Wiki hii zimetoka nafasi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya JKT.
Moja ya kitendo kinachokosa utu na kinachokiuka utamaduni wetu ni kuwavisha watoto wetu wa kike mavazi ya watoto wa kiume, nazungumzia vibukta kwa lazima.
Katiba ambayo ndio sheria mama inamlinda kila raia na imani yake kwa kutoa haki na uhuru wa kuabudu.
Kuvaa mavazi yenye stara kwa wanawake/mabinti wa kiislam ni sehemu ya ibada (kuabudu) inaolindwa na katiba.
Ndio maana wanafunzi mashuleni walipewa uhuru huo miaka ya 80 na serikali hii hii baada ya waislam kusimama umara na kutetea haki hii.
Huko JKT watoto wetu wa kiislam watavalishwa vibukta kwa jina la serikali isiyo na dini, kwa jina la uzalendo kwanza.
Kumekuwa na dhana kuwa tendo hili inafanywa kwa kwa kuwa itikadi ya nchi haina dini. Basi tunachojiuliza dhana hii kwa kuwa serikali haina dini ina maana ya kuwadhibiti wananchi wenye dini au kuwalinda?
Kudhibiti kwa kuwavua baadhi ya Watanzania imani za dini zao badala ya kuzilinda.
Ukweli katiba ya nchi ndio sheria kuu na hivyo kama kuna Sheria za JKT zinazowataka wasichana kuvaa vibukta.
Ieleweke ya kuwa sheria na amri hiyo ni batili. Kwa kuwa inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu.
Hoja ya uzalendo au serikali isiyo na dini naamini ni ya tafsiri ya tabaka la sasa la watendaji chini ya Chama Cha Mapinduzi tulioamua kuwaamini na kuwachagua watekeleze matakwa yetu. Kinyume chake wameamua kutafsiri dhana hizi kwa matakwa na imani tulizonazo ambazo haziathiri imani binafsi.
Kwa miaka mingi sasa JKT imeamua kuminya wenye dini wasipractice uhuru wao wa kuabudu unalindwa na katiba.
Kwani JKT ni moja ya taasisi hizo ni zetu sisi umma.
Tunaitaja jamii, vyama vya siasa, kijamii na taasisi za dini kupaza sauti na kuwatetea mabinti hawa ambao hawana wa kuwasemea.
Kama ambavyo vijana wa kike waliruhusiwa kuvaa nguo zenye stara mashuleni kwanini katika mafunzo ya JKT wasiwe na uhuru huo.
Ni katiba, ni serikali au sheria za chuo inayolazimisha mabinti wanaohitaji mafunzo na wanaohitaji stara kuvuliwa stara zao?
Iwapo ni masharti ya serikali (JKT) hawaoni wanaisigina Katiba inayotoa uhuru wa kuabudu na kwamba kuvaa uniform maalum vitakazolinda stara zao ni haki ya kimsingi kama ambavyo nchi tena zenye waislam walio wachache wanavyoruhusiwa kutekeleza ibada hii ya mavazi kwa kuweka dressing code kwa wanaotaka kuvaa hivyo, je, hii ni dhana ya serikali au ni tafsiri za watendaji wa serikali wanavyotafsiri wao sawa na imani zao?
Kuwavua mavazi ya stara mabinti zetu ni sehemu ya Uzalendo?
Kunawataka Watanzania waelewe hili, uhuru wa kuabudu ni misingi ya haki za binadamu.
Kwanini watz tuko wa ajabu sana linapokuja suala la kuvumiliana values zetu. Kila kundi linalounda watanzania. Kwanini tulazimushwe kufata imani na values za kipagani.
Kwani Ujamaa ni imani.
imani ya Ujamaa ni upagani.
Kama dini dini ni imani
Na kama Ujamaa ni imani
Then Ujamaa ni dini.
Hivyo kusema serikali haina dini ni uongo uliotengenezwa, disinformation and unconstitutuion.
Dini ni falsafa na Ujamaa ni falsafa.
Kwanini serikali iwe na imani ambayo iwe ni lazima kwa wenye imani nyingine kuifata.
Mataifa ya kidemokrasia yanayojipambanua kusimamia haki za binadamu na uhuru wa kuabudu wameweka
GUIDE ON RELIGION AND BELIEF IN THE ARMED FORCES.
Unaweza kugoogle hii title na tuelimike