Mabinti wenye umri wa kuolewa na hawajaolewa wafukuzwe nyumbani haraka

Mabinti wenye umri wa kuolewa na hawajaolewa wafukuzwe nyumbani haraka

Majitu mengine yakishalewa hukurupukia humu kutafutia usingizi. Inawezekana hata mtoto huna.

Zaa wako wa kike uone uchungu wake wa kumzaa, kuhangaika nae na malezi, shule na kuzeekea nyumbani bila kuolewa na umtimue kama una uthubutu huo. Sasa ukishamtimua ndo umejenga au umezidi kumsababishia despression huyo mtoto?!

Hovyo kabisa! 😏😏😏
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Wazazi wamekua wakijitahidi kulea mabinti zao vyema japo Lipo wimbi kubwa sana la wanawake kubweteka na kua malimbukeni kupita kiasi, hali hii imesababisha kujiona wao ni wao na wanaweza kuishi wenyewe bila kua na mwanaume atakae kua kichwa.

Mtazamo huu umechangia sana wanawake wengi kukataa wanaume wanaokuja kuwa chumbia kwa lengo la kuwa oa na kuweka ndani kama mke halali, na hili limechangiwa sana na kuiga wanawake wenzao hasa wanao wadanganya ndoa ni chungu, ndoa ni karaha, mwanamke ni jeshi kubwa, mwanamke anaweza, mwanamke ni mpambanaji na nguvu kubwa sana inayotoka kwa masingle maza walio zalishwa na kuachika kutokana na tabia zao mbaya.

Mabinti wengi sana wameharibika na kuwaharibu wale wenzao wachache walio salia salia na tabia njema, inasikitisha sana kukuta binti wa miaka 15+ anao mtazamo wakuja kuishi mwenyewe bila mwanaume naye anasema hataki kuolewa, tena anafika mbali zaidi ana kuambia nitazaa tuu na nitalea mwenyewe. Hebu jiulize hii elimu au huu mtazamo kaupata wapi kama sio kutoka kwa wanawake wenzake/ mabinti wenzake / hawa hawa masingle maza wanao ongoza kuharibu mabinti kwa kuwaambia kuishi na mwanaume ni utumwa.

Swala hili limesababisha sana wanawake wengi/ mabinti wengi kwa sasa kukataa wanaume pale wanapotongozwa kwa nia ya kuolewa na wengine kufikia mbali kutaka tuu mbegu na ukimpa mbegu hapo anakuona wewe huna thamani tena na sio kitu. Wengine wanakataa wanaume mpaka wanakuja kujutia ukubwani anapopita umri wa kuolewa nakuja kugundua kwamba walidanganyika na hawawezi tena kurudisha siku nyuma kutokana na kupoteza mvuto kwa mwanaume na hivyo kubaki kwa wazazi wao, majumbani au kwenye himaya za koo zao, ndugu jamaa na marafiki wakiwa magroup kwa magroup huku wakiendelea na kuharibu mabinti wanao chipukia wenye nia na ndoto za kuolewa na kuishi mume na mke.

Hivyo kama unaye binti au unaye mwanamke ambae hajaolewa nayupo katika umri wa kuolewa huyo ni hatari kwa kizazi cha mabinti wa sasa huyo mfukuze nyumbani acha maramoja kumchekea chekea hakika kwa kufanya hivyo ulimwengu utamchapa na hamu ya kuolewa itamjia na atajifunza mengi sana kuhusu maisha ya upweke kwa kweli.

