Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Eti kama benefit zina overturn losses. Aisee ivi tutaacha lini kutumia notes za form four ku argue practical matters
Hii ni kama unachoma takataka zenye sumu katikati ya mji. Afu unawaambia watu. Athari ya kiafya haiwezi kuonekana leo itaonekana baada ya miaka kumi. Ila tutakua tumeondoa takataka kwa njia rahisi ambayo ingetugharimu bilioni 500. Hivi kuna kitu kina thamani kwenye maisha kuliko afya yako. Stop that man. Yu wht am talking about
 
When it comes to health matters. We should not pretend as if kila kitu kiko normal. Benefit hazi work out kwenye swala linalohudisha maisha( afya) ya mwananchi.
Kwa hiyo point za darasani zibaki kua hukohuko. Lets come with practical and tangible facts

Pia kuhusu mradi yawezekana tukawa tumeona kama ulivosema lakini in a long run ikawa sivyo.
 
This's business, na hatutakiwi kuongozwa na patriotisms bali with commercial and economic conscious!
How can you separate patriotism with what you term "commercial and economic conscious(ness) as a nation?

Usiwe na kiwewe sana na hiyo hali ya China ilivyo sasa. India ipo hapo, hata wao huwezi kuwadharau jinsi wanavyoinukia haraka, ukiondoa hii corona inayowakabiri wakati huu.

Asia yote ile, siyo China pekee.
Kwa hiyo tulizana, biashara na mataifa mengi tu ipo tele sana. Sio lazima liwe taifa kubwa tu ndipo tuweze kufanya biashara ya maana.
 
China ndiye mwenye kujua thamani ya ujenzi wa hiyo bandari na ndiye aliyeweza kuja na kutaka kuwekeza, hivyo mtoa mada ndiye alivyoweza kuchangia katika yale anayoyajua kutokana na yanayoendelea kuhusu bandari ya Bagamoyo, na waliyopondwa kuwa ni wanyonyaji ni hao wachina hivyo kila mwenye kujua nini kifanyike katika kutoa mchango wa mawazo yake yupo huru
Ni nani "mwenye kujua ni nini kifanyike"?

Nimesoma andiko lako lote sikuelewa una maana gani?
 
Mtanzania mwenye upendo na nchi yake, mwenye kuelewa nini ndicho kina maslahi ya nchi na wananchi, mradi wa Bagamoyo sisi watanzania ndiyo tunaouhitaji hivyo sisi watanzania ndiyo wenye kujua ni nini kifanyike.
 
Nyie hamuhitaji mradi wa bagamoyo. Mmeambiwa na viongozi wenu unamanufaa. Nyie mnataka haki, maji, chakula na elimu bora
 
So yote yanayofanywa na serikali ni kufikia hayo. So its either kwa kujenga bandari au kufanya kitu kingine kitakachotufikisha kwenye mahitaji yetu. Sasa je bagamoyo itatufikisha kwenye chakula, maji, hewa safi, elimu, na haki
 
Mkuu Chige , Thanks for this. Kuna Watanzania wenzetu uwezo wao wa kuona mbali ni mwisho wa pua zao!. Tunajenga SGR, ile treni ina uwezo wa kuvuta mabehewa zaidi ya 100, ya 40ft container zikiwa double, zimepakatana!. SGR ukikamilika, huo mzigo wa kubebwa na SGR ili ijiendeshe kwa faida utatoka wapi?.
Niliuliza hili swali
Sikuwahi kujibiwa!.
Jibu la mzigo wa kuishibisha reli ya SGR ni bandari ya Bagamoyo.
P
Pasco jamaa hayupo leo unabadilisha upepo siyo, Mungu anakuona.
 
Mtanzania mwenye upendo na nchi yake, mwenye kuelewa nini ndicho kina maslahi ya nchi na wananchi, mradi wa Bagamoyo sisi watanzania ndiyo tunaouhitaji hivyo sisi watanzania ndiyo wenye kujua ni nini kifanyike.
Kwani uliponi'quote, ulijua mimi sio mTanzania; na ulijuaje kwamba mimi siupendi mradi huo! Umenisoma popote nikiupinga mradi usijengwe?
 
Nyie hamuhitaji mradi wa bagamoyo. Mmeambiwa na viongozi wenu unamanufaa. Nyie mnataka haki, maji, chakula na elimu bora
Ni kweli tumeambiwa mradi wa Bagamoyo una manufaa na wengine wamesema hauna manufaa ndiyo maana huu mjadala upo barazani, hivyo lete hoja ikiwa tuwape wachina au la au kama kuna rai nyingine itoe.
 
Kwanza, naomba msamaha kama nilisema literature review in proposal. Hapo nimechapia, nilichotaka kusema ni kuwa literature review ni sehemu ya prposal na ni sehemu muhimu ya proposal. Proposal inaandikwa na mtaalamu mwenyewe, kwa sababu yeye ndiyo anayeijuwa concet nzima ya utafiti anaotaka kufanya. Cha ajabu wewe ulikuwa recruited kama research assistant, lakini eti ukawa na jukumu la kuwa na sehemu kubwa katika hiyo proposal ya kuandika lietrature review. Mimi nilichokuuliza ni, je IRB ilikaa na kubariki huo utafiti ambao haukuwa na literature review. Ni mtafiti wa dunia gani atabeba mikoba yake kuja kufanya utafiti ambao proposal haijakamilika na kibali hajapewa cha kuja kufanya utafiti. Ndiyo maana nilikuambia siyo kweli wewe ndiyo mwandishi wa literature review. Kama wewe ni mtafiti huu ukweli unaujuwa. Mtu hawezi kwenda nchi ya kigeni kufanya utafiti ambao haujapitishwa. Ningeandika mengi, lakini huenda naongea na mtu ambaye hata concept ya statement on goals, objectives,utilization...research problem...research question(s), na hypothesis/hypotheses...methodology hajui nini. Ameparamia na kudanganya ameandika literature. Reseach assistants and or data collectors have no room in writing any section on a research proposal.
Say Whaaaaaaaaat!!!!!!!!
Aisee kaka Chige watu mpaka wakuelewe kutakuwa na kazi sana.
 
