Mabinti wenye umri wa kuolewa na hawajaolewa wafukuzwe nyumbani haraka

1. Tuende wapi sasa?
2. Unataka tukapange?
3. Mtoto wa kike kwenda kupanga ni balaa jingine hilo.
1. Tulieni nyumbani muwe na Heshima kwa wazazi, Walezi na Wakubwa wenu halafu mzingatie Ushauri wa bure mnaopewa mara kwa mara kutoka kwa waliowatangulia. Acheni na Epukeni ile tabia ya kujazana ujinga wa Rika lenu(Mashosti)e.g. binti anajigamba mbele ya wenzake "aah; Mm siwezi kuolewa na mtu kama yule mbona hana lolote, hajawahi kuninunulia hata ....hanitoi out.....n.k. .badala ya kuona mbali kwamba kwa hii fursa je, tunaweza kuyajenga kwa pamoja? Jiungeni katika vikundi vya Ujasiriamali, Vikoba au tafuteni mikopo halali muanzishe miradi midogo-midogo itakayo wakeep busy. Kama ni mtu wa Imani jiunge katika vikundi vilivyopo huko kwenye imani yako. Muwe na roho ya kupenda kujitoa kusaidia wengine e.g. kufundisha/kulea watoto au kuwatunza Wazee, n.k.. Acheni na Kataeni kwa nguvu zote kule kujiona kwamba kwa kuwa ww ni Ke ndo mtaji au ww ni wa kipekee sana. Acheni kupenda starehe na anasa kupita kiasi e.g. kwenda kulundikana baa/vilabuni au kujipitisha-pitisha maeneo huku mmevaa zile naniliu zenu.
2. Kama una kipato cha kukuwezesha, basi tumia kipato hicho kutoa support(wapige tafu) hapo unapoishi- hawatatamani uondoke.
3. Ni nini haswa kinachowasumbua/kera kiasi hata mdiriki kuwaza kwenda kupanga? au ni ile dhambi ya Adamu na Eva inawatafuna? 😳
 
Inasikitisha sana.
Heri kubaki nyumbani kuliko kuolewa na yeyote tu, mwisho wa siku ni majuto.
 
Fukuza binyi yako kwanza ili uonyeshe mfano,

Ila wakayi.mwingine juwa nawatafakari sana watu wa aina yako
 
Katika vitu ambavyo siwezi kuvifanya ni kufukuza mtoto wa kike, mwanangu wa kike ataondoka nyumbani pale atakapoolewa tu ata akifikisha miaka 40 hakuna kuondoka nyumbani.
Naomba niwe mwanao
 
Ndoa za sasa hazidumu pia kutokana na wazazi kudekeza mabinti zao, akiolewa utasikia "hujafukuzwa chumba chako kipo"!!! na kwa mume ataleta ujeuri kwa kuwa akirudi kwa wazazi wake anapokelewa, zamani ukiolewa ukirudi kwa mzazi wako unafukuzwa, sasa utoto na ujinga mwingi unaofanywa na wazazi kudekeza mabinti zao,
 
Hee mkuu
Comment yangu umeielewa kweli?
Nampinga mtoa mada anayesema mfukuze binti,
Unafukuzaje mtoto wako.?
Binti akiishi nyumbani kwao ni safe zaidi kuliko kwenda kujitegemea kupanga.

Kila mtu na timing yake kuolewa,, si wote wataolewa under , 25

Na Miaka ya siku hizi ajira zenyewe hakuna
Vijana wa kuoa ndio kwanza bado wanajitafuta,,, mabinti nao hivyohivyo
Halafu eti umfukuze binti yako.

Unakuta mchumba wake ndo huyo wametoka wote kumaliza chuo, wote hata pa kuanzia hawana..halafu unataka umfukuze binti wakati yeye na mchumba wake bado hawajajipanga.
 
Ndo maana nimezipa namba 1,2,3 ili nitoe nami koment kulingana na hoja hizo ulivyoziweka.
Mwisho lakini nimesema binti anaweza kufukuzwa nyumbani kama atamisbehave na hayuko tayari kuonywa. Hii ni conditional; Lakini kwa ujumla ufafanuzi ulioutoa nimekuelewa zaidi.
 
Sema hawara yake
Mchumba haitwi bila kufuata taratibu
Sasa kujipanga maisha yake bado, ataweza kuchumbia?
 
Akimisbehave anatakiwa aonywe kwa adhabu yoyote ila si kumfukuza

Msije kujaribu kuwafukuza watoto nyumbani nyie
Mtatengeneza bomu,,halafu imagine akakumbana na balaa huko nje akapoteza maisha..maumivu yake yatatopoa kamwe.

Ingekuwa wazazi wetu wangekuwa wanatufukuza nyumbani tukikosea basi pengine tungekuwa vibaka au machangudoa..
Mtoto akikosea muonye..
Kuna actions mama wa familia huwa anachukua ni adhabu tosha kwa binti.
 
Kama dada zako tu walivyozalia nyumbani

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mkuu pamoja na sifa unazompa mwanao wa kike ukae ukijua hayo malezi umem spoil sana . Hao ndo madaktari wenye frustration tulionao makazini. Kifupi ni kwamba mzazi ukilea Binti afu asiolewe na ameshafika umri wa kuolewa na amewezeshwa kielimu na kiuchumi kama ulivyo describe ujue umefeli sana. Wote wazazi na mwanao mtakua na stress sana.
 
Siyo sahihi
 
Sasa binti akivuruga utamfukuza nyumbani au kumkanya? Na vipi mwanaume ndo akiwa jeuri napo utamgomea mtoto asirudi nyumbani?
 

Sio kila mtu ataelewa usemalo. Wanawake wengi sana wanapitia unyanyasaji wa kijinsia na kuvumilia hadi wengine kufariki kwa kuhofia kutopokelewa makwao na kuhukumiwa na jamii.
 
Sio kila mtu ataelewa usemalo. Wanawake wengi sana wanapitia unyanyasaji wa kijinsia na kuvumilia hadi wengine kufariki kwa kuhofia kutopokelewa makwao na kuhukumiwa na jamii.

Inasikitisha sana mkuu
 
Kwanini wahenga waliweza kuishi na wake zaidi ya mmoja na wakaelewana kwa muda mrefu? Walifundwa.

Pitia uzi kwa kubofya hapo chini ujifunde kwa kina na upana zaidi kuhusu wanawake / wanaume 👇🏾

 
Mkuu nikweli kabsa, ndoa nyingi zinadumu kwasababu wanawake hawana kipato na hawana njia nyingine ya kuishi zaidi ya kumtegemea mwanaume, na inapelekea mateso makali sana kwa wamama wengi,
Kwa hiyo kumtegemea mume kwa mtazamo wako ni mateso ingawa kama ndivyo unavyoona yafaa zaidi ili izo ndoa zidumu kwa masilahi ya taifa na kizazi kijacho.

Kamwe huwezi mridhisha mwanamke kivyovyote, anatakiwa Aisha bila uhuru uliopitiza ambao kwa mtazamo wako unauita mateso.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…