Mfukuze kabisa nyumbani mwache ulimwengu ukamfunze thamani ya kuwa na mwanaume na kuolewa na ukamshape namna ya yeye kubehave kama mwanamke mbele ya wanaume.
Kwanza jiulize,hao mabinti "wanaokataa kuolewa"wanatoka katika malezi gani,familia zipi?
Ni familia zilezile zinazolea watoto wa kiume kama mandezi,mayai!
Wewe una watoto wa like na kiume,na wote unawalea kindezi ndezi,wa kike unamlea kama feminist,wa kiume analelewa kama yai,sasa nani atakubali kuoa femenist,na nani atakubali kuolewa na mwanaume mwenye akili za mvulana,ana miaka 25,lakini hawezi kufanya maamuzi mpaka amuulize mama yake!!
Kuwafukuza nyumbani sio suruhisho,wa kiume mjengee uchumi mzuri awe na pa kuanzia,ndoa ni gharama,na WA kike vilevile mpe uchumi Bora,na afundishwe kuchagua mume Bora,sio kuolewa na Hawa wanashinda mitandaoni,kijana mpaka anamaliza kidato Cha tatu,hajui atasoma nini chuo kikuu,
Wapo vijana wenye akili,
 
Kujitegemea atajitegemea lakini si kumfukuza eti akaolewe? Ndoa zenyewe hizi🙄
Ataenda kujitegemea akitaka na ataolewa akitaka. Asipotaka akae hapo nyumbano hadi azeeke.
Hukumuelewa mleta uzi anamaanisha unakaa nyumban na una umri wa kuolewa na bado anakaa nyumbani anamfukuza
Lakin kama anajitegemea na hakai nyumbani na hajaolewa huu uzi haumuhusu
 
For the moment i thought ur my dad....mwezi mmoja uliopita aliniambia maneno kama haya. Big up mkuu [emoji122][emoji122][emoji122]
May be I am. Hizi ID fake hizi huwezi jua....[emoji16][emoji16][emoji16]

[emoji3591][emoji3591] Baba yako ni mtu mwema na anajua maana halisi ya kuwa baba hasa kwa mtoto wa kike maana dunia hii ya sasa ina challenge nyingi sana kwenu mabinti. Baba anapaswa kuwa kama lighthouse kwa binti yake - taa ya matumaini inayong'ara sana na kumwongoza kila aendako huku akijua kuwa anaweza kurudi katika mwanga ule wa upendo wakati wo wote meli yake ya maisha ikikumbana na mawimbi makali huko katika bahari-dunia.

We are called dads for a reason, baby! [emoji123][emoji123][emoji123][emoji1545]
Screenshot_20230326_180735_Chrome.jpg
 
Majitu mengine yakishalewa hukurupukia humu kutafutia usingizi. Inawezekana hata mtoto huna.

Zaa wako wa kike uone uchungu wake wa kumzaa, kuhangaika nae na malezi, shule na kuzeekea nyumbani bila kuolewa na umtimue kama una uthubutu huo. Sasa ukishamtimua ndo umejenga au umezidi kumsababishia despression huyo mtoto?!

Hovyo kabisa! [emoji57][emoji57][emoji57]
Mkuu ni kweli...baba mwenye mtoto wa kike hawezi hata kuwaza huu upuuzi. Baba zetu wanavyotupenda[emoji7]
 
Mkuu ni kweli...baba mwenye mtoto wa kike hawezi hata kuwaza huu upuuzi. Baba zetu wanavyotupenda[emoji7]
Si wote. Mababa wendawazimu bado wapo dunia hii hii wana-exist

Kuna ndugu aliletaga uzi jinsi alivyokutana na mkewe humu. Ni kisa cha kusikitisha sana!

Binti alikutana na jamaa maeneo ya nyumbani kwao nje kidogo hapohapo mtaani kuna duka. Binti aliagizwa, akakutana na jamaa. Kwakuwa jamaa hakuwa anajua kiswahili vyema ikawa shida kuongea na mangi... mangi akamuomba msaada binti awe kama translator wake kwa kipindi kile kifupi pale dukani. Baada ya kumaliza kuwa kama mtafsiri akaaga akasepa. Mu-ethiopia akampa ki-memo binti kilichosomeka...

"meet me at hall six, 4tg floor (UDSM) on saturday. I'm having your gift" na nambari ya simu.