Ndugu yangu Chige niliahidi ntarudi, lakini naomba nizungumzie kidogo kuhusu hili suala la The Belt-Road-Initiative (BRI). Kwanza kabisa, huu mradi ulianza kupangwa kipindi cha Raisi Hu-Juntao na aliweka wazi kabisa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya chama cha kikomunisti cha Uchina.

Zaidi ya asilimia hamsini (50% of world merchandise) ya bidhaa za dunia hii zinapitia kwenye mfereji wa Malacca ambao ni muhimu sana kwa uchumi na usalama wa dunia. Hali hii inawafanya Uchina wajihisi kwamba lolote linaweza kutokea endepo ukanda wa Pasifiki utachafuka.

Gideon Rachman wa The Financial Times aliwahi kumnukuu moja wa Majemedari wakubwa kabisa wa Marekani akisema hivi "If the Chinese starts war in the Pasific, we will fucking sail those waters and choke them at the Malacca Strait". Mafuta yote yanayoenda Uchina, Vietnam, Japan na Korea kutoka Ghuba ya Uajemi hupitia mfereji wa Malacca.

Hivyo ukibana pale Uchina lazima atahangaika sana ukizingatia yeye ndiye nchi inayoongoza duniani kwa kuingiza mafuta na gesi kutoka nje (Greatest Importer of Oil and Gas). Pia ndiye msafirishaji mkubwa wa bidhaa duniani (The Greatest Exporter of Merchandise): Hivyo anategemea sana mfereji wa Malacca, lakini bahati mbaya sana Marekani ameshafahamu huu udhaifu ndiyo maana anaweka kambi ya jeshi eneo lile.

Uchina hili analiita The Malacca Dilemma, na Peter Navarro mmoja ya washauri wakubwa wa Raisi Donald Trump ameliandika sana kwenye kitabu chake kiitwacho Death by China: Confronting the Dragon-Global Call to Action , akikiri kwamba huu ni moja ya udhaifu ambao Marekani lazima iutumie katika kupambana na Uchina.

SASA TANZANIA INAINGIAJE KWENYE HILI:
Uchina katika kuhangaika na kukwepa hii kadhia akaamua kuja na BRI, ambapo wangefufua The GREAT SILK-ROAD ambayo itapita nchi kavu na baharini. Kama ulivyosema Bandari ya Bagamoyo ilitakiwa ijengwe Kenya na kwenye mkakati wa BRN inainyesha ni LAMU na siyo BAGAMOYO, lakini Mzee Kikwete na Benard Membe wakashawishi ije kujengwa hapa Tanzania.

Sasa lengo ni kwamba Uchina angejenga reli ndefu (Standard Gauge Railway) kutoka Uchina hadi nchini Pakistani ambapo ingekutana na bandari ya Gwadar (Gwadar Port) ambayo itakuwa na ukubwa kama ule wa bandari ya Bagamoyo. Lengo ni kwamba bandari hii itakuwa inapokea bidhaa zote kutoka Ghuba ya Uajemi na kuzipakia kwenye treni hadi Uchina, hivyo kukwepa kupita mfereji wa Malacca.

Hivyo, Bandari za Bagamoyo na Gwadar ndiyo yangekuwa malango makuu ya kuunganisha Bara la Afrika na Asia. Kwasababu Bagamoyo peke yake ingehudumia nchi nyingi sana za Afrika kwasababu ni Special Economic Zone. Pia kuna uwezekano mkubwa sana kama Bandari ya Bagamoyo ingejengwa basi ingeweza kuunganisha hadi Congo DRC, kufika Port Matada kwa njia ya reli na kufanikisha biashara baina ya Africa na Amerika Kusini.

SASA NINI TATIZO:
Watanzania wengi wanapinga sana huu mradi lakini binafsi Feasibility Study nimeiona. Pia waliohusika na kuandaa hii Study mkataba pia waliusona na nikabahatika kufahamu baadhi ya vitu. Inavyofahamika mkataba ni makubaliano ya pande mbili na huwezi kumlazimisha mtu akubali tu hata pale anapata hasara. Kuna mengi yameongelewa sana kuhusu huu mkataba, mengine yana ukweli na mengine ni propaganda zilizoambatana na ujinga wa kutofahamu mambo.

Lakini kubwa zaidi fahamu kwamba ndani ya nchi kumekuwa na kambi mbili zenye minyukano mikubwa sana. Kuna wale Pro-China na Pro-USA, bahati mbaya kuna baadhi ya watu wakubwa nchini wanahusika moja kwa moja na maslahi za hizi kambi (Hili ni jambo la hatari sana kwa usalama wa nchi). Kama tunaangalia maslahi ya kambi hizi mbili bila kuweka Tanzania mbele basi tutakuja kujuta sana huko mbele.

Kumekuwa na fitna, uzandiki na kuumizana sana, ikafika hadi kipindi tukaaminishwa kwamba Mzee Jakaya alikuwa ni mtu mpumbavu na mjinga kupindukia kiasi cha kutaka kuuza nchi yote hii kwa wakoloni wa Kichina na aliyezuia hili lisifanyike ni Mtanzania Mzalendo na Mwenye Uchungu na Nchi hii kuliko raisi mwingine yoyote kuwahi kutoke, Marehemu Raisi Magufuli. Hili kuna watu waliliamini na kuna wengine tulilitilia shaka kwasababu tulibahatika kufahamu kinachoendelea.

Nifahamuvyo mimi ni kwamba Mkataba ni makubaliono ya pande mbili na kama kuna mambo hayakaa vizuri ni vyema kurudi mezani na kufanya juu chini ili kuyazungumza upya. Alichokifanya Raisi Magufuli ni kutafuta umaarufu na kutaka kubagaza watu. Hivyo katika hili ningependa Raisi aunde tume maalumu ya wataalamu wa mikataba wa ndani ya nje ya nchi ambao watatusaidia kupitia vipengele mbalimbali, lakini pia kuajiri QUANTUM ANALYSTS ambao watafanya makadilio ya faida na hasara za kiuchumi ambazo Tanzania itazipata katika kipindi chote cha mkataba.

