Mabinti wa kisasa hebu acheni uongo usio na maana

We jamaa inaonekana ni mtu wa kushikilia vitu vidogo vidogo pia una asili ya ubinafsi ndani yako. Be fair, mie mtu akihitaji gari yangu wala simuulizi unaenda wap wala nn.
Inategemea na ninae mpa sio kwamba sijawahi au huwa siazimishi. Kuna siku nilimuachia mtu gari ikarudi imevunjwa taa ya nyuma na alikuwa anaendesha sijui ni dogo gani, muhusika akapotea na simu alikuwa haupokei.

Nilikuja kukutana nae mwaka na baade kwa bahati mbaya sana Moshi, akaishia kunambia tuyazungumze anaomba msamaha hakujua atanambia nini hadi akaamua tu kuondoka....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwann huwa wanakuwa waongo waongo. Me huwa sipendi mtu anitengenezee uongo aisee huwa napata hasira balaa. Maana anakuwa anakuletea hizo story halafu unakuta baadae anakupiga kirungu cha vocha ya buku.....

Sasa unakuwa unajiuliza, huyu mtu anaefanya dili kubwa kama hizi anakosa hata 10,000 kwenye mobile money au kwenye account?! Hapo ndio huwa nakerekwa.

Mwingine utasikia, "unaweza kuntumia buku hapo kwenye mpesa yangu ninunue umeme maana umekatika halafu siwezi kutoka sasa hivi kwenda kwenye ATM (as if hajui siku hizi kuna huduma ya kuvuta hela kutoka bank kwa sim au hata kununua umeme kwa sim kupitia account ya bank).

Sasa huwa nakerekewa na yale maigizo nakuwa naona sasa huyu mtu why nimekuwa nae karibu na kuzoeana nae.... Maana sikuwa na matarajio kuwa yupo hivi.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Umeona sasa hii kitu. Yaani mtu anakuwaje muongo muongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuelewa sana tu ila nilitaka kukuonyesha ulipojichanganya,

Hao ndo wanaitwa maslayqueen, kiufupi wengi wa kizazi chetu wanapenda kuishi maisha hayo ya maigizo ama kujikweza ili aonwe na jamii, uhuni mwingi na kwa mtoto wa kike kuwa na tabia hizo kiukweli haipendezi kabisa unakuwa kituko na kioja mbele ya jamii
 
Wazee wa kusikilizia michongo[emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna m'moja huyo, nilikutana nae kwenye stationary naona anasaidia kazi. Nikamuomba namba akanijibu mapema sana (ila usoni nikamuona tu huyu anajihami). Sikubembeleza nikakausha.

Kuna siku tukakutana nipo na gari ya rafiki yangu (harrier makalio ya nyani) nimekwenda nayo sokoni. Kuniona macho yakamtoka. Muda naondoka baada ya kununua vitu namuona ananipungia mkono. Nikampungia back kawaida tu nikaendelea na ratiba zangu.

Baada ya siku kadhaa at the same stationary, akaniona akaja haraka sana. Kufika akachukua simu yangu (kama utani hivi) kuishika inadai password. Akaniomba niweke password. Nikaweka akaweka namba zake akajipigia akanirejeshea simu yangu.

Picha ndio likaanza, akanitext usiku ule ule. Tukaanza kuchat. Huku na kule akaanza sasa story za kuonekana yeye yupo vema. Mara ananiambia ile stationary ni ya kwake yule ni mfanya kazi wake.

Mara ananiambia sijui hapa nasoma report ya biashara zangu, namuuliza biashara gani anahamisha magoli taratibu utasikia, "acha tu yaani biashara ni nyingi kwakweli, anyways leta story".

Hapo hapo mara aseme ana mambo mengi sana kichwani hadi anatamani kulewa ili apoteze mawazo, nimtoe out..... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Namuuliza mambo gani yanakuzonga. Oooh wazazi wangu unajua wamefariki, sisi kwetu tupo watatu tu, sasa tumeachiwa nyumba zipo huko mbezi Beach, kijitonyama na tabata, mimi ndio nasimamia. Sasa sijazunguka kufanya ukaguzi.

Namuuliza wewe unaishi wapi kwan kwa sasa, ooooh nakaa tegeta. Kuna siku namtext upo wapi, anasema nipo tegeta, namuuliza upo home, anajibu ndio, nikamwambia nielekeze nakuja kukusalimia nipite njia gani, anaanza kuhamisha magoli, aaaah upo njiani unakuja tegeta au upo tegeta kabisa,namjibu nipo tegeta hapa wewe upo wapi, aaaah sawa ngoja basi nikupigie baada ya dakika 1 maana simu yangu inazima chaji ipo betry low, ngoja niichomeke kwenye chaji isizime...... kisha nikuelekeze.

Kubabake kwan alipiga tena.... Nikapiga simu kimya haiiti..... Nilicheka balaa siku ile.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mkuu, these morons that are not even 'wife material' kwa nn unahangaika nao?

Mwisho watakupiga hiyo ndinga muda si mrefu!
 
Hata mimi nikija kumiliki gari, nitakuwa siulizi kabisaaa... I promise
Ha ha ha ha hadi siku mtu akuazime gari yako halafu achelewe kukurejeshea atakapokupigia simu akwambie bro, naomba tuzungumze, ndipo utaelewa....

Gari sio pasi kusema ikiharibika au ikizingua utatoa 45,000 ununue nyingine.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamwambia mtu tutoke out anakuletea story kuwa anavijua viwanja kweli kweli hapa Dar na hakuna sehemu hajawahi kwenda.

Haya tukaenda KFC pale mlimani, naona mtu anatoa macho anasubiria kila jambo nimuongoze na ameshakwambia hayo ni maeneo yake ya kujidai na haelewi hata pa kuanzia baada ya kufika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Dah sasa unakuwa unajiuliza huyu mtu kwann anidanganye mimi lakini....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee hao ni kunguru wa darπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hapo Hana kazi Wala ramani mjini, kaona gari akajua uko vema sasa shobo Kama zoteπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Katika hili la kuazimishana magari nakuunga mkono mi siwezi kugawa gari langu hivyo, hata useme unaendea mbinguni sitoi gari, nikikuhurumia sana nitakupeleka unakotaka,
 
Man who u been been dating?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…