Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Why Not.

Kwa mujibu wa wanachuoni wa karne hii. Mwanamke yyt aliyepitiliza miaka 45 anaruhusiwa kuongoza taasisi yyt.

Mke wa mtume (s) bi Aisha aliwahi kuongoza jeshi ktk historia ya uislam.

Hata hivyo hiyo ni mada mpya, fungua threat yako.
Mbona hakuna watawala wanawake Saudi Arabia, Jordan, UAE, Kuwaiti, Qatar, Morocco, Oman na Iran.
 
Hata katika mfumo wa majimbo jeshi haliwezi kuwa suala la kimajimbo, jeshi litabakia kuwa federal tu, la kitaifa.
Ni ujuha kutamani majimbo ili mwanao tu asivae bukta jeshini.
Soma zaidi, ona zaidi.

Switzerland yafaa kuwa case study ya katiba yenye mfumo wa majimbo yenye uhuru zaidi au uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

 
Mbona hakuna watawala wanawake Saudi Arabia, Jordan, UAE, Kuwaiti, Qatar, Morocco, Oman na Iran.
No reasech no right to speak.

Pamoja na kutokuwa na viongozi wanawake ktk nchi ulizozitaja ziko nchi zenye waislam wengi zina viongozi wanawake ikiwa ni pamoja na Indonesia, Malasia, Utiruki, Bangladesh.

Kwa mfano. Indonesia ina wakuu wa taasisi, mamlaka wanawake wafanya maamuzi wengi kuliko ilivyo kwa Marekani
 
Lazima kuwe na sheria na taratibu za pamoja kama nchi ambazo ziko juu ya dini zote, haiwezekani kila mtu akataka kuingiza mambo ya dini yake katika mifumo ya serikali. Yani wa Niqab atake niqab jeshini, rastafarian atake kusuka rasta jeshini, msabato akatae kulinda nchi Jumamosi hilo litakuwa jeshi au uwanja wa vurugu.
Sheria na taratibu za pamoja nyinyi mtakubali kuvumilia ikiwa taratibu na sheria hivo sio universal kwa maana haziakisi value zenu.

Ktk mataifa yanayojali haki kama sheria na taratibu hauko universal kila society inawekewa taratibu zake.

Case study ni hijab kwa wanafunzi tz. Kama ninyi hamuumii wanafunzu wa kike kuvaa hijab, kwa jkt mnapaswa kuvumilia pia. Kinyume chake tusilazimishwe watu wa imani nyingine kupractice imani ya kipagani. Kama ambavyo wapagani wasilaximishwe kufata Uislamu. Tupo ktk taifa au tunataka kutengeza taifa la free society
 
Bila kusahau pia mashoga wanaruhusiwa katika jeshi la Marekani na Africa Kusini.
sina hakika kwa africa kusini. Hata hivyo makundi hayo hatahusishi kwa mataifa kama turkey, saudi arabia..

Hoja hata taifa la tz halihusishi, kwa sababu lina percentage ndogo.

Ktk nchi ya kidemokrasia walio wengi ndio hufunga sheria. Na wachache huvumilia. Kwa tz waislam ni miongoni mwa jamii ya walio na idadi kubwa ya population lkn wenyewe wamelala na ndio hivyo hawapewi umuhimu na wenye wafanya maamuzi
 
No reasech no right to speak.

Pamoja na kutokuwa na viongozi wanawake ktk nchi ulizozitaja ziko nchi zenye waislam wengi zina viongozi wanawake ikiwa ni pamoja na Indonesia, Malasia, Utiruki, Bangladesh.

Kwa mfano. Indonesia ina wakuu wa taasisi, mamlaka wanawake wafanya maamuzi wengi kuliko ilivyo kwa Marekani
Hizi nchi ulizozitaja hapa zinafuata mfumo wa demokrasia wa magharibi zaidi kuliko sharia.
 
Wiki hii zimetoka nafasi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya JKT.

Moja ya kitendo kinachokosa utu na kinachokiuka utamaduni wetu ni kuwavisha watoto wetu wa kike mavazi ya watoto wa kiume, nazungumzia vibukta kwa lazima.

Katiba ambayo ndio sheria mama inamlinda kila raia na imani yake kwa kutoa haki na uhuru wa kuabudu.

Kuvaa mavazi yenye stara kwa wanawake/mabinti wa kiislam ni sehemu ya ibada (kuabudu) inaolindwa na katiba.

Ndio maana wanafunzi mashuleni walipewa uhuru huo miaka ya 80 na serikali hii hii baada ya waislam kusimama umara na kutetea haki hii.

Huko JKT watoto wetu wa kiislam watavalishwa vibukta kwa jina la serikali isiyo na dini, kwa jina la uzalendo kwanza.

Kumekuwa na dhana kuwa tendo hili inafanywa kwa kwa kuwa itikadi ya nchi haina dini. Basi tunachojiuliza dhana hii kwa kuwa serikali haina dini ina maana ya kuwadhibiti wananchi wenye dini au kuwalinda?

Kudhibiti kwa kuwavua baadhi ya Watanzania imani za dini zao badala ya kuzilinda.

Ukweli katiba ya nchi ndio sheria kuu na hivyo kama kuna Sheria za JKT zinazowataka wasichana kuvaa vibukta.

Ieleweke ya kuwa sheria na amri hiyo ni batili. Kwa kuwa inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu.

Hoja ya uzalendo au serikali isiyo na dini naamini ni ya tafsiri ya tabaka la sasa la watendaji chini ya Chama Cha Mapinduzi tulioamua kuwaamini na kuwachagua watekeleze matakwa yetu. Kinyume chake wameamua kutafsiri dhana hizi kwa matakwa na imani tulizonazo ambazo haziathiri imani binafsi.