HILI LINANIKUMBUSHA JAMBO LILILOWAHI KUTOKEA KIPINDI CHA MZEE NYERERE:
Wakati Mzee Nyerere anataka kujenga TAZARA aliwafuata Wamarekani na wakasema ile reli ingejengwa kwa miaka 20. Kuna wataalamu wetu walipigia sana hili jambo chapuo lakini akaamua kwenda Uchina wakasema wangejenga kwa miaka 5. Mao Zedong na Zhou Enlai walimwambia Mzee Nyerere wewe ni rafiki yetu na sisi wote ni masikini, lakini mahitaji yetu na yenu ni tofauti hivyo tutawasaidia kujenga reli.

Marekani, Urusi, Uingereza na Ujerumani walipinga sana huu mradi kufanywa. Wale wahandisi walifanya uchunguzi ambapo walitembea kwa mguu kwa zaidi ya miezi tisa wakiangalia sehemu ambayo reli ingepita. Waziri Mkuu wa Uingereza bwana Harold Wilson alimwambia Nyerere kwamba mashirika ya ujasisi yamefanya uchunguzi na kufahamu kwamba mawaziri wengi wa Nyerere kama Mohamed Babu, Prof. Ibrahimu Kaduma na wengine ni majasusi wa Uchina na wanalipwa na Uchina ili kuuiza Tanzania.

Ilipingwa kampeni kubwa ambayo ilifika kipindi wakasema kwamba Tanzania inaenda kuwa koloni la Uchina. Baadhi ya wasomi wa Tanzania wa wakati huo walikubali na kuamini zile propaganda. Tofauti na Mzee Magufuli, Raisi Nyerere alikuwa ni Shrewd Statesman and an Excellent Diplomat with a clear understanding of global politics. Aliamua reli ijengwe na akasema yeye anachotaka ni pesa hajali kama ni Nyekundu kutoka kwa Wakomunisti au Bluu kutoka kwa Mabepari.

KITU AMBACHO WENGI HAWAKIFAHAMU:
Wakati reli inajengwa wamarekani walitumia vyombo vya habari na wataalamu kukashifu na kusema kwamba ile reli haitakuwa na kiwango cha ubora kama reli za Ulaya na Marekani. Wengi waliikashifu TAZARA kwa kuiita reli ya mwanzi (The Bamboo Railway): Yule Muhandisi wa kichina aliyesimamia Ujenzi wa reli na wenzake walishawahi kuvamiwa na majasusi wa Marekani hadi kupigana makonde wakati wa ujenzi wa ile reli.

SHIDA IKO WAPI SASA ???:
Nasema kwa ujasiri na uhakika mkubwa kabisa kwamba wasomi wa kitanzania walioko kwenye vyama vya siasa, jeshi na kwenye idara zetu za ujasusi na upelelezi ni watu ambao hawana uelewe mpana wa mambo. Watanzania wengi hatuna kumbukumbu ya nchi hii imetokea wapi na imefikaje hapa zaidi ya kupeana taarifa za kusimuliana tu. Hatufahamu dunia inaendaje na jinsi gani mwenendo huu wa dunia unaweza kuathiri siasa za nchi changa kama Tanzania. Pia hatufahamu wapi nchi yetu inaenda na hatuna kabisa uhakika wa taswira ya nchi yetu kwa miaka 20 ijayo.

Huwa najiuliza sana kama Mzee Nyerere angekuwa na roho nyepesi na hana uelewa mpana wa mambo sidhani kama leo hii Tanzania ingekuwa na reli ya TAZARA, sidhani. Nilimsikia Bwana Kakoko akisema kwamba Uchina ya leo siyo Uchina ile ya kipindi cha TAZARA na nikapata uhakika wa hicho nilichokisema hapo juu, cha kukosa uelewa wa siasa za dunia. AU Aidha Kakoko alikuwa anafahamu lakini akaamua kupiga Propaganda, lakini yote tisa mimi ambaye nimesoma Political Science and Diplomacy nikaamua kumsamehe kwasababu huenda hana utaalamu na haya mambo.

Ila nachokifahamu ni kwamba UCHINA alijenga TAZARA siyo kwasababu ya kusaidia wajamaa wenzake wa kiafrika peke yake, bali aliangalia maslahi ya kiuchumi ya miaka zaidi ya 40 mbele. Kama watanzania wanaamini kwamba ile reli ilikuwa ni zawadi kutoka kwa mjomba basi nawashauri waache kufikiri huo ujinga kuanzia leo. Uchina na Urusi wote walitoa misaada kwasababu ilifanikisha ajenda zao za kisiasa, kiusalama na kidiplomasia. TAZARA imemsaidia sana Uchina kidiplomasia, kiuchumi na kiusalama kama ambavyo Bagamoyo itamsaidia. Hivyo Uchina wa kipindi kile na Uchina wa leo ni walewale wale na hawajawahi badilika, kama mnadhani duniani kuna FREE-LUNCH basi mnajidanganya.

NINI KIFANYIKE SASA ???:
Katika pilika zangu za kusoma migogoro ya kimataifa, uwekezaji na kuifanyia kazi nimefahamu kitu kimoja cha msingi sana. Ili migogoro itatuliwe vizuri ni lazima kuwe na CONFIDENTIALITY, ili kusaidia Political Passion of Citizens zisivuruge kabisa majadiliano. Naamini hili suala lingekuwa wazi kuishia ngazi za Bunge tu, ambapo kamati za Bunge zingepewa mamlaka kulijadili na siyo kila raia ambaye hana hata ufahamu nalo akalizungumzia.

