!
Na katika hilo nimesema wazi, based on case studies za Bandari ya Piraeus, Greece na Hambantota, nimesema wazi kwamba ni kweli Wachina huwa wanataka msamaha wa Income Tax!
Hata hivyo, haiwezekani, mathalani wewe uagize magari na yakapitia Bagamoyo halafu VAT on imported cars ichukuliwe na Wachina... hakuna kitu kama hicho!!!
Sasa hilo nalo linahitaji kusoma mkataba hilo?
Na hata kwenye VAT nimesema wazi Wachina wanaweza kuomba msamaha kwenye imported capital goods zitakazotumika kwenye ujenzi... sasa hilo nalo linahitaji kuona mkataba hilo wakati lipo kwenye sheria ya kodi ya mwaka 2017, 2018, na 2019?!
my concern ni kwanini watu wanampigia sana Chapuo Mchina,
Kama this Port tumekubaliana ni such important kwanini hatu consider kuijenga wenyewe kama nchi ,
Hiyo 10bn dollar hatuwezi kuigawa kwa miaka let say 6 or so tukaijenga wenyewe,
Kama mchina ameweza kukaa kwenye Meza ya mazungumzo Na sisi kwa miaka yote hiyo zaidi ya mitano sasa ,means kuna interest kubwa sana kwake hapa Na dunia sasa kwanini tusigumie hii fursa na sie kuweka hoja zetu zenye faida kwa Taifa then iwe take it or leave it kwa Mchina!?
Ikiwa ni lazima mwekezaji why isiwe kwa ubia or win win situation!?
Mkuu Idugunde , kwanza asante sana kwa hoja hii ya mizigo mingi kupitia Kahama kwa barabara hivyo kuharibu barabara zetu. Mizigo hiyo yote inayopita Kahama kwa malori, inatoka bandari ya Dar, na pale bandarini kuna reli kutoka bandarini hadi bandari kavu ya Isaka. Kwanini hiyo mizigo usisafirishwe na reli mpaka Isaka halafu ndio ikaanzia hapo kwenda Rwanda, Burundi na DRC?.
Wanabodi Kuna msemo usemao "ukiona mwenzako ananyolewa, wewe tia maji tia maji" Tanzania tunajenga reli ya SGR, wenzetu Kenya wametangulia, ila reli yao imeanza kwa kuwa ni a white elephant. Jee kuna haja ya sisi Watanzania tujifunze kwa wenzetu, kuiepusha reli yetu kuwa tembo mweupe, au wao...
www.jamiiforums.com
Tena THA na TRC wakiweza wafufue Bandari Kavu ya Isaka na kuifanya iwe active ili, mizigo yote ya DRC, Rwanda na Burudi, ikishuka tuu Dar Port, inapakiwa straight kwenye SGR, na kwenda Moro na ikifika Moro, inahamishiwa straight reli ya zamani na kupelekwa straight Isaka, malori ya Rwanda, Burundi na DRC yaanzie Isaka.
Bandari ya Mombasa is very busy kwa sababu ya mizigo ya Uganda, Sudan ya Kusini na Tanzania. Hata kama tutaboresha efficiency ya Bandari ya Dar, mizigo yote ya Tanzania itapitia Dar, hivyo bandari yetu ikifanikiwa kwenye hili, mizigo yote ya DRC, Rwanda na Burundi itapita Dar na kuifanya Dar port kuwa the biggest, the busiest na the most profitable kuliko bandari ya Mombasa, lakini bado haiwezi kushibisha SGR ikajiendesha kwa faida, ndio maana wenye kuona mbali, wakaamua tujenge bandari ya kisasa Bagamoyo, na kuziboresha Bandari za Dar, Tanga na Mtwara na ndipo tutakuwa na mzigo wa kutosha kuishibisha SGR na kuiendesha kwa faida. Lakini wakatokea wenye uoni wa mpaka mwisho tuu wa pua zao, wakaambizana eti bandari ya Bagamoyo atafaidi Mkwere, waka abandon hii project.
Upende usipende bandari lazima itajengwa tu: Haya unayoleta wewe ni kelele za mbwa asiye na meno.
Hivyo nimeamua kukupuuza kwasababu nimepima na kuona uko na uelewa finyu mno....
my concern ni kwanini watu wanampigia sana Chapuo Mchina,
Kama this Port tumekubaliana ni such important kwanini hatu consider kuijenga wenyewe kama nchi ,
Hiyo 10bn dollar hatuwezi kuigawa kwa miaka let say 6 or so tukaijenga wenyewe,
Kama mchina ameweza kukaa kwenye Meza ya mazungumzo Na sisi kwa miaka yote hiyo zaidi ya mitano sasa ,means kuna interest kubwa sana kwake hapa Na dunia sasa kwanini tusigumie hii fursa na sie kuweka hoja zetu zenye faida kwa Taifa then iwe take it or leave it kwa Mchina!?
Ikiwa ni lazima mwekezaji why isiwe kwa ubia or win win situation!?
Aidha, issue sio wenyewe kuwa na uwezo wa kuijenga hiyo bandari bali uwezo wa kui-utilize hiyo bandari!
Greece sio wapumbavu walioamua kumwamchia bandari Mchina Bandari ya Piraeus baada ya wao kuona inawashinda licha ya kwamba bandari hiyo ndiyo langu kuu la kuunganisha Asia na Europe!!
Hata kama nchi za Magharibi zinasema Greece hawakuwa na option kutokana na kuelemewa mzigo wa madeni, lakini ukweli bado unabaki pale pale kwamba Piraeus Port haikuwa inafanya vizuri lakini kwavile Mchina ana-handle biashara kubwa sana duniani, hatimae ameweza kuifanya Piraeus Port kuwa tishio Ulaya!!
Mtaleta hoja nyingi zenye kila aina ya rangi lakini hicho unachokitetea hakina tija. Weka kataba wake hapa sio kuleta porojo za utafiti feki na makala zilizojaa hisia binafsi kutokana na maslahi uliyokuwa nayo
Upende usipende bandari lazima itajengwa tu: Haya unayoleta wewe ni kelele za mbwa asiye na meno.
Hivyo nimeamua kukupuuza kwasababu nimepima na kuona uko na uelewa finyu mno....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.