Mabinti Hawa majasiri wamenikosha sana, Mungu awabariki sana

Mabinti Hawa majasiri wamenikosha sana, Mungu awabariki sana

Fanya urudi bongo ujionee si ulisema upo USA, baba anauza vikapu ana mke na watoto wanne, anatembea kutwa hajauza hata kikapu kimoja unafikiri hapo nini kinafuata
Ni uzembe wa mpango uzazi bwashee, fuatilia historia ya Finland
 
Hao mabinti wanajitambua nimewapenda. Hakuna raha km mwanamke kutafuta pesa yako halali bila kutweza utu wako.

Mambo ya chuo tunayafahamu, show off nyingi na kutaka kwenda na wakati lazima utumike..!!
Ndio hivyo ukila vya watu lazima uliwe hata ukiwa umepoa kama kiporo.
 
Habari waungwana, Leo nilienda saloon moja ambapo sio mbali sana na kilipo chuo kikubwa Cha serikali.

Wakati nikiwa hapo nahudumiwa Kuna kabinti akawa ameleta huduma ya mtori na chai Kwa hao wadada wa salon.

Basi baada ya yule muhudumu kuondoka ndo hao mabinti wa saluni wakawa wanasema kuwa huyu ikifika mchana anaenda chuo halafu anaingia yule mwenzanke basi bwana baada ya kusikia maongezi yao hivo nikawauliza Kwani huyu Binti ni mwanafunzi wakanijibu ndio ni mwanachuo wa hicho chuo Cha serikali hapo, wapo wawili wanapokezana kufanya kazi hapo muda ambao hawana masomo darasani wanapiga kazi hapo kwenye hicho kimgahawa hapo nje wameaajiriwa hapo kuosha vyombo, kuhudumia wateja kupika chapati chai, Baada ya kazi wanarudi zao hostel Maana wanaishi ndani ya hostel za chuo.

Pia aina ya.mgahawa ni kadogo sana tena kalichozungushiwa maturubai na viti hata havifiki hata 8 lakini mabinti wa watu wameamua kujitoa kumtafuta riziki zao

Hakika nilistaajabu Maana kwanza ni vibinti vidogo vizuri sana wanajituma vizuri na Kwa heshima sana pia hawajapenda kujikweza kama ilivo Kwa mabinti wengine ambao wanapenda Maisha ya shortcut huku wanasoma
Siweki neno
 
Umewasifia sio mda mrefu hao mabinti kuwa wanajituma hawategemei men sahivi tena unaomba kulikoni mamtu 😂 kweli hii kitu mnayo damuni
Hao mabinti mi mshangazi 😹
Kwani kuomba kuna tatizo?
Tatizo unamuomba nani?

Kwani wewe ukinisaidia utaomba returns yoyote?? 😹
 
Back
Top Bottom