Sasa ili kukata mzizi wa fitina na kusaidia nchi isonge mbele Raisi angeunda tume huru ya uchunguzi (Commission of Inquiry) ya wataalamu ambayo itahusika na kupitia mkataba wa Bandari ya Bagamoyo. Tena ili kuhakikisha weledi Raisi atafute wasomi nguli hata wa nje ili kusiadia kuifanyia Consultancy hiyo Tume: Lakini pia maadamu watu walioandaa huo mkataba kipindi cha awamu ya Mzee Kikwete bado wapo basi waitwe na hiyo tume wahojiwe na watoe sababu za kwanini wao kukubaliana na ule mkataba.

Pia maadamu timu ya wataalamu wa kipindi cha utawala wa Raisi Magufuli waliomshauri akatae ule mradi kwasababu mkataba ni wa hovyo, kijinga na kifisadi bado wapo nao waitwe na tume na kutoa sababu zao. Mwisho wa siku tume ipimie nani anasema ukweli , wapi tumekwama na watoea mapendekezo ya jinsi mkataba unaweza kutekelezwa kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili (Tanzania na Uchina).

Siku zote kukiwa na utata wa namna hii njia pekee ni kuunda COMMISSION OF INQUIRY ya wataalamu ili kupima hoja zinazotolewa na pande zote mbili. Kitaalamu kama jambo limetokea na kila pande inasema kitu chake, tume za namna hii huundwa ili kutafuta ukweli ni upi, na mwisho huishia kutoa mapendekezo ya kitaalamu. Sasa nadhani suala nyeti kama hili linaweza kumalizwa na wataalamu siyo wanasiasa wasio na ufahamu wowote kuhusu hili jambo.

Mwisho kabisa Raisi na Bunge wapelekewe hiyo ripoti ya uchunguzi ili wao washauriane na kufanya maamuzi sahihi. Aidha tunaukataa huu mradi au tunaukubali: Hili la kusema eti mradi mzuri ila mkataba mbaya hatuyataki. Tukiendelea kwenda hivi gizani na kutegemea kauli za wanasiasa basi ukweli hatutaufahamu kamwe na hujuma na uzandiki vitaendelea.......

RAI YANGU KWA WASOMI WA KITANZANIA:
Mbali na maslahi ya kiuchumi ya Tanzania kuhusishwa, huu ni mtifuano mkubwa sana wa kimataifa ambao haukuanza leo wala jana. Nadhani kabla ya kukosoa, kukubali au kupinga ni vyema tukawa na taarifa sahihi kwanza. Pia tufahamu kabisa huu mradi ukijengwa au kukataliwa ni faida au hasara kwa haya mataifa mawili makubwa: Hivyo tusichague tuweke nchi yetu mbele kwanza na tupate taarifa sahihi ili kuepuka kutumika kisiasa bila kufahamu.
 
Ndugu yangu Chige niliahidi ntarudi, lakini naomba nizungumzie kidogo kuhusu hili suala la The Belt-Road-Initiative (BRI). Kwanza kabisa, huu mradi ulianza kupangwa kipindi cha Raisi Hu-Juntao na aliweka wazi kabisa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya chama cha kikomunisti cha Uchina.

Zaidi ya asilimia hamsini (50% of world merchandise) ya bidhaa za dunia hii zinapitia kwenye mfereji wa Malacca ambao ni muhimu sana kwa uchumi na usalama wa dunia. Hali hii inawafanya Uchina wajihisi kwamba lolote linaweza kutokea endepo ukanda wa Pasifiki utachafuka.

Gideon Rachman wa The Financial Times aliwahi kumnukuu moja wa Majemedari wakubwa kabisa wa Marekani akisema hivi "If the Chinese starts war in the Pasific, we will fucking sail those waters and choke them at the Malacca Strait". Mafuta yote yanayoenda Uchina, Vietnam, Japan na Korea kutoka Ghuba ya Uajemi hupitia mfereji wa Malacca.

Hivyo ukibana pale Uchina lazima atahangaika sana ukizingatia yeye ndiye nchi inayoongoza duniani kwa kuingiza mafuta na gesi kutoka nje (Greatest Importer of Oil and Gas). Pia ndiye msafirishaji mkubwa wa bidhaa duniani (The Greatest Exporter of Merchandise): Hivyo anategemea sana mfereji wa Malacca, lakini bahati mbaya sana Marekani ameshafahamu huu udhaifu ndiyo maana anaweka kambi ya jeshi eneo lile.

Uchina hili analiita The Malacca Dilemma, na Peter Navarro mmoja ya washauri wakubwa wa Raisi Donald Trump ameliandika sana kwenye kitabu chake kiitwacho Death by China: Confronting the Dragon-Global Call to Action , akikiri kwamba huu ni moja ya udhaifu ambao Marekani lazima iutumie katika kupambana na Uchina.

SASA TANZANIA INAINGIAJE KWENYE HILI:
Uchina katika kuhangaika na kukwepa hii kadhia akaamua kuja na BRI, ambapo wangefufua The GREAT SILK-ROAD ambayo itapita nchi kavu na baharini. Kama ulivyosema Bandari ya Bagamoyo ilitakiwa ijengwe Kenya na kwenye mkakati wa BRN inainyesha ni LAMU na siyo BAGAMOYO, lakini Mzee Kikwete na Benard Membe wakashawishi ije kujengwa hapa Tanzania.

Sasa lengo ni kwamba Uchina angejenga reli ndefu (Standard Gauge Railway) kutoka Uchina hadi nchini Pakistani ambapo ingekutana na bandari ya Gwadar (Gwadar Port) ambayo itakuwa na ukubwa kama ule wa bandari ya Bagamoyo. Lengo ni kwamba bandari hii itakuwa inapokea bidhaa zote kutoka Ghuba ya Uajemi na kuzipakia kwenye treni hadi Uchina, hivyo kukwepa kupita mfereji wa Malacca.