Kwa miaka mingi sasa JKT imeamua kuminya wenye dini wasipractice uhuru wao wa kuabudu unalindwa na katiba.

Kwani JKT ni moja ya taasisi hizo ni zetu sisi umma.

Tunaitaja jamii, vyama vya siasa, kijamii na taasisi za dini kupaza sauti na kuwatetea mabinti hawa ambao hawana wa kuwasemea.

Kama ambavyo vijana wa kike waliruhusiwa kuvaa nguo zenye stara mashuleni kwanini katika mafunzo ya JKT wasiwe na uhuru huo.

Ni katiba, ni serikali au sheria za chuo inayolazimisha mabinti wanaohitaji mafunzo na wanaohitaji stara kuvuliwa stara zao?

Iwapo ni masharti ya serikali (JKT) hawaoni wanaisigina Katiba inayotoa uhuru wa kuabudu na kwamba kuvaa uniform maalum vitakazolinda stara zao ni haki ya kimsingi kama ambavyo nchi tena zenye waislam walio wachache wanavyoruhusiwa kutekeleza ibada hii ya mavazi kwa kuweka dressing code kwa wanaotaka kuvaa hivyo, je, hii ni dhana ya serikali au ni tafsiri za watendaji wa serikali wanavyotafsiri wao sawa na imani zao?

Kuwavua mavazi ya stara mabinti zetu ni sehemu ya Uzalendo?

Kunawataka Watanzania waelewe hili, uhuru wa kuabudu ni misingi ya haki za binadamu.

Kwanini watz tuko wa ajabu sana linapokuja suala la kuvumiliana values zetu. Kila kundi linalounda watanzania. Kwanini tulazimushwe kufata imani na values za kipagani.

Kwani Ujamaa ni imani.

imani ya Ujamaa ni upagani.

Kama dini dini ni imani
Na kama Ujamaa ni imani
Then Ujamaa ni dini.

Hivyo kusema serikali haina dini ni uongo uliotengenezwa, disinformation and unconstitutuion.

Dini ni falsafa na Ujamaa ni falsafa.

Kwanini serikali iwe na imani ambayo iwe ni lazima kwa wenye imani nyingine kuifata.

Mataifa ya kidemokrasia yanayojipambanua kusimamia haki za binadamu na uhuru wa kuabudu wameweka

GUIDE ON RELIGION AND BELIEF IN THE ARMED FORCES.

Unaweza kugoogle hii title na tuelimike

Mimi sishauri mtu kwenda kujiunga huko hii wanayooiitaga sijui operesheni kitu gani.. Full stop
Labda kama ni ajira
 
Sheria na taratibu za pamoja nyinyi mtakubali kuvumilia ikiwa taratibu na sheria hivo sio universal kwa maana haziakisi value zenu.

Ktk mataifa yanayojali haki kama sheria na taratibu hauko universal kila society inawekewa taratibu zake.

Case study ni hijab kwa wanafunzi tz. Kama ninyi hamuumii wanafunzu wa kike kuvaa hijab, kwa jkt mnapaswa kuvumilia pia. Kinyume chake tusilazimishwe watu wa imani nyingine kupractice imani ya kipagani. Kama ambavyo wapagani wasilaximishwe kufata Uislamu. Tupo ktk taifa au tunataka kutengeza taifa la free society
Kuna mambo ambayo nchi hii imeyakosea sana ikiwemo kuruhusu hijabu mashuleni, kuweka vipindi vya dini na tahasusi za kidini katika shule za umma.
 
Kuna mambo ambayo nchi hii imeyakosea sana ikiwemo kuruhusu hijabu mashuleni, kuweka vipindi vya dini na tahasusi za kidini katika shule za umma.
Kipengele gn cha katiba kimekiukwa.


Mimi natumia haji ya uhuru wa kuabudu uliomo ndani ya katiba
 
Ni Africa pekee ndio tunapenda kufanya jambo bila kuhoji. Ukihoji unashambuliwa vibaya sana.

Kwanza swalI langu la msingi kwa nini watu wanyoe mapara? For what reason

Nchi zote kubwa dunuani, zinatambua heshima za dini husika ndio maana unqona jeshini wanawake wa kiislam wanapewa uhuru wa kujisitiriView attachment 3000836

View attachment 3000833
View attachment 3000834View attachment 3000835View attachment 3000840
Tumia akili hao juu ni wanajeshi kamili hao wa chini ni wanafunzi. Umesha ona us marine soldiers wanavyo kuwa trained kwenye extreme conditons? Atagalagala kwenye yope na hijabu? Atapita chini ya nyavu zenye miiba akiwa ametundika hijab?
 
Kila Uhuru Una mipaka yake. Unazungumzia Uhuru huo katika katiba Yani Uhuru wa kuabudu. Uhuru huo unaishia uraini na si kwenye mafunzo ya jeshi.
 
Kwa misingi ya ulicho kiandika hata kwenda JKT kwa wasichana ni dhambi. Na kama wakienda wafanye mazoezi wakiwa wamevaa magauni marefu. Kutokufunika nywele nayo ni dhambi. Je wafanye mazoezi wakiwa wamefunika nywele na nyuso. Michezo nayo inahitaji nguo za michezo na nadhani aina ya nguo hizi nazo ni dhambi.

Mtoa Mada tuelekeze namna ya kuvuka hivi vihunzi bila kutenda dhambi
 
Back
Top Bottom