Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Somalia Waislamu watupu wanapigana wenyewe Kwa wenyewe

Sudan Waislamu watupu wanapigana wenyewe Kwa wenyewe
Sawa. Kuna mambo mawili unapaswa kuelewa sudan na Somalia. Kama ilivyokuwa Afghanistan.

Vita vyvyt unavyovisikia, iwe Ukraine, Eritrea nchi za wakristo wengi ujue kuna mkono wa
Mmarekani.

Na kila nchi ina puppets na wamarekani huwatumia kuanzisha vurugu. Kwa tz unaweza mwenyewe kuwajua nani ni pupets wa wamarekani. Sio waislam.

Waislam ni anti wazungu na ndio walioipigania na kuipatia tz uhuru. Wakati huo pupets waliungana na wakoloni wazungu.

Somalia ilipokuwa chini ya mahakama ya kiislam ili ilikuwa ya utulivu na GDP yao ilipanda ghafla.

Kwa hiyo mpenda vita na mshikilia shoka la vita na ugaidi ni wamarekani. Bila Marekani hakuna vita, bila Marekani hakuna ugaidi.

Anyway hii sio mada kuu
 
Waislamu akili hamna wanajua kuzaa zaa hovyo tuu. Na kushinda mskitini.
Unadhani kuwa na watoto wengi ni kukosa akili

Kuzaa bila ndoa ndio laana.

Wewe umezaluwa wazazi wako wakiwa kwenye ndoa au ktk hatua ya kupimana.

na wewe utaoa kwanza au utaanza kupima kujya kama mbuzi wako mtamu na anakizazi..

Heri yetu Sisi tusie na akili kuliko kuwa na kizazi cha .........
 
Hayo mambo pelekeni jeshi la Zanzibar sio huku Tanganyika.
Waznz baada ya kuona wasichana wanavisha boxer huku bara akaanzisha jku.

Znz naona ni jimbo lenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyew.

Kuna haja kwa wadanganyika kuhamasishana Tubadili mfumo wa utawala. Kutoka serikali kuu kuwa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Kama Lissu anavyosema ngorongoro ni ya wamasai kwa mujibu wa hisia. Na mnamuunga mkono, basi nami Mohd nasema Pwani ni ya waislam. Tuungeni mkono pia.
 
Dhana ya Kuabudu

Kuvaa mavazi yenye stara ktk imani ya kiislam ni ibada. Ni kuabudu.

Kuabudu si kuswali, kusali na kusifu tu.

Kuabudu ni kutekeleza kila amri ya Mungu kwa mujibu wa imani yako.

Katiba ya nchi kifungu cha 19.

Kifungu cha pili kinatoa uhuru wa kuabudu kwa kila raia.

Na ibara ya 29 - 30 inayozuia mtu yyt (watendaji wa serikali) kuwazuia wengine kutekeleza haki zilizoanishwa na katiba. Kwa muhtadha wa mada hii ni KUABUDU.



19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo


(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.


Masharti ya Jumla (Ib 29-30)


29. Haki na wajibu muhimu


(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
30. Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu
(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma. Mwisho wa kunukuu.



Wiki hii zimetoka nafasi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya JKT.

Moja ya kitendo kinachokosa utu na kinachokiuka utamaduni wetu ni kuwavisha watoto wetu wa kike mavazi ya watoto wa kiume, nazungumzia vibukta kwa lazima.

Katiba ambayo ndio sheria mama inamlinda kila raia na imani yake kwa kutoa haki na uhuru wa kuabudu.

Kuvaa mavazi yenye stara kwa wanawake/mabinti wa kiislam ni sehemu ya ibada (kuabudu) inaolindwa na katiba.

Ndio maana wanafunzi mashuleni walipewa uhuru huo miaka ya 80 na serikali hii hii baada ya waislam kusimama umara na kutetea haki hii.

