Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Nimeshasema huna hoja, so stop wasting my time!! Huwezi kushindwa kujadili mada eti kisa hakuna mkataba wakati tangu umezaliwa hujawahi kujadili mada yenye mkataba hapa JF!!

Na ikiwa unashindwa kujua hata mambo madogo kama hayo ambayo yameshawekwa wazi tangu zamani, si itakuwa kupotezeana muda tu kuendelea kujadiliana na mtu wa aina yako!
Hoja yako imeegemea upande mmoja.

Unasema huu mradi una faida sana kwetu tofauti na wanavyotuaminisha selikali kwamba mkataba umekaa kinyonyaji.

Tumekuuliza una mkataba tuone jinsi tutakavyofaidika ili tuzidi kuwadharau hawa seilikali? Huna.

Hivyo huu unabaki kuwa upuuzi kama ulivyo upuuzi mwingine tu.
 
Mtaleta hoja nyingi zenye kila aina ya rangi lakini hicho unachokitetea hakina tija. Weka kataba wake hapa sio kuleta porojo za utafiti feki na makala zilizojaa hisia binafsi kutokana na maslahi uliyokuwa nayo
Kama ulivyowahi kuwekewa mkataba na nani, na kwenye project ipi?
 
Nimesoma hii kitu usiku wakati usingizi umekata, strong points which need strong minds kuijadili, bila facts huna sababu ya kupinga hoja za mdau lakini pia bila facts za mkataba hatuwezi kufanya objections zozote kwa sasa.
 
Kwahiyo unataka nianze kujadili yooote aliyofanya JPM, ninayoyaunga na nisiyoyaunga mkono?! Nimekutajia miradi ya JPM ambayo watu wenye chuki nae tumekuwa tunaipinga... mbona unashindwa kuelewa?

Halafu acheni kujificha kwenye mkataba kwa sababu tu hamna hoja!!!

Nimekuuliza, Kakoko aliyewaambia Wachina wanataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, amekuonesha huo mkataba?

Ikiwa hata huko bungeni Wabunge wamekuwa wakililia kupewa mikataba na hawapewi, halafu unataka huo mkataba nikuwekee mimi JF?

Upo serious kujadili mada wewe?!

Hoja zangu zinajadilika bila kuona mkataba kwa sababu ni matokeo ya research!!!
Eti research!

Yani research ni sawa na mkataba?
 
Nimesoma hii kitu usiku wakati usingizi umekata, strong points which need strong minds kuijadili, bila facts huna sababu ya kupinga hoja za mdau lakini pia bila facts za mkataba hatuwezi kufanya objections zozote kwa sasa.
Na ndio hicho wanataka watu mkuu! MKATABA basii..
 
Hoja yako imeegemea upande mmoja.

Unasema huu mradi una faida sana kwetu tofauti na wanavyotuaminisha selikali kwamba mkataba umekaa kinyonyaji.

Tumekuuliza una mkataba tuone jinsi tutakavyofaidika ili tuzidi kuwadharau hawa seilikali? Huna.

Hivyo huu unabaki kuwa upuuzi kama ulivyo upuuzi mwingine tu.
Kwanza kuna kila dalili, hujasoma!!

Nilichofanya mimi ni kupangua hoja za wanaopinga mradi!

Kwa mfano, Kakoko amesema Wachina wanataka wasemehewe kodi kwa miaka 30! Nimehoji, ni kodi ipi kwa sababu pale bandarini kuna kodi za aina nyingi!!

Aidha, kote duniani zipo kodi unazoweza kusamehewa, na zipo kodi ambazo katu huwezi kusamehewa kwa sababu ni mali ya serikali!!

Sasa huwezi tu kusema wanataka msamaha wa kodi bila kutaja ni kodi zipi!

Sasa kujadili hoja kama hiyo nako kunahitaji kuona mkataba?!

Na katika hilo nimesema wazi, based on case studies za Bandari ya Piraeus, Greece na Hambantota, nimesema wazi kwamba ni kweli Wachina huwa wanataka msamaha wa Income Tax!

Hata hivyo, haiwezekani, mathalani wewe uagize magari na yakapitia Bagamoyo halafu VAT on imported cars ichukuliwe na Wachina... hakuna kitu kama hicho!!!

Sasa hilo nalo linahitaji kusoma mkataba hilo?

Na hata kwenye VAT nimesema wazi Wachina wanaweza kuomba msamaha kwenye imported capital goods zitakazotumika kwenye ujenzi... sasa hilo nalo linahitaji kuona mkataba hilo wakati lipo kwenye sheria ya kodi ya mwaka 2017, 2018, na 2019?!
 
my concern ni kwanini watu wanampigia sana Chapuo Mchina,

Kama this Port tumekubaliana ni such important kwanini hatu consider kuijenga wenyewe kama nchi ,
Hiyo 10bn dollar hatuwezi kuigawa kwa miaka let say 6 or so tukaijenga wenyewe,

Kama mchina ameweza kukaa kwenye Meza ya mazungumzo Na sisi kwa miaka yote hiyo zaidi ya mitano sasa ,means kuna interest kubwa sana kwake hapa Na dunia sasa kwanini tusigumie hii fursa na sie kuweka hoja zetu zenye faida kwa Taifa then iwe take it or leave it kwa Mchina!?

Ikiwa ni lazima mwekezaji why isiwe kwa ubia or win win situation!?

Nadhani imefika time tuache kuwa kondoo!
 
