Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mabomu hayo yamepigwa baada ya kumalizika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Pamba Jiji dhidi ya Simba SC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Baada ya mchezo kumalizika mashabiki wa simba wameonekana kutoridhishwa na matokeo hayo huku wakimtupia lawama mwamuzi kwa kutowatendea haki katika baadhi ya matukio.
Ambapo imshuhudiwa mashabiki hao wakiwatupia makopo ya maji waamuzi wakati wa kuingia vyumbani baada ya mchezo huo.
Polisi wametumia mabomu hayo takribani matatu ili kuwatawanya na kuwalazimisha kuondoka uwanjani.
Hata hivyo, mashabiki wawili kutokana na vurugu hizo walipoteza fahamu na kukimbizwa kwenye gari la wagonjwa kupewa huduma ya matibabu.
Hata hivyo baada ya dakika chache hali imerudi kama kawaida baada ya polisi kuacha kupiga mabomu na kuwaacha mashabiki hao waondoke taratibu.
Ni mchezo wa pili mfululizo unaoihusisha Simba unashuhudiwa jeshi la polisi likitumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki. Ambapo wiki iliyopita katika mchezo ulioahirishwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mabomu ya machozi yalipigwa kuwatoa mashabiki uwanjani.
Pia soma: FT: Pamba SC 1-1 Simba SC | NBC Premier League | CCM Kirumba
Chanzo: Nipashe