Huko JKT watoto wetu wa kiislam watavalishwa vibukta kwa jina la serikali isiyo na dini, kwa jina la uzalendo kwanza.

Kumekuwa na dhana kuwa tendo hili inafanywa kwa kwa kuwa itikadi ya nchi haina dini. Basi tunachojiuliza dhana hii kwa kuwa serikali haina dini ina maana ya kuwadhibiti wananchi wenye dini au kuwalinda?

Kudhibiti kwa kuwavua baadhi ya Watanzania imani za dini zao badala ya kuzilinda.

Ukweli katiba ya nchi ndio sheria kuu na hivyo kama kuna Sheria za JKT zinazowataka wasichana kuvaa vibukta.

Ieleweke ya kuwa sheria na amri hiyo ni batili. Kwa kuwa inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu.

Hoja ya uzalendo au serikali isiyo na dini naamini ni ya tafsiri ya tabaka la sasa la watendaji chini ya Chama Cha Mapinduzi tulioamua kuwaamini na kuwachagua watekeleze matakwa yetu. Kinyume chake wameamua kutafsiri dhana hizi kwa matakwa na imani tulizonazo ambazo haziathiri imani binafsi.

Kwa miaka mingi sasa JKT imeamua kuminya wenye dini wasipractice uhuru wao wa kuabudu unalindwa na katiba.

Kwani JKT ni moja ya taasisi hizo ni zetu sisi umma.

Tunaitaja jamii, vyama vya siasa, kijamii na taasisi za dini kupaza sauti na kuwatetea mabinti hawa ambao hawana wa kuwasemea.

Kama ambavyo vijana wa kike waliruhusiwa kuvaa nguo zenye stara mashuleni kwanini katika mafunzo ya JKT wasiwe na uhuru huo.

Ni katiba, ni serikali au sheria za chuo inayolazimisha mabinti wanaohitaji mafunzo na wanaohitaji stara kuvuliwa stara zao?

Iwapo ni masharti ya serikali (JKT) hawaoni wanaisigina Katiba inayotoa uhuru wa kuabudu na kwamba kuvaa uniform maalum vitakazolinda stara zao ni haki ya kimsingi kama ambavyo nchi tena zenye waislam walio wachache wanavyoruhusiwa kutekeleza ibada hii ya mavazi kwa kuweka dressing code kwa wanaotaka kuvaa hivyo, je, hii ni dhana ya serikali au ni tafsiri za watendaji wa serikali wanavyotafsiri wao sawa na imani zao?

Kuwavua mavazi ya stara mabinti zetu ni sehemu ya Uzalendo?

Kunawataka Watanzania waelewe hili, uhuru wa kuabudu ni misingi ya haki za binadamu.

Kwanini watz tuko wa ajabu sana linapokuja suala la kuvumiliana values zetu. Kila kundi linalounda watanzania. Kwanini tulazimushwe kufata imani na values za kipagani.

Kwani Ujamaa ni imani.

imani ya Ujamaa ni upagani.

Kama dini dini ni imani
Na kama Ujamaa ni imani
Then Ujamaa ni dini.

Hivyo kusema serikali haina dini ni uongo uliotengenezwa, disinformation and unconstitutuion.

Dini ni falsafa na Ujamaa ni falsafa.

Kwanini serikali iwe na imani ambayo iwe ni lazima kwa wenye imani nyingine kuifata.

Mataifa ya kidemokrasia yanayojipambanua kusimamia haki za binadamu na uhuru wa kuabudu wameweka


Mwongozo ni huu



View: https://youtu.be/WYAUNij6meo?si=KF6MURiFhUFat7Xx


KWANI JESHI LETU NI LA MRENGO WA KIDINI. AU UNASAHAU KAMA TANZANIA SIYO NCHI YA KIDINI.
 
moyo haujakubali kuwa vazi (uniform) yenye vigezo vya kuitwa hijab ni haki kwa mabinti wa kiislam jeshini au ktk kambi za jeshi.

