Mabomu ya Machozi yatumika kuwasambazi wananchi pamoja na Wanafunzi Mjini Dodoma


lakini TBC1 wanaripoti kuwa wanafunzi wa UDOM walifika pale ukumbini asubuhi na mapema; kilichofuata ni mchujo. wakawa wanazuiwa wasiingie.

we cannot go like this.
 

Haaaa,hawakuwa na namna ingine ya kuwazuia jamani?
Hao polisi sijui ndo hawana shida na katiba mpya au ?
 

Naunga mkono hoja, public hearings is not enough, itumike njia nyingine kuwapata watu wengi zaidi. mtandao uandaliwe kwa watumiaji watoe zao hisia.
 
Daaah kaz kwel kwel! Huyo ndo Jk na CCM yake! Kitaelewaka tu watake wactake!

post kama hizi huwa zinanikera ile mbaya, na zinanikera hivi: kosa alifanye mwingine halafu alaumiwe mtu mwingine kisa tu huyo unayemlaum una chuki nae, this is not fr. Katika hili mimi kilio changu naomba aliye panga mdahalo ufanyikie sehemu ambayo haitoshi watu wengi. Ivi wewe sweet unataka kuniambia Jk ndio alichagua huo ukumbi au ndiye katoa sauti kuwa FfU piga hao. nakuomba uache ulimbukeni huo. jana niliona mtu mwingine wa sampuli yako eti mtoto wake kapata Division four kisha anamlaumu Jk na anadai kama slaa tungemruhusu kuwa rais eti mwanae angepata Dvsn One, mawazo kama haya naona mtu huwa anayatype baada ya kuvuta bangi
 
kwanza kwanini public hearing dar na dom peke yake?
 
imenibid nifatile kesi ya wale wakenya kutoka kule the hegi......citizen tv ya kenya wako live ..na sasa ruto anasomewa mashataka yake...hapa kwetu ubabaisha mwingi
 
Naunga mkono hoja, public hearings is not enough, itumike njia nyingine kuwapata watu wengi zaidi. mtandao uandaliwe kwa watumiaji watoe zao hisia.
its a gud idea, tatizo ni mtandao gani utumike? mie naona wafanye kama vile Shabani Kisu alivyokuwa akiendesha mchakato majimboni,so this time iwe hadi kila kijiji kuwe na mdahalo na yote iwe recorded, na wasimamizi watoke taasisi zote na vyama vya siasa visioneshe interest zao, viongozi wa vyama wachangie kama wananchi rais naye achangie kama mwananchi tu.
 

Angalizo wasiandae watu maalum kutoa maoni
 
Haaaa,hawakuwa na namna ingine ya kuwazuia jamani?
Hao polisi sijui ndo hawana shida na katiba mpya au ?

Polisi wa Tanzania wapo kama Roboti ambapo wakijiload tu, kinachofuata ni kusikiliza sauti ya piga. Bila huruma, wanapiga dungu zao, watoto wao, jirani zao na jamaa zao. Na hii inasababisha na mufumo wa utawala tulionao [Raisi, Jeshi, Polisi, etc] kutokuamini kwamba watanzania wamebadilika sana, wanajua haki, kupigania nchi yao na wala hawadanganyiki tena. Hawa watawala bado wanatumia njia ya kuwatisha kwa mabomu n.k bila kujua kwamba ndo wanawachochea kabisa. Na huo uchochezi ndo unongeza nguvu za kuwapinga ambapo nguvu kubwa zaidi itakapotumika kutoka kwa wananchi ndipo wataamini kwamba watanzania wamebadilika kweli. Wakati huo watakuwa wamechelewa sana kwani uongozi utakuwa mikononi mwa watanzania wenyewe.
 
Sio kweli Muhosin, Ukumbi hautoshi wangekaa wapi? na bunge ni sehemu ya kuheshimiwa wao wana mabango wanawaza vurugu tu, katika hili natetea kwasababu nashuhudia, ukumbi ni mdogo, kosa labda ni kuchagua ukumbi that all.

Remmy nakubaliana na wewe kwamba ukumbi ni mdogo. Mimi niliposikia kwamba itafanyika Msekwa nilishangaa kama walipanga wanajua nguvu ya umma inayoshiriki katika huu mswada. Pale Mkuruma serikali iliambiwa kwamba public hearing ya mara moja na inayofanyika dodoma siyo haki, kama kawaida yao wakapuuzia.

Tatizo langu Remmy ni nia na uwezo wa serikali. Hakuna jambo moja ambalo mimi nalifahamu ambalo serikali ilipanga vizuri bila kudhulumu haki za raia, kudharau mawazo ya wananchi, na kuwakandamiza kwa kutumia mabavu. Serikali haikutakiwa kuendesha mchakato huu kwa ad-hoc planning. ilitakiwa kusikiliza wadau wanasema nini na itekeleze

Serikali haikutakiwa kuwanyanyasa wananchi waliofika dodoma kwa namna yoyote ile. Haikuwalipia gharama yoyote! Siyo kosa la mwananchi aliyetoka Tanga kwamba ukumbi hautoshi wakati ameshajiandaa point zake anazotaka kuzisema na ametumia gharama.

