Mabinti wenye umri wa kuolewa na hawajaolewa wafukuzwe nyumbani haraka

Waende wapi ndugu. Suala la ndoa sio la KILA mtu ndoa ni maalumu KWA ajili ya watu maalumu. Ndoa ni ibada SAsa wote wanaweza fanya ibada
 
Wanawake upitia kipindi kigumu Sana ajira hawana, wahongaji hawana kitu, mwanaume atahonga Ili avue samaki akishapata samaki haitaji tena samaki huyo.
Mwanamke yeyeto akikuomba pesa na unayo mpe pasipo kutegemea malipo ya kulisoma gazeti lake.
Kataa uzinzi unaleta magonjwa ya kiroho na kimwili.
 
..........kumfukuza mtoto nyumbani Lisa haolewi inaweza kuwa sio sahihi sana, ilahuwa naona watu wanafukuza Binti nyumbani indapo kashika mimba ingawa nalo sio suluhisho limekaa kihasira zaidi.....
........napendekeza Kwa wale wenye mabinti wakubwa ambao tayari wanamaliza elimu za sekondari na wanaanza chuo, pamoja na wale waliopo nyumbani hawasomi ila ni wakubwa tayari, wazazi au wlezi waane kuwaeleza ukweli umuhimu was ndoa .....
........wawaeleze na kuwafundisha ukweli kwamba Wana haki ya kuchagua wenza lakini hawatakiwi kuwa selective too much, kwamba anapotokea mwenye Nia ya dhati ya kuoa na anakidhi vigezo viwili vitatu wakubali kuolewa vinginevyo wahuni watawazaliaha na kuwaacha nyumbani....
........ukweli mchungu ni kwamba ndoa ni muhimu, heshima na hitaji kubwa Kwa mwanamke kuliko mwanaume, frustrations na stress za kukosa ndoa alizonazo mwanamke ni kubwa kuliko mwanaume, wazazi wawa-incourage mabinti kuolewa kuliko kuwasapoti kwenye kukataa wanaume Kwa vigezo vya kijinga na kuona hayo ndo malezi ya kisasa.............. ........mind you waoaji ni wachache nowadays, hiki ni kizazi cha kataa ndoa, mwanao kuzeekea nyumbani sio sifa kwamba we ndo unalea kizungu, haki na democracy........
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787], yote hayo yanini?? They have a choice, usilazimishe ndoa utawaumiza sasa watoto wakiume. Just mjenge mtoto wako wakiume akae vizuri kifikra, kielimu na kiuchumi mengine yatakuja.
 
Uko sahihi.....

Wewe lea unavyoona ni sawa....

Tusipangiane tu!

Huo mjadala wa ushoga uache tu maana hilo ni suala tata sana. Ukipenda lianzishie uzi wake tujadili huko!

Lakini binti yangu yuko poa na tunaheshimiana mno...na nina uhakika kuwa I have raised a strong, independent and a powerful woman.

Hakuna kitu chenye impact kubwa kwa mtoto wa kike kama upendo wa kweli wa baba yake. Mfanye awe rafiki yako. Mwonyeshe how a real man is supposed to be. Awe safe kwako in every possible situation. Na aijue pia mipaka yake kwako na vitu vitakavyokupa huzuni kama akivitenda. Nakwambia ni raha sana!

Wewe lea kwa kutumia hayo maguvu na vitisho lakini kizazi hiki kina changamoto zake tofauti sana. May be utafanikiwa. May be not ila kama nilivyosema haya mambo ni kila mzazi na lwake na hakuna guarantee. Ila kwangu mimi upendo umenipa matokeo bora sana...

Hata nikipata mtoto mwingine, my MO will be the same and I won't change a thing!
 
Yaani mzazi amfukuze mtoto? Nani sasa atakaye mpokea kama wazazi wamemfukuza, nadhani kumfukuza ndio hatari sana kwa jamii kuliko kubaki nyumbani...
Inafuatana na mazingira mkuu mfano kama binti hajapata wa kumchumbia hapo huwezi kumfukuza.

Lakini chukulia mfano huu: Ww kama mzazi una binti wa miaka 23 nyumbani hasomi na anabahati wanakuja wanaume wa maana kumchumbia ili wamuoe anawakataa, alafu wakati huo huo analiwa hovyo mitaani na mabodaboda na wanyoa viduku , hivi ww kama mzazi ukiendelea kumchekea mtoto wa aina hii utakuwa una faa kuwa mzazi kweli?

Binti yangu akifikisha umri wa kuolewa na akaja mtu kumchumbia na nikamuona ni mtu sahihi kwake ni razima aolewe kama hataki aondoke nyumbani kwangu akajitegemee ili apate uhuru vizuri wa kufanya anacho taka.
Ndani ya nyumba yangu siwezi kulea mzinzi mm ambaye badae atakuja kunijazia matoto yasiyo julikana baba zao wako wapi.

Wazazi wa siku hizi wamekuwa na mchango mkubwa katika kuharibu maisha ya mabinti zao kwa sababu ya uzembe na uzungu wa kipumbavu.
 