Ndio maana hata link nilizokuwekea unasema ni wanajeshi nchi za kiarabu.

Ukweli wanajeshi hao ni wa uk, marekani na malawi.

Nakuwekea tena link moja uone uhuru huu wa kuabudu marekani


View: https://youtu.be/LFVeJK2ZdkQ?si=EH4qAnZOdW_YILxY

Hauwezi kuniaminisha kuwa nguo ni vazi la kidini, nitafurahi ukinionesha picha ya wanajeshi wanawake wakiwa wamevaa hijabu, au wakiwa hawajavaa suruali ambayo haikubaliki kwa mwanamke kuvaa.
 
Kwani jeshi la Marekani la kidini.

Kwani jeshi la polisi scotland yard ni la kidini.

Ni Katiba inayotoa uhuru wa kuabudu ukiwa mtaani au ukiwa ni mtumishi wa umma.


View: https://youtu.be/zddiPwicaH0?si=oDVehMbqsHZVbpLm


View: https://youtu.be/RDx2zl5li5k?si=TwW5LxcLzKEYHPPA

Uhuru wa kuabudu ni huko unakoabudu Sio ofisini au jeshini

Pilinhiyo mifano ya nchi nyingine unayotoa ya kwao Sisi Sio photocopy copy machine ya kutoka photocopy za nchi zingine ndio maana majina yetu Sisi tunaitwa Tanzania na wao nchi zao Zina majina Yao

Wana ya kwao na Sisi tuna ya kwetu.

Uhuru wa kuabudu ni huko kwenye ibada huko iwe makaburini mtu anaomba mizimu au msikitini huko Kuna ma uniform yake yawe makanzu au mahijabu mtu Yuko huru huko kuvaa sababu ni uniform ya msikitini katiba inatoa ruksa huru kuabudu aonavyo mtu awe na nguo au Hana

Hayo maeneo mengine hayatambuliki kama maeneo ya ibada Kuna mavazi Yao huko uniform ambayo askari wote wanavaa uniform aina moja iwe kaptula au suruali bila midevu kama ya Osama bin Laden kama ambavyo askari wa Aghanstan hufuga madevu hiyo midevu Yao kule kwao ni uniform yao
 
Ukisoma somo la falsafa. Utagundua hakuna mtu anaweza kuishi bila imani. Wewe una imani, serikali pia lazima uwe na imani.

Kwa hiyo imani haikwepeki.

kwa maana waafrika wote wana imani.

Kilichopo ni hiki. Ktk jamii na zama tulizonazo za kistaarabu kama serikali inapaswa kuongozwa na sheria ambazo zinaakisi universal law.

Kwa kulitambua hili mataifa ya kistaarabu yenye mchanganyiko wa watu wenye mila, imani na tamaduni mbali mbali kutengeza utaratibu wa kuwaacomodate jamii zote. Kwa mfano wanafunzi kuvaa hijab tz. Ni sheria inayowahusu waislam pekee.

Kule znz kuna wasichana hawavishwi vibukta.

Kwa kumalizia serikali yetu inaongozwa na imani ya ujamaa.

Ujamaa ni imani.

Ujamaa ni unatokana na ukomonist, ni imani isiyoamini uwepo wa Mungu (upagani)

Sasa ninyi ndugu zetu mnataka waislam kuuwa wapagani?

Ni muhali.. hata hivyo naamini serikali haijakusudia kufanya hivyo. Bali inafata mazoea au hawatokujua kuwa wanatenda kosa.

Kwa hiyo ni suala la muda tu. Serikali sikivu hii ikiongozwa na 4R. R moja wapo ni reconciliation (upatanisho)

Mtego wa imani.
Si kila imani ni sahihi. Kuna imani zingine ni potofu. Na kwa kuona hilo lazima secular government iweke sheria ambazo zitakuwa huru bila kuingiliwa na itikadi za makundi mbalimbali. Na ilivyo, kila mmoja anapaswa kuitii serikali au mamlaka, kwa maana iko pale kwa ajili ya wananchi wote bila kujali background. Suala la waislam kutaka kuwa treated with exceptional ni kukosa utambuzi na hekima. Maana nchi yetu si ya kiislam.
 