Binti akajua ni zali hili... hapo yupo form four

Binti alienda kumtembelea muethiopia hostel za UDSM siku husika. Bahati mbaya au nzuri binti hakuwa na dhana mbaya alihisi ni zali kapata rafiki kutoka nje akawa na illusions. Kufika jamaa alikuwa peke yake mazungumzo yalikolea mwisho akamlazimisha tendo, binti hakuweza kubana akabakwa 😔😔😔

Akaondoka akiwa kakasirika sana na akakata mazoea na mawasiliano na yule muethiopia... kumbe alikuwa kashajazwa mimba. Masiku na mamiezi kupita mama wa binti alimtazama mwanae akagundua ndipo binti akalia sana na kufunguka lkn ilikuwa too-late! Baba wa binti alikuwa mwanajeshi mkubwa na mkali sana! Mama na mwana ikawa vilio na kujadili cha kufanya na jinsi ya kufikisha kwa baba mtu hatua ichukuliwe. Baba mtu baada ya kuambiwa akamtimua mwanae. Na hakumtafuta tena! Mtoto alienda kulelewa na watu baki. Na mpaka leo hakujua tena wazazi wake qashakufa au wapo hai. Na wazazi hata hawajui mtoto yupo wapi ila tayari ana kazi yake na yupo serikalini, ana familia na alishagaolewa. Maisha safi! Yupo Dodoma.

Alizaa mtoto wa kike wa yule muethiopia ni kisu balaa!
 
Habari za wakati huu ndugu zangu.

Wazazi wamekua wakijitahidi kulea mabinti zao vyema japo Lipo wimbi kubwa sana la wanawake kubweteka na kua malimbukeni kupita kiasi, hali hii imesababisha kujiona wao ni wao na wanaweza kuishi wenyewe bila kua na mwanaume atakae kua kichwa.

Mtazamo huu umechangia sana wanawake wengi kukataa wanaume wanaokuja kuwa chumbia kwa lengo la kuwa oa na kuweka ndani kama mke halali, na hili limechangiwa sana na kuiga wanawake wenzao hasa wanao wadanganya ndoa ni chungu, ndoa ni karaha, mwanamke ni jeshi kubwa, mwanamke anaweza, mwanamke ni mpambanaji na nguvu kubwa sana inayotoka kwa masingle maza walio zalishwa na kuachika kutokana na tabia zao mbaya.

Mabinti wengi sana wameharibika na kuwaharibu wale wenzao wachache walio salia salia na tabia njema, inasikitisha sana kukuta binti wa miaka 15+ anao mtazamo wakuja kuishi mwenyewe bila mwanaume naye anasema hataki kuolewa, tena anafika mbali zaidi ana kuambia nitazaa tuu na nitalea mwenyewe. Hebu jiulize hii elimu au huu mtazamo kaupata wapi kama sio kutoka kwa wanawake wenzake/ mabinti wenzake / hawa hawa masingle maza wanao ongoza kuharibu mabinti kwa kuwaambia kuishi na mwanaume ni utumwa.

Swala hili limesababisha sana wanawake wengi/ mabinti wengi kwa sasa kukataa wanaume pale wanapotongozwa kwa nia ya kuolewa na wengine kufikia mbali kutaka tuu mbegu na ukimpa mbegu hapo anakuona wewe huna thamani tena na sio kitu. Wengine wanakataa wanaume mpaka wanakuja kujutia ukubwani anapopita umri wa kuolewa nakuja kugundua kwamba walidanganyika na hawawezi tena kurudisha siku nyuma kutokana na kupoteza mvuto kwa mwanaume na hivyo kubaki kwa wazazi wao, majumbani au kwenye himaya za koo zao, ndugu jamaa na marafiki wakiwa magroup kwa magroup huku wakiendelea na kuharibu mabinti wanao chipukia wenye nia na ndoto za kuolewa na kuishi mume na mke.

