Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], yote hayo yanini?? They have a choice, usilazimishe ndoa utawaumiza sasa watoto wakiume. Just mjenge mtoto wako wakiume akae vizuri kifikra, kielimu na kiuchumi mengine yatakuja.Habari za wakati huu ndugu zangu....
Wazazi wamekua wakijitahidi kulea mabinti zao vyema japo Lipo wimbi kubwa sana la wanawake kubweteka na kua malimbukeni kupita kiasi, hali hii imesababisha kujiona wao ni wao na wanaweza kuishi wenyewe bila kua na mwanaume atakae kua kichwa ..
Mtazamo huu umechangia sana wanawake wengi kukataa wanaume wanaokuja kuwa chumbia kwa lengo la kuwa oa na kuweka ndani kama mke halali, na hili limechangiwa sana na kuiga wanawake wenzao hasa wanao wadanganya ndoa ni chungu, ndoa ni karaha, mwanamke ni jeshi kubwa , mwanamke anaweza , mwanamke ni mpambanaji na nguvu kubwa sana inayotoka kwa masingle maza walio zalishwa na kuachika kutokana na tabia zao mbaya ..
Mabinti wengi sana wameharibika na kuwaharibu wale wenzao wachache walio salia salia na tabia njema, inasikitisha sana kukuta binti wa miaka 15+ anao mtazamo wakuja kuishi mwenyewe bila mwanaume naye anasema hataki kuolewa , tena anafika mbali zaidi ana kuambia nitazaa tuu na nitalea mwenyewe... Hebu jiulize hii elimu au huu mtazamo kaupata wapi kama sio kutoka kwa wanawake wenzake/ mabinti wenzake / hawa hawa masingle maza wanao ongoza kuharibu mabinti kwa kuwaambia kuishi na mwanaume ni utumwa..
Swala hili limesababisha sana wanawake wengi/ mabinti wengi kwa sasa kukataa wanaume pale wanapotongozwa kwa nia ya kuolewa na wengine kufikia mbali kutaka tuu mbegu na ukimpa mbegu hapo anakuona wewe huna thamani tena na sio kitu. Wengine wanakataa wanaume mpaka wanakuja kujutia ukubwani anapopita umri wa kuolewa nakuja kugundua kwamba walidanganyika na hawawezi tena kurudisha siku nyuma kutokana na kupoteza mvuto kwa mwanaume na hivyo kubaki kwa wazazi wao, majumbani au kwenye himaya za koo zao ,ndugu jamaa na marafiki wakiwa magroup kwa magroup huku wakiendelea na kuharibu mabinti wanao chipukia wenye nia na ndoto za kuolewa na kuishi mume na mke.
Hivyo kama unaye binti au unaye mwanamke ambae hajaolewa nayupo katika umri wa kuolewa huyo ni hatari kwa kizazi cha mabinti wa sasa huyo mfukuze nyumbani acha maramoja kumchekea chekea hakika kwa kufanya hivyo ulimwengu utamchapa na hamu ya kuolewa itamjia na atajifunza mengi sana kuhusu maisha ya upweke kwa kweli...mfukuze kabisa nyumbani mwache ulimwengu ukamfunze thamani ya kuwa na mwanaume na kuolewa na ukamshape namna ya yeye kubehave kama mwanamke mbele ya wanaume
Uko sahihi.....Kama mtoto wa kike ndo unamlelea hivyo sipati picha huyo mtoto wako wa kiume atakua ni dhaifu balaaa itakua mke akimzingua kidogo anakimbilia nyumbani
Ndo maana tunakizazi nyoronyoro sana sababu ya malezi mabovu kama haya kuna siku wewe haupo dunia ataishije, umekua mzee nguvu huna ataishije
Ndo maana sishangai maswala ya ushoga yanarindima sana kwa sababu watoto wanalelewa kinyoronyoro sana
Inafuatana na mazingira mkuu mfano kama binti hajapata wa kumchumbia hapo huwezi kumfukuza.Yaani mzazi amfukuze mtoto? Nani sasa atakaye mpokea kama wazazi wamemfukuza, nadhani kumfukuza ndio hatari sana kwa jamii kuliko kubaki nyumbani...