Baada ya serikali kuchemsha kuhusu kushindwa kuwapatia wananchi fursa ya kuingia ukumbini, ilitakiwa iwabembeleze na kuwatuliza kwa busara siyo mabavu na mabomu na kauli za amri. Serikali ilitakiwa kwa haraka sana ikodi ukumbi mwingine na kuwapeleka hao wanaharakati na kuandaa utaratibu wa kuwasikiliza. Kwa bahati mbaya serikali inafikiri kutumia polisi kila inaposhindwa kuhudumia wananchi

Remmy naomba pia ufute fikra kwamba walio nje ya ukumbi wa bunge ni wanafunzi wanaofanya fujo na vurugu. Pattern yako ya kufikiri hasa ndivyo ya serikali na ccm, kwamba yeyote anayejieleza kinyume na utawala unavyotaka anafanya fujo. Nje ya viwanja vya bunge pia kuna watu wazima na heshima zao, wengine ni wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na wengine ni viongozi wa dini. Wote wamezuiliwa kuingia na wamechanganyikana na wanafunzi kwa sababu ni swala la haki siyo "heshima na amani"

Kama serikali haikutaka wananchi wafanye fujo, kwa nini hawakutekeleza maoni mazuri kabisa yaliyotolewa Nkuruma na ambayo yameendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari hadi leo? Serikali ingekuwa sikivu na inayojali amani, baada ya mjadala wa Nkuruma tu ilitakiwa irejeshe huo mswada kuandikwa upya badala ya kuendelea kukejeli na kudhihaki wananchi eti inakusanya maoni ya mswada mfu!

Mwisho naomba nitofautiane na wewe kwamba bungeni ni mahali pa kuheshimiwa kwamba mabango eti yanavunja hiyo heshima. Hizi ni fikra za kale sana, nasikitika kusema hivyo. Bungeni ni mahali pa uhuru wa kujieleza usiotakiwa kuzuiliwa kwa namna yoyote ile. Kubeba mabango kunavunja vipi amani? Hata kufanya maandamano ndani ya viwanja vya bunge kunavunga vipi amani?
 
Tatizo ni pale walipoonyesha upendeleo kwa hao vijana wa sekondari wa city lakini wangeingiza watu waliokuwa wamepanga foleni idadi ikitimu wakasema basi labda wangeepusha shari hii,hivi vitu vya public hearing huwezi kuanza kwa kuwa na walengwa wako halafu ukasema ni public hearing nadhani wamepata fundisho kwamba hata siku moja wasidharau wananchi vinginevo kila kitu wanachokifanya kinyume kitakutana na resistance kubwa kutoka kwa wananchi ,tayari wanao ufahamu mkubwa kwamba mamlaka wa mustakabali wa nchi yao uko mikononi mwao hapo ndio ngoma watapiga watu mabomu risasi na washawasha lakini haitawazuia hata kidogo kutafuta haki yao ningekuwa mimi muandaaji ningeandaa eneo kubwa la wazi kuruhusu kila mtu
 
ebu tueleze uhalisia wa ukumbi kama unaweza kuwachukua wabunge wote na wananchi walioko hapo. na kama ni mdogo aliyepanga kufanyikia ukumbi huo ajieleze maana amehamasisha mambo ambayo hatuyahitajii kwa sasa. mambo ya mabomu yanakera kuyasikia

Walihasisha bila kudhamiria wakijua watu hawata itikia then waseme tulihamasisha na watu walitokea na maoni yao ndiyo tumeyachukua; kumbe wao wameweka watu wao wakusema ndiyo mheshimiwa fanya haraka!
 
nilikuw po nje na nilikuwa mmoja wa wanaharakati walokuwepo, asubuhi hatukujibiwa kuhusu udogo wa ukumbi bali tuliambiwa tutaingia kwa vitambulisho pia wakaja na w
nachuo waandike majina mara wakasema kila chuo waingie watu 10, chaajabu uvccm wachache a wamama flani flani wakapitishiwa mlango wa nyuma wadau tulipogundua hilo tukazunguka na kule nyuma wakafunga mlango , cha ajabu ni kwamba ukumbi hata kama ulijaa basi ni wale wageni rasmi walopewa mwariko ambao ni wanafunzi wa shule za sec. jamuhuri na city pia wale wamama mahususi jiri ya vigeregere. hakuna kulala kitaeleweka tulianza mchakatuo pale pale bungeni nje kuujadiri huo mswada kama mapanki.
 
Wel,dats wat it got 2b when ua desperately runing against time!!
 
Mabomu watatupiga,watatuua...lakini lazima watupe nchi yetu...
 
Hivi ilikuwaje JF haikupatikana kwa muda wa masaa mawili? Au hujuma ilikuwa watu kushindwa kupata habari ontime? Nilitaka niwashe gari kwenda dodoma muda ule,sema sikuwa na taarifa kamili..
 
mwaka huu kazi ipo, hiyo katiba lazima watu wachache wafe kwenye vurugu ndipo tutaipata, hiyo mirungu ni mwanzo tu hadi katiba ipatikane wengine wameshaingia magerezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…