Hivyo, Bandari za Bagamoyo na Gwadar ndiyo yangekuwa malango makuu ya kuunganisha Bara la Afrika na Asia. Kwasababu Bagamoyo peke yake ingehudumia nchi nyingi sana za Afrika kwasababu ni Special Economic Zone. Pia kuna uwezekano mkubwa sana kama Bandari ya Bagamoyo ingejengwa basi ingeweza kuunganisha hadi Congo DRC, kufika Port Matada kwa njia ya reli na kufanikisha biashara baina ya Africa na Amerika Kusini.

SASA NINI TATIZO:
Watanzania wengi wanapinga sana huu mradi lakini binafsi Feasibility Study nimeiona. Pia waliohusika na kuandaa hii Study mkataba pia waliusona na nikabahatika kufahamu baadhi ya vitu. Inavyofahamika mkataba ni makubaliano ya pande mbili na huwezi kumlazimisha mtu akubali tu hata pale anapata hasara. Kuna mengi yameongelewa sana kuhusu huu mkataba, mengine yana ukweli na mengine ni propaganda zilizoambatana na ujinga wa kutofahamu mambo.

Lakini kubwa zaidi fahamu kwamba ndani ya nchi kumekuwa na kambi mbili zenye minyukano mikubwa sana. Kuna wale Pro-China na Pro-USA, bahati mbaya kuna baadhi ya watu wakubwa nchini wanahusika moja kwa moja na maslahi za hizi kambi (Hili ni jambo la hatari sana kwa usalama wa nchi). Kama tunaangalia maslahi ya kambi hizi mbili bila kuweka Tanzania mbele basi tutakuja kujuta sana huko mbele.

Kumekuwa na fitna, uzandiki na kuumizana sana, ikafika hadi kipindi tukaaminishwa kwamba Mzee Jakaya alikuwa ni mtu mpumbavu na mjinga kupindukia kiasi cha kutaka kuuza nchi yote hii kwa wakoloni wa Kichina na aliyezuia hili lisifanyike ni Mtanzania Mzalendo na Mwenye Uchungu na Nchi hii kuliko raisi mwingine yoyote kuwahi kutoke, Marehemu Raisi Magufuli. Hili kuna watu waliliamini na kuna wengine tulilitilia shaka kwasababu tulibahatika kufahamu kinachoendelea.

Nifahamuvyo mimi ni kwamba Mkataba ni makubaliono ya pande mbili na kama kuna mambo hayakaa vizuri ni vyema kurudi mezani na kufanya juu chini ili kuyazungumza upya. Alichokifanya Raisi Magufuli ni kutafuta umaarufu na kutaka kubagaza watu. Hivyo katika hili ningependa Raisi aunde tume maalumu ya wataalamu wa mikataba wa ndani ya nje ya nchi ambao watatusaidia kupitia vipengele mbalimbali, lakini pia kuajiri QUANTUM ANALYSTS ambao watafanya makadilio ya faida na hasara za kiuchumi ambazo Tanzania itazipata katika kipindi chote cha mkataba.

HILI LINANIKUMBUSHA JAMBO LILILOWAHI KUTOKEA KIPINDI CHA MZEE NYERERE:
Wakati Mzee Nyerere anataka kujenga TAZARA aliwafuata Wamarekani na wakasema ile reli ingejengwa kwa miaka 20. Kuna wataalamu wetu walipigia sana hili jambo chapuo lakini akaamua kwenda Uchina wakasema wangejenga kwa miaka 5. Mao Zedong na Zhou Enlai walimwambia Mzee Nyerere wewe ni rafiki yetu na sisi wote ni masikini, lakini mahitaji yetu na yenu ni tofauti hivyo tutawasaidia kujenga reli.

Marekani, Urusi, Uingereza na Ujerumani walipinga sana huu mradi kufanywa. Wale wahandisi walifanya uchunguzi ambapo walitembea kwa mguu kwa zaidi ya miezi tisa wakiangalia sehemu ambayo reli ingepita. Waziri Mkuu wa Uingereza bwana Harold Wilson alimwambia Nyerere kwamba mashirika ya ujasisi yamefanya uchunguzi na kufahamu kwamba mawaziri wengi wa Nyerere kama Mohamed Babu, Prof. Ibrahimu Kaduma na wengine ni majasusi wa Uchina na wanalipwa na Uchina ili kuuiza Tanzania.

Ilipingwa kampeni kubwa ambayo ilifika kipindi wakasema kwamba Tanzania inaenda kuwa koloni la Uchina. Baadhi ya wasomi wa Tanzania wa wakati huo walikubali na kuamini zile propaganda. Tofauti na Mzee Magufuli, Raisi Nyerere alikuwa ni Shrewd Statesman and an Excellent Diplomat with a clear understanding of global politics. Aliamua reli ijengwe na akasema yeye anachotaka ni pesa hajali kama ni Nyekundu kutoka kwa Wakomunisti au Bluu kutoka kwa Mabepari.

KITU AMBACHO WENGI HAWAKIFAHAMU:
Wakati reli inajengwa wamarekani walitumia vyombo vya habari na wataalamu kukashifu na kusema kwamba ile reli haitakuwa na kiwango cha ubora kama reli za Ulaya na Marekani. Wengi waliikashifu TAZARA kwa kuiita reli ya mwanzi (The Bamboo Railway): Yule Muhandisi wa kichina aliyesimamia Ujenzi wa reli na wenzake walishawahi kuvamiwa na majasusi wa Marekani hadi kupigana makonde wakati wa ujenzi wa ile reli.

SHIDA IKO WAPI SASA ???:
Nasema kwa ujasiri na uhakika mkubwa kabisa kwamba wasomi wa kitanzania walioko kwenye vyama vya siasa, jeshi na kwenye idara zetu za ujasusi na upelelezi ni watu ambao hawana uelewe mpana wa mambo. Watanzania wengi hatuna kumbukumbu ya nchi hii imetokea wapi na imefikaje hapa zaidi ya kupeana taarifa za kusimuliana tu. Hatufahamu dunia inaendaje na jinsi gani mwenendo huu wa dunia unaweza kuathiri siasa za nchi changa kama Tanzania. Pia hatufahamu wapi nchi yetu inaenda na hatuna kabisa uhakika wa taswira ya nchi yetu kwa miaka 20 ijayo.

