Mabinti wanaomaliza vyuo na kurudi nyumbani wananyanyapaliwa sana na wazazi kuliko vijana wa kiume

Mabinti wanaomaliza vyuo na kurudi nyumbani wananyanyapaliwa sana na wazazi kuliko vijana wa kiume

Huyu hata akitokea mtu akamuambia muda huu njoo tuishi wote anaenda.
binti kama huyo uwa wanajilengesha ili apate mimba atoke kwao aje kwako sasa ukizingua ndio unaambiwa wanaume tuna nyanyasa watoto wa watu kumbe mwamba hukuwa na mpango ila dem shida zake anataka na wewe uhusike..
 
Kuna binti nilikutana nae mrembo sana anatafuta kazi ,alikuwa ana stress nikaongea nae akaanza kulia ,nikamuacha alie kwanza
Nikamuuliza kwanin usirudi nyumbani kwenu Tabora mi nitakupa nauli ,hapa mwanza anaishi tu kwa wazazi wa rafiki yake,akasema bora akae tu kwa watu kuliko nyumbani ni shida sana akanisimuliza visa vya baba ake na mama yake wa kambo!
Ila wazazi tubadilike tufanye nyumbani iwe sehemu amani ya kwa watoto wetu warudi wanapotaka ilimradi wawe na adabu
Inasikitisha kwa kweliii.
 
Hakuna mzazi pia anayependa mwanae arudi nyumbani baada ya kuhitimu chuo kikuu kwa uwekezaji mkubwa aliohangaika kumsomesha, kurudi kuja kugombea ugali na wadogo zake. Mzazi wa enzi zetu ilikuwa kijana akienda chuo na chumba chake kinapangishwa au wanachukua wadogo zake. Mzazi anapenda baada ya kuhitimu mtoto aje mara chache kusalimia sio kuja kubanana na wakubwa wenzie (wazazi wake) nyumbani kwao.
Sio kwa usawa huu, ilikua zamani wallah.
 
Ni human nature, ni rahisi mzazi kukaa na kijana wa kiume ambaye hajaoa kuliko kukaa na binti ambaye hajaolewa, yani ndani ya moyo anakuwa anakuona kama mzembe, akiwaza mpaka sasa binti hujaolewa anaona kama problem is you, kwa nn usipate mwanaume?

Hiyo ni nafsi yake inamuambia ivo.
Sasa ajitongozeshe ihiiiii...hao wazee vipi!
 
Mmoja anafanya kazi ila still home wanaona kama "BADO HAITOSHI".... Yani mama mtu ana kitu moyoni anatamani akiseme lakini ndo ivo hawezi kukisema directly..
🤣🤣🤣Walijua mtoto wao atakuwa mkurugenzi nini akaishia kuwa mkata tiketi wa mwendo kasi!
 
Kimsingi inaondoa kabisa maana ya kwenda shule! Inamaanisha umeenda na kurudi na boksi tupu, elimu ilitakiwa ikubadilishe tofauti na ulivyokuwa kabla hujaondoka kwenu. Ukitoka nenda kapambane usirudi kwenu.

Ndege wa angani vifaranga vyao vikikua wanavunja kabisa kile kiota ili watoto hata wakirudi wanakuta hamna kambi wakatafute wenyewe, wewe binadamu unarudije kwenu? Ina maana vijana wa siku hizi wamezidiwa akili na kunguru??
Huo ndio umasikini wa fikra sasa.
Huyo ndege kabla ya kumfukuza kinda wake anahakikisha amemfundisha kila kitu kujitafutia, kujilinda na kujenga kiota pia kila kitu anafundishwa kwanza ndio anafukuzwa

Sasa turudi huku kwetu wewe umepelekwa shule kusoma ualimu au kozi yyte ile then kwa situation ya sasa ilivyo huna connection wala elimu ya mtaa then unafukuzwa tu.

Mentor wa wakwanza ni wazazi au walezi wako ukiona umefail ujue wao kuna sehemu wamefail juu yako pia..
Na hili lipo wazi kabisa!
 
Huo ndio umasikini wa fikra sasa.
Huyo ndege kabla ya kumfukuza kinda wake anahakikisha amemfundisha kila kitu kujitafutia, kujilinda na kujenga kiota pia kila kitu anafundishwa kwanza ndio anafukuzwa

Sasa turudi huku kwetu wewe umepelekwa shule kusoma ualimu au kozi yyte ile then kwa situation ya sasa ilivyo huna connection wala elimu ya mtaa then unafukuzwa tu.

Mentor wa wakwanza ni wazazi au walezi wako ukiona umefail ujue wao kuna sehemu wamefail juu yako pia..
Na hili lipo wazi kabisa!