Aende wapi sasa wakati hapo ndio kwao,ukimfukuza ndio utakuwa umemaliza tatizo?Akizaa watoto watatu nyumbani kwako utamlea yeye na watoto wake??
Sina mtoto mkuu, mimi sikupingi ni haujanielewa tu, msisitizo wangu huko kwenye kumuandaa mtoto... wengi wa vijana ikiwemo mimi tumelelewa kwa mazingira ambayo ni yakutunyima kujiongeza.. wazazi wetu wamekuwa wakituminya sana kwanzia tukiwa wadogo mtu unakuja kupata uhuru ukiwa chuo ujui mambo mengi ya maisha.. Tazama wazazi wawenzetu (wahindi na tz baadhi) mtoto yuko sekondari lakini jioni anafanya kazi dukani kwao, hardware kwao, hotelini kwao, anaanza kujua biashara anaanza kumiliki asset n.k, nitofauti kabsa na yule anayerudi kutoka shule nakuanza kusisitiziwa kusoma, kunyimwa kutoka nyumbani na kunyimwa kujichanganya(ambayo ndio maisha walio lelewa watu wengii)...Ndo maana waafrika ni race dhaifu sana sababu ya watu wenye fikra zako na wanawalelea watoto wao kwenye fikra kama zako, ukikaa na wazungu utagundua wanafundishwa ujasiri tokea wakiwa wadogo na wanafundishwa kutokuogopa maisha
Wewe endelea kumlelea mtoto wako kimayai mayai
Hao waliomzalisha hawana pa kukaa??Aende wapi sasa wakati hapo ndio kwao,ukimfukuza ndio utakuwa umemaliza tatizo?
Mkuu nikweli kabsa, ndoa nyingi zinadumu kwasababu wanawake hawana kipato na hawana njia nyingine ya kuishi zaidi ya kumtegemea mwanaume, na inapelekea mateso makali sana kwa wamama wengi,Wanawake upitia kipindi kigumu Sana ajira hawana, wahongaji hawana kitu, mwanaume atahonga Ili avue samaki akishapata samaki haitaji tena samaki huyo.
Mwanamke yeyeto akikuomba pesa na unayo mpe pasipo kutegemea malipo ya kulisoma gazeti lake.
Kataa uzinzi unaleta magonjwa ya kiroho na kimwili.
Nakubaliana na wewe mkuu, ila kwenye kumchagulia mtoto mtu wakumuoa au kumlazimishia inaweza kukuleta shida mbeleni na ukawa wewe ndio wakulaumiwa,,, chamsingi nikuongea na mabinti na vjana kuhusu haya mambo baada ya kuwaandaa kwanzia wakiwa wadogo.. nakazia wazazi nikipengele sana kuaribika, kubweteka kwa viajana japo sio vijana wote wameharibika kwasabbu ya malezi mabaya ya wazazInafuatana na mazingira mkuu mfano kama binti hajapata wa kumchumbia hapo huwezi kumfukuza.
Lakini chukulia mfano huu: Ww kama mzazi una binti wa miaka 23 nyumbani hasomi na anabahati wanakuja wanaume wa maana kumchumbia ili wamuoe anawakataa, alafu wakati huo huo analiwa hovyo mitaani na mabodaboda na wanyoa viduku , hivi ww kama mzazi ukiendelea kumchekea mtoto wa aina hii utakuwa una faa kuwa mzazi kweli?
Binti yangu akifikisha umri wa kuolewa na akaja mtu kumchumbia na nikamuona ni mtu sahihi kwake ni razima aolewe kama hataki aondoke nyumbani kwangu akajitegemee ili apate uhuru vizuri wa kufanya anacho taka.
Ndani ya nyumba yangu siwezi kulea mzinzi mm ambaye badae atakuja kunijazia matoto yasiyo julikana baba zao wako wapi.
Wazazi wa siku hizi wamekuwa na mchango mkubwa katika kuharibu maisha ya mabinti zao kwa sababu ya uzembe na uzungu wa kipumbavu.