Huwa najiuliza sana kama Mzee Nyerere angekuwa na roho nyepesi na hana uelewa mpana wa mambo sidhani kama leo hii Tanzania ingekuwa na reli ya TAZARA, sidhani. Nilimsikia Bwana Kakoko akisema kwamba Uchina ya leo siyo Uchina ile ya kipindi cha TAZARA na nikapata uhakika wa hicho nilichokisema hapo juu, cha kukosa uelewa wa siasa za dunia. AU Aidha Kakoko alikuwa anafahamu lakini akaamua kupiga Propaganda, lakini yote tisa mimi ambaye nimesoma Political Science and Diplomacy nikaamua kumsamehe kwasababu huenda hana utaalamu na haya mambo.

Ila nachokifahamu ni kwamba UCHINA alijenga TAZARA siyo kwasababu ya kusaidia wajamaa wenzake wa kiafrika peke yake, bali aliangalia maslahi ya kiuchumi ya miaka zaidi ya 40 mbele. Kama watanzania wanaamini kwamba ile reli ilikuwa ni zawadi kutoka kwa mjomba basi nawashauri waache kufikiri huo ujinga kuanzia leo. Uchina na Urusi wote walitoa misaada kwasababu ilifanikisha ajenda zao za kisiasa, kiusalama na kidiplomasia. TAZARA imemsaidia sana Uchina kidiplomasia, kiuchumi na kiusalama kama ambavyo Bagamoyo itamsaidia. Hivyo Uchina wa kipindi kile na Uchina wa leo ni walewale wale na hawajawahi badilika, kama mnadhani duniani kuna FREE-LUNCH basi mnajidanganya.

NINI KIFANYIKE SASA ???:
Katika pilika zangu za kusoma migogoro ya kimataifa, uwekezaji na kuifanyia kazi nimefahamu kitu kimoja cha msingi sana. Ili migogoro itatuliwe vizuri ni lazima kuwe na CONFIDENTIALITY, ili kusaidia Political Passion of Citizens zisivuruge kabisa majadilioano. Naamini hili suala lingekuwa wazi lakini lingeishia ngazi za Bunge ambapo kamati za Bunge zingepewa mamlaka kulizungumzia na siyo kila raia ambaye hana hata ufahamu nalo akalizungumzia.

Sasa ili kukata mzizi wa fitina na kusaidia nchi isonge mbele Raisi angeunda tume huru (Commission of Inquiry) ya wataalamu ambayo itahusika na kupitia mkataba wa Bandari ya Bagamoyo. Tena ili kuhakikisha weledi Raisi atafute wasomi nguli hata wa nje ili kusiadia kuifanyia Consultancy hiyo Tume: Lakini pia maadamu watu walioandaa huo mkataba kipindi cha awamu ya Mzee Kikwete bado wapo basi waitwe na hiyo tume wahojiwe na watoe sababu za wao kukubaliana na ule mkataba.

Pia maadamu timu ya wataalamu wa kipindi cha utawala wa Raisi Magufuli waliomshauri akatae ule mradi kwasababu mkataba ni wa hovyo, kijinga na kifisadi bado wapo nao waitwe na tume na kutoa sababu zao. Mwisho wa siku tume iangalie nani anasema ukweli, wapi tumekwamba na watoea mapendekezo ya jinsi wanataka mkataba uwe kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili.

Mwisho kabisa Raisi na Bunge wapelekewe hiyo ripoti ili wafanye maamuzi sahihi, aidha tunaukataa huu mradi au tunaukubali. Lakini tukiendelea kwenda hivi gizani ukweli hatutaufahamu kamwe na hujuma na uzandiki vitaendelea.......

RAI YANGU KWA WASOMI WA KITANZANIA:
Mbali na maslahi ya kiuchumi ya Tanzania kuhusishwa, huu ni mtifuano mkubwa sana wa kimataifa ambao haukuanza leo wala jana. Nadhani kabla ya kukosoa, kukubali au kupinga ni vyema tukawa na taarifa sahihi kwanza. Pia tufahamu kabisa huu mradi ukijengwa au kukataliwa ni faida au hasara kwa haya mataifa mawili makubwa: Hivyo tusichague tuweke nchi yetu mbele kwanza na tupate taarifa sahihi ili kuupa kutumika kisiasa bila kufahamu.
Naunga mkono hoja[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA,

I'm speechless! What a comprehensive piece of information!

Na kama ambavyo ulivyosema kuhusu kumsamehe Kakoko kwavile huenda hana utalaamu na hayo uliyosema, ndipo nami kwa upande mwingine nikajiaminisha hivyo kwa jinsi alivyokuwa ameliongelea suala la kodi!

Nikajiaminisha ama ameamua tu kutumika na kupiga propaganda, au hana uelewa na masuala ya kodi hasa kwa kuzingatia yeye ni mhandisi.

Aidha, nakubaliana na wewe kwa mapendekezo yako, manake hata nami nimeshaur serikali ikae na wadau kujadili hili suala kwa mapana na marefu.

Aidha umegusia hili suala:-
Hivyo, Bandari za Bagamoyo na Gwadar ndiyo yangekuwa malango makuu ya kuunganisha Bara la Afrika na Asia. Kwasababu Bagamoyo peke yake ingehudumia nchi nyingi sana za Afrika kwasababu ni Special Economic Zone. Pia kuna uwezekano mkubwa sana kama Bandari ya Bagamoyo ingejengwa basi ingeweza kuunganisha hadi Congo DRC, kufika Port Matada kwa njia ya reli na kufanikisha biashara baina ya Africa na Amerika Kusini.
Nchi nyingi za Afrika along Atlantic Ocean zina miradi ya bandari ya Mchina! Aidha zipo shipping lanes kutoka South America kwenda China zinazopitia Cape of Good Hope in SA na pale zinatawanyika. Aidha, zipo shipping lane zinazotoka hadi US East Coast to South America, Cape of Good Hope, na kutokea hapo zinatawanyika kuelekea China na nchi zingine za Mashariki ya Mbali.