Mkuu Idugunde , kwanza asante sana kwa hoja hii ya mizigo mingi kupitia Kahama kwa barabara hivyo kuharibu barabara zetu. Mizigo hiyo yote inayopita Kahama kwa malori, inatoka bandari ya Dar, na pale bandarini kuna reli kutoka bandarini hadi bandari kavu ya Isaka. Kwanini hiyo mizigo usisafirishwe na reli mpaka Isaka halafu ndio ikaanzia hapo kwenda Rwanda, Burundi na DRC?.

Tena THA na TRC wakiweza wafufue Bandari Kavu ya Isaka na kuifanya iwe active ili, mizigo yote ya DRC, Rwanda na Burudi, ikishuka tuu Dar Port, inapakiwa straight kwenye SGR, na kwenda Moro na ikifika Moro, inahamishiwa straight reli ya zamani na kupelekwa straight Isaka, malori ya Rwanda, Burundi na DRC yaanzie Isaka.

Bandari ya Mombasa is very busy kwa sababu ya mizigo ya Uganda, Sudan ya Kusini na Tanzania. Hata kama tutaboresha efficiency ya Bandari ya Dar, mizigo yote ya Tanzania itapitia Dar, hivyo bandari yetu ikifanikiwa kwenye hili, mizigo yote ya DRC, Rwanda na Burundi itapita Dar na kuifanya Dar port kuwa the biggest, the busiest na the most profitable kuliko bandari ya Mombasa, lakini bado haiwezi kushibisha SGR ikajiendesha kwa faida, ndio maana wenye kuona mbali, wakaamua tujenge bandari ya kisasa Bagamoyo, na kuziboresha Bandari za Dar, Tanga na Mtwara na ndipo tutakuwa na mzigo wa kutosha kuishibisha SGR na kuiendesha kwa faida. Lakini wakatokea wenye uoni wa mpaka mwisho tuu wa pua zao, wakaambizana eti bandari ya Bagamoyo atafaidi Mkwere, waka abandon hii project.

P
Good good

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
We ndio huna akili kumsifia mpumbavu anayeandika andiko refu huku hajui anaandika kitu gani. Wote hamna akili ni wapumbavu msio na akili.
Upende usipende bandari lazima itajengwa tu: Haya unayoleta wewe ni kelele za mbwa asiye na meno.
Hivyo nimeamua kukupuuza kwasababu nimepima na kuona uko na uelewa finyu mno....
 
my concern ni kwanini watu wanampigia sana Chapuo Mchina,

Kama this Port tumekubaliana ni such important kwanini hatu consider kuijenga wenyewe kama nchi ,
Hiyo 10bn dollar hatuwezi kuigawa kwa miaka let say 6 or so tukaijenga wenyewe,

Kama mchina ameweza kukaa kwenye Meza ya mazungumzo Na sisi kwa miaka yote hiyo zaidi ya mitano sasa ,means kuna interest kubwa sana kwake hapa Na dunia sasa kwanini tusigumie hii fursa na sie kuweka hoja zetu zenye faida kwa Taifa then iwe take it or leave it kwa Mchina!?

Ikiwa ni lazima mwekezaji why isiwe kwa ubia or win win situation!?

Nadhani imefika time tuache kuwa kondoo!
Issue sio kumpigia chapuo Mchina bali Mchina ndie alijitokeza kutaka kuwekeza Bagamoyo!!

Aidha, issue sio wenyewe kuwa na uwezo wa kuijenga hiyo bandari bali uwezo wa kui-utilize hiyo bandari!

Greece sio wapumbavu walioamua kumwamchia bandari Mchina Bandari ya Piraeus baada ya wao kuona inawashinda licha ya kwamba bandari hiyo ndiyo langu kuu la kuunganisha Asia na Europe!!

Hata kama nchi za Magharibi zinasema Greece hawakuwa na option kutokana na kuelemewa mzigo wa madeni, lakini ukweli bado unabaki pale pale kwamba Piraeus Port haikuwa inafanya vizuri lakini kwavile Mchina ana-handle biashara kubwa sana duniani, hatimae ameweza kuifanya Piraeus Port kuwa tishio Ulaya!!

The same applies to Hambantota Port!!!
 
Eti research!

Yani research ni sawa na mkataba?
Una serious problem, hujijui tu! Na yote hii ni kwa sababu tu suala zima linamhusu JPM, nawe umeapa kumtetea kwa mabaya na mazuri!!

Narudia, suala la kutaka mkataba linathibitisha wazi huna hoja, kwa sababu hoja zangu hazihitaji kuona mkataba!

On top of that, nimekuuliza Kakoko aliyewaambia Mchina anataka asemehe kodi kwa miaka 30, amewaonesha mkataba?
 
Upende usipende bandari lazima itajengwa tu: Haya unayoleta wewe ni kelele za mbwa asiye na meno.
Hivyo nimeamua kukupuuza kwasababu nimepima na kuona uko na uelewa finyu mno....
Unaambiwa jamaa ali-join mada kwa ajili ya kumwaga mitusi tu, basi!!!
 
Mleta mada ndio alisaini?

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Kama hakushiriki katika kusaini na haui kilichokuwemo kwanini anashikia bango jambo asililolijua?

Aliyesaini mkataba huo ni Dr Mary Nagu (Waziri Uwekezaji na Uwezeshaji) mbele ya Rais wa Tanzania J Kikwete na Rais wa China Xi Jinping mwaka 2013.

Acheni kupigia chapuo suala la msingi kama hilo ambalo undani wake hauelewi kinagaubaga
 
Back
Top Bottom