Tatizo kubwa la watanzania tunasahau matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu inshort tunaogopa sana maishabora abakii akiwa mzima kuliko kuolewa na mtu asiye sahihi na kurudi akiwa ndani ya jeneza atabaki hadi apate mtu sahihi kwa ajili yake
Kuna vitu lazima umzuie mtoto wako asivijue kwa sababu anakua hajakomaa kiakili wazazi walikua sahii kukubana huwezi mpa mtoto uhuru anaoutaka utamuharibu sababu bado hajakomaa kiakiliSina mtoto mkuu, mimi sikupingi ni haujanielewa tu, msisitizo wangu huko kwenye kumuandaa mtoto... wengi wa vijana ikiwemo mimi tumelelewa kwa mazingira ambayo ni yakutunyima kujiongeza.. wazazi wetu wamekuwa wakituminya sana kwanzia tukiwa wadogo mtu unakuja kupata uhuru ukiwa chuo ujui mambo mengi ya maisha.. Tazama wazazi wawenzetu (wahindi na tz baadhi) mtoto yuko sekondari lakini jioni anafanya kazi dukani kwao, hardware kwao, hotelini kwao, anaanza kujua biashara anaanza kumiliki asset n.k, nitofauti kabsa na yule anayerudi kutoka shule nakuanza kusisitiziwa kusoma, kunyimwa kutoka nyumbani na kunyimwa kujichanganya(ambayo ndio maisha walio lelewa watu wengii)...
Mimi najitolea mfano mwenyewe nimelelewa mzingira yakuto kukutana na watu sana yaani mda wote ndani na dada wa kazi kwasababu ya biasharaa za wazazi wangu zilikua sii rafiki kwa watoto.. kitu ambacho kimeniathiri mpaka sasa uwezo wa kuchanganyika sina , kuongea tu ma mtu mgeni jasho mwili mzima kwahyo changamoto ni malezi sio vijana
Nimekupangia wapi nakukumbusha hii ni forum lazima ujibiwe pona yako ni usicomment kabisaUko sahihi.....
Wewe lea unavyoona ni sawa....
Tusipangiane tu!
Huo mjadala wa ushoga uache tu maana hilo ni suala tata sana. Ukipenda lianzishie uzi wake tujadili huko!
Lakini binti yangu yuko poa na tunaheshimiana mno...na nina uhakika kuwa I have raised a strong, independent and a powerful woman.
Hakuna kitu chenye impact kubwa kwa mtoto wa kike kama upendo wa kweli wa baba yake. Mfanye awe rafiki yako. Mwonyeshe how a real man is supposed to be. Awe safe kwako in every possible situation. Na aijue pia mipaka yake kwako na vitu vitakavyokupa huzuni kama akivitenda. Nakwambia ni raha sana!
Wewe lea kwa kutumia hayo maguvu na vitisho lakini kizazi hiki kina changamoto zake tofauti sana. May be utafanikiwa. May be not ila kama nilivyosema haya mambo ni kila mzazi na lwake na hakuna guarantee. Ila kwangu mimi upendo umenipa matokeo bora sana...
Hata nikipata mtoto mwingine, my MO will be the same and I won't change a thing!
Asante baba🙏My daughter will always be my daughter, whether she is 15 or 90...and my home is her home forever!
Ataondoka akitaka na atarudi wakati wo wote akitaka. This is her safe place akichoshwa na dunia huko anarudi kwenye usalama wa baba yake.
Aamue kuolewa au kutoolewa huo ni uamuzi wake!
me sijamwambia ayaogope yy ndio anajua yupi sahihi yupi sio siku akimpata huyo anayeona kwake ni sahihi ndio atatokaTatizo kubwa la watanzania tunasahau matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu inshort tunaogopa sana maisha
Huyo mtu ambaye ni sahii au sio sahii unamjuaje no one know tommorow mfundishe mtoto wako apambane kukubaliana na magumu na sio kuyaogopa
Ulichoandika hapa na reply ulionijibu ni vitu viwili tofautime sijamwambia ayaogope yy ndio anajua yupi sahihi yupi sio siku akimpata huyo anayeona kwake ni sahihi ndio atatoka