Sina mtoto mkuu, mimi sikupingi ni haujanielewa tu, msisitizo wangu huko kwenye kumuandaa mtoto... wengi wa vijana ikiwemo mimi tumelelewa kwa mazingira ambayo ni yakutunyima kujiongeza.. wazazi wetu wamekuwa wakituminya sana kwanzia tukiwa wadogo mtu unakuja kupata uhuru ukiwa chuo ujui mambo mengi ya maisha.. Tazama wazazi wawenzetu (wahindi na tz baadhi) mtoto yuko sekondari lakini jioni anafanya kazi dukani kwao, hardware kwao, hotelini kwao, anaanza kujua biashara anaanza kumiliki asset n.k, nitofauti kabsa na yule anayerudi kutoka shule nakuanza kusisitiziwa kusoma, kunyimwa kutoka nyumbani na kunyimwa kujichanganya(ambayo ndio maisha walio lelewa watu wengii)...
Mimi najitolea mfano mwenyewe nimelelewa mzingira yakuto kukutana na watu sana yaani mda wote ndani na dada wa kazi kwasababu ya biasharaa za wazazi wangu zilikua sii rafiki kwa watoto.. kitu ambacho kimeniathiri mpaka sasa uwezo wa kuchanganyika sina , kuongea tu ma mtu mgeni jasho mwili mzima kwahyo changamoto ni malezi sio vijana
 
Mkuu nikweli kabsa, ndoa nyingi zinadumu kwasababu wanawake hawana kipato na hawana njia nyingine ya kuishi zaidi ya kumtegemea mwanaume, na inapelekea mateso makali sana kwa wamama wengi,
 
Nakubaliana na wewe mkuu, ila kwenye kumchagulia mtoto mtu wakumuoa au kumlazimishia inaweza kukuleta shida mbeleni na ukawa wewe ndio wakulaumiwa,,, chamsingi nikuongea na mabinti na vjana kuhusu haya mambo baada ya kuwaandaa kwanzia wakiwa wadogo.. nakazia wazazi nikipengele sana kuaribika, kubweteka kwa viajana japo sio vijana wote wameharibika kwasabbu ya malezi mabaya ya wazaz
 
bora abakii akiwa mzima kuliko kuolewa na mtu asiye sahihi na kurudi akiwa ndani ya jeneza atabaki hadi apate mtu sahihi kwa ajili yake
 
bora abakii akiwa mzima kuliko kuolewa na mtu asiye sahihi na kurudi akiwa ndani ya jeneza atabaki hadi apate mtu sahihi kwa ajili yake
Tatizo kubwa la watanzania tunasahau matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu inshort tunaogopa sana maisha

Huyo mtu ambaye ni sahii au sio sahii unamjuaje no one know tommorow mfundishe mtoto wako apambane kukubaliana na magumu na sio kuyaogopa
 
Kuna vitu lazima umzuie mtoto wako asivijue kwa sababu anakua hajakomaa kiakili wazazi walikua sahii kukubana huwezi mpa mtoto uhuru anaoutaka utamuharibu sababu bado hajakomaa kiakili
 
Nimekupangia wapi nakukumbusha hii ni forum lazima ujibiwe pona yako ni usicomment kabisa
Mimi simlelei mtoto kwa vitisho namlelea asiogope maisha pale anapokutana na changamoto atumie akili na mbinu azikibali awe wa kike au wakiume

Sio kila changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wake kuzikabili anakimbilia kwangu hapana, anakuja kwangu mpaka nijiridhishe amerun-out of option simlelei mtoto kimayai au kwa vitisho namlelea aweze kutumia akili yake effectively sababu matatizo tumeumbiwa wanadamu
 
Tatizo kubwa la watanzania tunasahau matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu inshort tunaogopa sana maisha

Huyo mtu ambaye ni sahii au sio sahii unamjuaje no one know tommorow mfundishe mtoto wako apambane kukubaliana na magumu na sio kuyaogopa
me sijamwambia ayaogope yy ndio anajua yupi sahihi yupi sio siku akimpata huyo anayeona kwake ni sahihi ndio atatoka
 
me sijamwambia ayaogope yy ndio anajua yupi sahihi yupi sio siku akimpata huyo anayeona kwake ni sahihi ndio atatoka
Ulichoandika hapa na reply ulionijibu ni vitu viwili tofauti
Umesema "bora abakii akiwa mzima kuliko kuolewa na mtu asiye sahihi na kurudi akiwa ndani ya jeneza atabaki hadi apate mtu sahihi kwa ajili yake"
 
Kuolewa sio lazima,,,nimfukuze aende wapi sasa wakati starehe yangu na Mama yake ndio imemleta yeye,,mbaya zaidi yeye alikuwa hajui na wala hatukuingia makubaliano nae,,ingewezekana angekataa tusimlete dunia,,,kwani kaka ulishawahi kutuletea hata sukari kwa ajili ya malezi???Tuachie watoto wetu wa kike tutawalea hata wakizeekea nyumbani safii tuu kwa kuwa ni wa kwetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…