Hivyo kama unaye binti au unaye mwanamke ambae hajaolewa nayupo katika umri wa kuolewa huyo ni hatari kwa kizazi cha mabinti wa sasa huyo mfukuze nyumbani acha maramoja kumchekea chekea hakika kwa kufanya hivyo ulimwengu utamchapa na hamu ya kuolewa itamjia na atajifunza mengi sana kuhusu maisha ya upweke kwa kweli.

Mfukuze kabisa nyumbani mwache ulimwengu ukamfunze thamani ya kuwa na mwanaume na kuolewa na ukamshape namna ya yeye kubehave kama mwanamke mbele ya wanaume.
Mimi nitamwambia mapema kama unataka kuzaa nenda kwako ila kuzalia nyumbani niwe nalisha Mimi Hilo hapana nitamtimua.

Labda nijihakikishie kwamba anaweza ku provide msosi Kwa huyo mjukuu wa kuokoteza 🤪😜
 
Yaani mzazi amfukuze mtoto? Nani sasa atakaye mpokea kama wazazi wamemfukuza, nadhani kumfukuza ndio hatari sana kwa jamii kuliko kubaki nyumbani...
Akajiyegemee,kwani nani hakuwahi kuwa mtoto? Utoto una kikomo Cha utegemezi.
 
1. Ina fuatana na mazingira mfano binti kama hajapata mtu wa kuja kumchumbia hapo ukimfukuza utakuwa kichaa tena kichaa kwelikweli.

2. Ila binti yangu akiwa na tabia ya kuwakataa wanaume wa maana wanao kuja kumchumbia na kumpa thamani ya kuwa mke, badala yake anaenda kuliwa hovyo na mabodaboda na masharobaro mitaani hata mm kwangu hakai ,na ww mzazi ukimdekeza binti mwenye akili za kipumbavu kama huyo utakuwa una pwaya sana.

3. Binti una miaka 23 husomi ,huna kazi inayo kupa kikwazo cha kuolewa, sio mgonjwa, wanaume wa kukuchumbia unawapata na bado hutaki kuolewa ww kama si malaya tukuiteje?
Nimezipa namba hizo paragrafu ili tuweze kwenda sawa.
1. Naunga mkono hoja hiyo 100%. Safi sana.
2.Binti yako kama ni mtulivu na sio kiruka njia, anaweza kumkataa mwanaume anayekuja ambaye wewe unamwona wa maana lakini huwezi kujua sana kwa undani ni kitu gani hasa kilichopelea yeye akamkataa. Usimshinikize kuingia kwenye ndoa na mwanaume bila hiari yake huyo binti. Wewe ninaamini ni Me. Hebu waangalie vijana hawa tunaowaita vijana wa dotcom a.k.a Kizazi kipya. Hana vision yoyote, hana kitu cha kusema hichi hapa ni changu 100% yan tunasema bado anakula ugali wa shikamoo. Je, akija kumchumbia binti yako utaridhia kama mzazi? Huyo anaficha ukweli kwamba anachotaka ni kumlaghai binti yako kwa mwamvuli wa kuoa lakini ukweli anatafuta pa kusuuzia rungu tuu. Akisha mla anaingia mitini. Mimi ninadhani cha msingi hapa ni nyie wazazi esp.Baba kusaidia binti aweze kufanya maamuzi sahihi kwani maisha ya ndoa ataenda kuyaishi yeye mwenyewe.
Sishauri sana au sipendekezi mama amsaidie binti kwa sababu akina mama wamekuwa wakati mwingine ndo chanzo cha mabinti kupotea au kufanya maamuzi yasiyo sahihi na chanzo cha ndoa/mahusiano ya mabinti zao kuharibika au kuvunjika(Samahani kina mama ila ninao uzoefu wa kutosha kwenye hoja hii)
3.Nashauri Binti aonyeshwe upendo hapo nyumbani na kamwe kusiwe na namna yoyote ya kumshinikiza eti aolewe kisa ni umri unaenda. Kumbuka kosa la siku moja ie.siku aliyokubali na kusema NDIYO inaweza kumgharimu maisha yake yote yakawa ni maisha yaliyojaa misukosuko, masononeko makubwa, simanzi na majuto maisha yake yote. Mbona huo umri wa 23yrs sio wa kutisha sana ukizingatia uamuzi wa busara hautachukua hata mwezi mmoja? Kingine huyo binti ahimizwe tu kuwa na hofu ya Mngu asikimbilie kula tunda kimasihara. Ikiwa ni mla tunda hata mimi ningemtimua asubuhi na mapema sana kwani atasababisha balaa hapo nyumbani na familia kwa ujumla.
 