Kwa kuangalia hizo shipping lane, na kama Bandari ya Bagamoyo ingejengwa kama ilivyokuwa imekudiwa, hiyo biashara uliyoisema ni kweli isingekwepeka!

Meli zisingekuwa na sababu ya kutoka South America to China or Singapore ilipo transshipment port wakati hapa njiani kuna bandari nyingine inayoweza kufanya hivyo. Na licha ya China kuwa na port projects across Africa of Atlantic Ocean, hakuna hata moja inayofikia angalau nusu ya Bagamoyo Project!

Hiyo inaonesha wazi lengo la Mchina ni kufanya Bandari ya Bagamoyo kuwa makutano ya meli kutoka Amerika ya Kusini na Western Africa!!!

Unajua nilishtuka sana na mpango wa Portside Industrial City ambao ukikamilika, mradi utakuwa na uwezo wa kuwa na wastani wa viwanda 700!!

Nikajiuliza, kama plan zao ndo hizo, mbona mradi utakuwa mkubwa sana, hasa nikizingatia viwanda hivi havitakuwa vile vya "Tanzania ya Viwanda" ambavyo, ukiweka mashine ya kusaga unahesabiwa Kiwanda cha Usindikaji wa Nafaka!!

Sasa ulipozungumzia Malacca Strait, now it makes sense, kwa sababu if anything happens, anaweza kuitumia Bagamoyo portside industrial city kama Chinese's Satellite Manufacturing City! Lakini kwa upande mwingine, pamoja na macho na ngozi zao kufanana, Singapore is more of America as compared to China!

What a genius move kuamua kujenga reli from China to Pakistan!

Lakini hata ukiacha hii minyukano ya kimataifa, kwa upande mwingine Malacca Strait ipo occupied sana miaka ya karibuni, kiasi cha kuifanya Singapore Port wakati mwingine kuelemewa na meli zinazofaulisha shehena. Kwa mfano, ni mwezi mmoja t uliopita zilitolewa habari kuhusu bandari hiyo kuwa na msongamano wa meli, kiasi kwamba wastani umeongezeaka kutoka meli 17 hadi 49 kwa siku ambazo zinakaa bandarini hapo kwa zaidi ya siku mbili!

Na huu ubize uliopo pale Bandari ya Singapore ndio unaweza kuzifanya baadhi ya meli from/to Atlantic Ocean kuishia Bagamoyo, na kufaulisha mizigo hapo!
 
Issue ya bagamoyo project hakuna alieikataa ila tuliambiwa na mkuu wa nchi awamu ya tano kwamba una mashart magumu mno ambayo hayana tija kwa nchi yetu. So la msingi ni kwamba upelekwe bungeni watu wausome na waujadili kwa kina then wananchi nasi tuwe kwenye tv tufanye analysis zetu pia.

Wewe mwenyewe umeanza kuleta mada baada ya hayati JPM kututoka na kamishina wa bandari pia keshatimuliwa. So kwanini hoja kama hii hukuibua kipindi kile maana najua kile chuma kingejibu hadharani na kingeuleta mkataba tena hata kwa press conference.so kusubiri hawa watu wawili kutokuwepo na kuleta mada ni kama inaegemea upande mmoja the best way ni kupelekwa bungeni.

Wewe mwenyewe unaleta uthibitisho wa mchina tu huleti screenshot za mkataba na pia haiingii akilini kutetea kitu ambacho hujakiona. So kama umeusoma tunauomba tuuone. Na kama hukuusoma its bull shit.

Pia ulivyohitimisha wewe mwenyewe haujaunga mkono 100%.it means na wewe pia unamashaka nao.
 
Uko sahihi, ila moja iangalie kwa jicho la tano, wazungu walioajiriwa ndio ilikua kivutio na kuunganisha pande 2 ili zifanye biashara tz wanasubiri nini kutumia hata advantage moja tu waliyonayo
Sikatai hilo suala la Wazungu! Ninachosema ni kwamba, kikubwa kabisa kilichosaidia China ni kwa wao kuwa na soko kubwa ambalo sisi hatuna! REMEMBER, kwa sasa, population ya China now is almost 1.4 Billion.

Hili soko kubwa likavutia kampuni mbalimbali kutoka developed world na kwenda kuwekeza China! Hizi kampuni automatically zikaingiza teknolojia nchini China, na kwavile kampuni husika zilikuwa zinaajiri Wachina, hapo ikawa ni rahisi zaidi kwa China kupata uzoefu wa hii teknolojia iliyoletwa na Wawekezaji!!!

Na hiyo ndo faida kubwa ya FDI! Sio tu inaleta capital bali inafanya technology transfer kutoka huko kwao na kupeleka kule wanakoenda kuwekeza!

Kingine kilichowasaidia ni kile ambacho hadi kesho ndio kimekuwa chanzo kikuu cha ugomvi kati ya China na US... Industrial Espionage. Aidha, Wachina wanawekeza sana kwenye tech starts-up in the US!

Sasa turudi kwa Tanzania kwa kufuata ushauri wako!

Hao Wazungu watakaowezesha tech transfer tutawaajiri kwenye sekta wakati taasisi za kibiashara zipo chini ya sekta ya binafsi?! NI rahisi kwa sisi kuvutia FDI ambayo ndiyo itachochea hiyo tech transfer kuliko sisi kuajiri Wazungu!
 
Issue ya bagamoyo project hakuna alieikataa ila tuliambiwa na mkuu wa nchi awamu ya tano kwamba una mashart magumu mno ambayo hayana tija kwa nchi yetu. So la msingi ni kwamba upelekwe bungeni watu wausome na waujadili kwa kina then wananchi nasi tuwe kwenye tv tufanye analysis zetu pia.

Wewe mwenyewe umeanza kuleta mada baada ya hayati JPM kututoka na kamishina wa bandari pia keshatimuliwa. So kwanini hoja kama hii hukuibua kipindi kile maana najua kile chuma kingejibu hadharani na kingeuleta mkataba tena hata kwa press conference.so kusubiri hawa watu wawili kutokuwepo na kuleta mada ni kama inaegemea upande mmoja the best way ni kupelekwa bungeni.

