Mabinti wanaomaliza vyuo na kurudi nyumbani wananyanyapaliwa sana na wazazi kuliko vijana wa kiume

Dah huyo wa udsm mwambie aje nimpe kazi ila nipo mkoa
 

kuna baadh ya familia ambaz mtoto wa kike akifikisha miaka 20 na kuendelea kama hana kaz ni makelele tu wanataman aolewe visa vinakua vingi mpka unachoka tena usiombe hiy familia iwe ya watu wengi,, hakuna picha utaacha kuona.. na hawa wazaz ndo chanz watot wao wa kike kujiingiza kwenye makundi mabaya,, nimeyashuhudia haya kuanzia nilipoanz kujitambua mpka sas ninayaona na yanaumiza sio siri
 



Umasikini tu ndo shida mkuu hayo mambo huwezi kuyakuta katika familia zetu zenye PESA
 
kawaida ya wazazi maskini... elewa neno maskini
 
Hata kwa hao vijana wataenda kunyanyasika pia

Ila suala la kutengwa na wazazi nadhini sio kwa wazazi wote na hili hata upande wa wahitimu wa kiume linatokea na case kama hizo Niko na vivid example ambapo nimeona vijana wakitengwa na wazazi wao mpaka kufikia hatua ya kuchukiwa kabisa.

Ila wakati mwingine inakuwa ni waking call ya kuwaambia kama wamekuwa sasa waanze kujitegemea
 
Hili tangazo lako limekaa kitaalamu sana.
 
Acha tu! Mi nishaambiwa nina laana ndio maana sifanikiwi kila nikifanyacho ...maneno haya niliambiwa na mama yangu mzazi niliporudisha mpira kwa kipa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Mm nikirudi home nikapata Kaz mwaka tu nikaachana nayo. Mzee naye kichwani Kuna maji, anaongea maneno kama guluguja! Nikasepaga mpaka Leo Sina mpango wa kurudi
 
[emoji419][emoji419]Nakazia na huu uzi ufungwe
 

Hakuna mzazi pia anayependa mwanae arudi nyumbani baada ya kuhitimu chuo kikuu kwa uwekezaji mkubwa aliohangaika kumsomesha, kurudi kuja kugombea ugali na wadogo zake. Mzazi wa enzi zetu ilikuwa kijana akienda chuo na chumba chake kinapangishwa au wanachukua wadogo zake. Mzazi anapenda baada ya kuhitimu mtoto aje mara chache kusalimia sio kuja kubanana na wakubwa wenzie (wazazi wake) nyumbani kwao.
 

Kimsingi inaondoa kabisa maana ya kwenda shule! Inamaanisha umeenda na kurudi na boksi tupu, elimu ilitakiwa ikubadilishe tofauti na ulivyokuwa kabla hujaondoka kwenu. Ukitoka nenda kapambane usirudi kwenu.

Ndege wa angani vifaranga vyao vikikua wanavunja kabisa kile kiota ili watoto hata wakirudi wanakuta hamna kambi wakatafute wenyewe, wewe binadamu unarudije kwenu? Ina maana vijana wa siku hizi wamezidiwa akili na kunguru??
 
Kama umefanya utafiti basi bado haujakamilisha. Umerukaruka tu na hoja zako na umetanguliza hisia mbele kwa kusema mabinti wananyanyaswa lakini haujasema sababu. haiwezekani tu mtu akurupuke kumdhulumu mwanae. rudi kaulize sababu ndipo urudi hapa.

Kwa kukusaidia tu, ni hivi ukiwa nyumbani kwa wazazi wewe unakuwa ni mtoto na una wajibu wa kufuata ratiba au utaratibu wanaoupanga wao. sasa wewe unaishi kwa mzazi hlf kila siku unajifanya una ratiba yako sasa hapo ndio shida inapoanzia.
 
Kijana wa miaka 25 huna ratiba yoyote umekuwa msukule? Kila binadamu ana ratiba zake hata kama wewe mzazi utaona za kipuuzi

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…