Kuvaa mavazi yenye stara ktk imani ya kiislam ni ibada. Ni kuabudu.

Unlikely na imani yenu. Na nadhani hapo ndipo tusipoelewana. Kwani kuabudu si kuswali, kusali na kusifu.

Kuabudu ni kutekeleza kila amri ya Mungu kwa mujibu wa imani yako
Uniformity (mfanano) ili kuwezesha ufuatiliaji na usimamizi wenye ufanisi ndiyo malengo ya kunyoa vipara,kuvaa mavazi ya kufanana,kula chakula cha kufanana ili ikitokea akapata nafasi ya kulitumikia taifa upande wa majeshi yetu avumilie hivyo vitu pale inapomhitaji kuwa hivyo.

Sasa akavae kanzu,juba sijui ijabu (samahani km nitakosea majina),wakiambiwa suruali yule aje na fupi mimi ndefu na ya kubana malengo yatafikiwa kweli?

Ndio maana nikasema wahusika wahamie Saudi Arabia ama waunde taifa lao. Kama vipi kuja jamaa hapo juu kasema hatoruhusu binti zake kwenda JKT unaweza kuungana naye.
 
Kwa maana hiyo sisi ni wengi kuzidi nyinyi mnaomwaga nje
Sasa huu upupu wa wagalatia ndio mmejazano bongo mnautoa wapi
Mbuzi nyinyi mnaletwa mijini na Necta, mkilowea mnasahau umasikini wenu wa maporini, mnaanza kulinganisha Masaki na Tandale
kwanini usilinganishe Mbagala na huko ulikotokea Ibadakuli au Mwakaleli
acha kuilinganisha mwakaleli na sehemu zenye hewa chafu,we unaisifu masaki huku unaishi yombo na kobazi wa kizaramo wengi wao huishia kariakoo,buguruni,tandika,kigamboni huko masaki wakafanye nini?
 
Kwa sababu umeandika kisheria na m nakujibu kwa kisheria kwa haya maswali machache:-

1. Je ni lazima kwenda JKT?
2. Wameenda kwa hiari au kulazimishwa?
3. Je kuna option nyingine wangeweza kwenda badala ya JKT?

Ukipata majibu rudi kwenye ile rule ya "EX TURPI CAUSA NON ORITUR ACTIO"

Case closed.
 
Kuna jamaa kasema hapo ninyi ndio mnafanya Waislamu kuonekana wapumbavu Sanaa

Kwa kifupi Sana hili siyo taifa la kiisilamu bake na libint lako nyumbani kwako
 
Leo unalalamikia mavazi jeshini kesho utalalamikia kutoruhusiwa kufuga ndevu jeshini.
Mara watakuja wakristo wa Iman Kali nao walalamike wanawake kunyolewa nywele jeshini
Aje mmasai nae aseme anataka avae mashuka yao jeshini hiv Hilo litakuwa jeshi kweli.

Dini ni Mila za watu sio Kila sehemu hizo mila zitaruhusiwa na hii IPO Ili kuwepo na umfanano kwa wote

Alafu kumbuka JKT ni kwamjibu wa Sheria ila sio lazima usipoenda hawatokufata nyumbani kukupeleka kambini.
 
Nina hakika kabisa kwa comment yako hii kuna watu wanakuona na wewe pia hamnazo!

Ukikuwa utagundua kuwa comment ya mtu juu ya mtu haiamui ukweli wa jambo! .... Inasaidia tu kupata attention ikiwa sauti yako ni kubwa kuliko mwenzako.
Mkuu acha wivu kike
 
Back
Top Bottom