Wewe mwenyewe unaleta uthibitisho wa mchina tu huleti screenshot za mkataba na pia haiingii akilini kutetea kitu ambacho hujakiona. So kama umeusoma tunauomba tuuone. Na kama hukuusoma its bull shit.

Pia ulivyohitimisha wewe mwenyewe haujaunga mkono 100%.it means na wewe pia unamashaka nao.
Mosi, unachekesha sana!!!

FYI, nimeanza kuandika issue ya Bandari ya Bagamoyo for over 5 years now! Yaani kwavile wewe na wenzako mlikuwa mnamuogopa huyo Jiwe ndo mnadhani kila mtu alikuwa anashindwa kwa kumuogopa yeye... VERY FUNNY!

Kwamba ndo maana mimi mwenyewe sijaunga kwa 100%; kwani hiyo serikali imeukataa kwa 100%?! Hivi unaelewa unapoambiwa kuna mambo wamekubaliana na kuna mambo hawajakubaliana?!

Nikupe screenshot ya mkataba wakati nimeshasema bado majadiliano yanaendelea na hakuna mkataba uliosainiwa hasi sasa! Btw, unanitaka nikuoneshe mkataba, hao waliokuambia mkataba ni wa kinyonyaji wamekuonesha huo mkataba?!

Kwamba Chuma kingeleta mkataba kwenye conference... huyu ndugu yangu unafahamu jinsi serikali yako inavyoendesha mambo yake?! Tangu umeingia JF, umewahi kuiona mikataba mingapi hapa JF?! Ina maana hujawahi kuwasikia hata Wabunge wanavyoilalamikia serikali jinsi inavyofanya mikataba kuwa siri?
 
How can you separate patriotism with what you term "commercial and economic conscious(ness) as a nation?
Nimeweka wazi kuhusu hao patriots!! Wazalendo wa Magufuli, ambao kimsingi, majority hawana uzalendo wowote!! Nyie hamna uzalendo wa kumzidi Mchina lakini bado alifahamu umuhimu kama sio ulazima wa FDI! Wala hawakusema "tuna soko kubwa kwahiyo kama viwanda tutajenga wenyewe"! Wao waliongozwa na commercial mind, na sio ule uzaleno uliopitwa na wakati wa "Madini hayaozi"!
Usiwe na kiwewe sana na hiyo hali ya China ilivyo sasa. India ipo hapo, hata wao huwezi kuwadharau jinsi wanavyoinukia haraka, ukiondoa hii corona inayowakabiri wakati huu.
Another misunderstanding!

Kwani Marekani si bonge la tajiri?!

Hapo issue sio nchi hii na ile na zenyewe ni tajiri bali ni nchi ipi ipo tayari ku-offer nini!!! Hao Wahindi kwa sasa tusubiri tu waje kununua mbaazi zetu!!
Asia yote ile, siyo China pekee.
Kwa hiyo tulizana, biashara na mataifa mengi tu ipo tele sana. Sio lazima liwe taifa kubwa tu ndipo tuweze kufanya biashara ya maana.
Kwahiyo hizo nchi zingine ndo zitajali sana maslahi ya Tanzania?!
 
Sikatai hilo suala la Wazungu! Ninachosema ni kwamba, kikubwa kabisa kilichosaidia China ni kwa wao kuwa na soko kubwa ambalo sisi hatuna! REMEMBER, kwa sasa, population ya China now is almost 1.4 Billion.

Hili soko kubwa likavutia kampuni mbalimbali kutoka developed world na kwenda kuwekeza China! Hizi kampuni automatically zikaingiza teknolojia nchini China, na kwavile kampuni husika zilikuwa zinaajiri Wachina, hapo ikawa ni rahisi zaidi kwa China kupata uzoefu wa hii teknolojia iliyoletwa na Wawekezaji!!!

Na hiyo ndo faida kubwa ya FDI! Sio tu inaleta capital bali inafanya technology transfer kutoka huko kwao na kupeleka kule wanakoenda kuwekeza!

Kingine kilichowasaidia ni kile ambacho hadi kesho ndio kimekuwa chanzo kikuu cha ugomvi kati ya China na US... Industrial Espionage. Aidha, Wachina wanawekeza sana kwenye tech starts-up in the US!

Sasa turudi kwa Tanzania kwa kufuata ushauri wako!

Hao Wazungu watakaowezesha tech transfer tutawaajiri kwenye sekta wakati taasisi za kibiashara zipo chini ya sekta ya binafsi?! NI rahisi kwa sisi kuvutia FDI ambayo ndiyo itachochea hiyo tech transfer kuliko sisi kuajiri Wazungu!
Nimekuelewa kwa upande mmoja ila bado kuna siri unashindwa kuiona amabayo sio ya kisomi ni maarifa na utambuzi, idadi ya china na india ziko sawa, na wazungu walianza uhusiano na india kabla ya china, china wakatumia hio nafasi ya kuajiri wazungu, wakapata ushauri na wakautumia, na kati ya ushauri huo ni kuondoa kuweka kiwango cha chini cha kodi na chache, kutotumia nguvu kwa wafanya biashara hata kama wamekosea, kutowafilisi wawekezaji, kuruhusu wazungu kuingia na kufanya kazi bila usumbufu, kutumia mazungungumzo ktk kila nyanja na mambo mengine. Hata Singapore walitumia njia hii na unaona waliko sasa. FDI bila hayo hapo juu haiwezi fanikiwa kwani ndio njia ilitumika kipindi cha mkapa na ilishindwa, lazima Kiongozi number moja awe na washauri kutoka kule pesa na tekinologia inakotoka ili kumsaidia kujua namna ya kufanikisha mission yake. us inahangaika sasa kwa sababu master mind wa china ni wamarekani ambao wanalipwa vizuri na china
 
Back
Top Bottom