Kibongobongo wazazi wanajua wakishakupeleka shule na kukulipia ndio washakumentor hivyo, baada ya kukua ukiwa kwenu mkuu! Na wewe ukienda shule ukadesa ukarudi home na makarai yako ujue huna tena chumba! Washachukua wadogo zako. Tukiacha unafiki mzazi gani anamentor mwanae mkuu? Mzazi anajua mtoto akitoka kwake anaenda kujitafutia maarifa ya maisha yake na harudi tena, so ukirudi wanakuona mzigo tu, ndio fact hata tukiwa nyuma ya keyboard tukajitoa ufahamu!
 
Hili huenda likakushangaza lakini ndiyo ukweli wenyewe. Hii hali ipo sana sana mijini, nimeshashuhudia mabinti kadhaa hasa wanaotoka familia za kati na duni wakiwa wanaishi kwa tabu sana na wazazi pindi wanaporudi nyumbani baada ya kumaliza vyuo.

Wa kwanza alimaliza SUA mwaka 2020. Akarudi kwao Dar kwa mzazi wake aliyebaki hai ambaye ni mama. Yule binti mateso na manyanyaso aliyopitia mpaka ilifika kipindi akataka kuondoka kwao, ila hakuwa na pa kwenda. Bahati nzuri akapata kazi serikalini, baada ya kupata kazi ndiyo angalau wameanza naye ni mtu.

Wa pili kamaliza chuo mwaka jana tu hapo UDSM. Huyu wazazi wake wote 2 bado wako hai. Mzee wake alishastaafu ila mama bado anafanya kazi. Kwa jinsi anavyoteswa na wazazi wake yupo kwenye hatua za mwisho kuondoka kwao aende anakokujua akajitafutie maisha. Na hana boyfriend, ananiambiaga wazi angekuwa naye basi angeshasepa kitambo akaishi naye.

Huyu hata akitokea mtu akamuambia muda huu njoo tuishi wote anaenda. Vituko na visa anavyofanyiwa na wazazi wake mpaka huwa namuuliza "Una uhakika hao ni wazazi wako? Maana wameshafikia mpaka hatua ya kumuambia aondoke ndani mwao. Cha kushangaza ni kwamba hapo nyumbani yupo kaka yake na anasema huwa hapewi harrassments kama anazopewa yeye.

Wa 3 huyu naye yuko Dar. Alisoma Diploma ya Sheria kisha akawa yupo tu nyumbani hajabahatika kuajriiwa mpaka sasa. Huyu naye ni yaleyale, ameteswa kisaikolojia na wazazi mpaka sasa ukimuona amekonda mno. Ilifikia mpaka kipindi alitaka kufanya suicide kwa sababu ya psychological torture aliyokuwa anapitia toka kwa wazazi wake.


Je, hii ni wakeup call kwa mabinti walioko vyuoni kuhakikisha hawamalizi vyuo bila wenza, na wasirudi makwao maana hawataepuka mateso? Maana kulingana na nature yetu waafrika, ni rahisi sana kuishi na kijana wa kiume nyumbani kuliko binti. Yani binti ambaye umeshafika miaka 26+ kukaa na wazazi nyumbani ina tension kubwa kwa wazazi kuliko kuishi na kijana wa kiume.
Hii ni pande zote hata kwa vijana wakiume inawatokea
hasa wanapomaliza vyuo na kushindwa kupata kazi kwa haraka wananyanyapaliwa,kuchekwa na ndugu zao na kudhihakiwa pia
Sisemi kama inafaa ila mdomaana baadhi ya vijan wakishapata kazi au mishe nzuri huwa wanawapotezea baadhi ya ndugu zao
 
Kuna mzazi alishamtamkia haya maneno mwanae baada ya kukaa zaidi ya miaka 5 bila kazi ya kueleweka, Mungu si John baptist sasa ni mtumishi wa umma nafasi nzuri Tu, hiyo huyo mzazi wake full praises on him kama si yeye aliyekuwa kutwa akimsema si chochote, si lolote mpaka kwa majirani. Tuwasamehe tu wazazi wetu wanaopitia frustrations nyingi......
Ni kweli
Mambo hubadilika ghafla
 
Acha tu! Mi nishaambiwa nina laana ndio maana sifanikiwi kila nikifanyacho ...maneno haya niliambiwa na mama yangu mzazi niliporudisha mpira kwa kipa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Ngoja upate hela utaona mkuu. Huyo huyo aliyesema,kila mwezi atakuwa anakuja kwako kupumzika(ili aondoke na chochote)
 
Back
Top Bottom