Ni kifungu cha 19 cha katiba. Kifungu cha pili kinachoitoa uhuru wa kuabudu. Na ibara ya 29 - 30 inayozuia mtu yyt kuzuia wengine kutekeleza haki zilizoanishwa na katiba.
Ufafanuzi.
Kuabudu ni nini.
Jamii moja inayounda watanzania wanaamini kuabudu ni kwenda ktk majumba ya ibada au kumsifia Mungu. Ktk uislam kuabudu ni kutekeleza kila amri ya Mungu. Kwa mfano kuvaa mavazi ya stara tasiyoonyeshesha mapaja, nywele za msichana wa kiislam ni ibada, ni kuabudu. Na ktk miaka ya 80 kama ulikuwepo jamii inayoamini kuamudu ni kwenda kanisani au msikitini walipanga hivi hivi wazo la watoto wa kike wa kiislam kuvaa uniform zenye sifa za kuitwa hijab. Lkn kisheria ikaoneshana yafaa wasichana kuvaa hijab.
Ndio tunachojaribu kutumia kifungu vile vile kwa wanafunzi wa mafunzo ya kijeshi na uzalendo wa kiislam, sinhasinga, wayahudu wavishwe uniform zinazikidhi sifa za kuwa ni uniform ya kiibada (kuabudu).
19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo
(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
Masharti ya Jumla (Ib 29-30)
29. Haki na wajibu muhimu
(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
30. Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu
(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.