Nyie mnaosema wanawake wanakataa Wanaume Ni uongo mtupu labda mnazungumzia maeneo ya vijijini lakini huku mjini Hakuna waoaji tuache uongo hata sisi tuna dada zetu tunajionea.
Wanawake wanakataa wanaume mkuu, dada zako wachunguze vizuri sio kwamba hawapati wakuwaoa.. wanakataa na wanachagua sana.. amini nakuambia mkuu
 
Unamfukuza nyumbani kwako ili akawe Malaya?
Unamfukuza kwako ili akaharibike na kufanya kazi zisizo na stara?
Unamfukuza kwako ili akawe Cha wote?
Unamfukuza kwako ili iweje?
Binti akitoka kwa baba basi anaenda kwa Mume unless kazi yake iwe mbali.

N.B Alikosa Mume wewe mzazi unalazimika kumtafutia Mume ili apate stara.
 
Ni kweli mwanamke ana haki ya kukataa wanaume, ila anatakiwa afahamu ni ngumu sana kupata mwanaume anayemtaka yeye in short ana limited option ni tofauti na mwanaume

Hata ukiwauliza wanawake walio wengi ambao wako kwenye ndoa watakuambia waume zao in first place waliku hata hawawapendi kihivyo ila walikuwa hawana jinsi ikabidi wawakubalie
Mkuu usituingize chaka
Ushauri wako unaweza kuwa mzuri kwa namna moja, pia ukawacost watu kwa namna nyingine.
Mtu anaweza kimbilia kuolewa na yeyote,baadaye akaja kujuta.
 
Ukiangalia wanyama wanatabia ambazo nazipenda sana mtoto akifikia umri flani anafukuzwa na yeye aende akapambane na maisha yake sio kwamba hawampendi anatakiwa ajitegemee ni lazima sio option

Mtoto anamiaka let say 25, wengine mpaka 40 wanakaa nyumbani comfortable na mzazi anaona ni sawa ndo maana kizazi hiki ni dhaifu sana
Tuende wapi sasa?
Unataka tukapange?
Mtoto wa kike kwenda kupanga ni balaa jingine hilo.
 
Wanawake wanakataa wanaume mkuu, dada zako wachunguze vizuri sio kwamba hawapati wakuwaoa.. wanakataa na wanachagua sana.. amini nakuambia mkuu
Kwahiyo aolewe na yeyote tu hata kama hafai?
 
Mkuu usituingize chaka
Ushauri wako unaweza kuwa mzuri kwa namna moja, pia ukawacost watu kwa namna nyingine.
Mtu anaweza kimbilia kuolewa na yeyote,baadaye akaja kujuta.
"Mtu anaweza kimbilia kuolewa na yeyote,baadaye akaja kujuta".
Yes! Tena majuto makubwa sana. Ndo maana unakuta wengine ndoa zao hazidumu hata miaka 5 kutokana na yale Madhila, Kero na Mapungufu ambayo binti anayagundua baadaye ambayo mwanzoni yalifichika kwa huyo mumewe. Kumbuka wanaume wengi hujivika roho ya uungwana wakati wa kutongoza,kuchumbia lakini ikishakuwepo ndoa hapo wanaonesha makucha yao halisi. Wengine hufikia hatua ya kuwaua wake zao, kuwajeruhi n.k. achilia mbali kuchepuka kulikokithiri huku wakiwalazimisha wake zao wawe wavumilivu. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom