Maboresho katika sekretarieti ya ajira: Kwanini mtu wa 'degree' asiruhusiwe kuomba kazi za wenye 'diploma'?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
 
Tofauti ya Diploma na degree
1. Salary
2. Skills
Sasa mtu kama kaona anaweza kuomba kazi inayotaka Diploma kwanini asiruhusiwe si maamuzi yake??.

Mfano Dereva wa Bus umkataze asiendeshe IST, utumishi wanafeli sana hapa.
Hapo ndio wanafeli sana na pengine kwa kufanya kazi huku kuna siku itakuja kufutwa
 
Ni sheria za kazi ndo zinawaelekeza hivyo na malipo kulingana na elimu ulio nayo
Diploma ni elimu ya chini kwa degree hivyo mwenye degree ana uwezo mkubwa kiufanisi na kiutendaji. Ndio maana nimesema Kama kuna sheria au utaratibu uangaliwe ili kupata watu wenye ufanisi makazini.

Haiwezekani tunawaacha wenye degree na Elimu za juu na kuajiri wenye diploma huku tunajua wanaweza wakaleta ufanisi zaidi.

Mashirika binafsi yanasema 'at least' awe na diploma maana hawafungi upande mmoja
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
sasa Je zikitokea Ajira za wenye Degree mwenye Diploma ataweza kuomba hiyo Ajira ?

mfumo naona Upo sawa shida inakuja kwa wewe mlengwa anapokoswa na Vigezo vya msingi.

hata Recruitment portal za majeshi , kuna space kwa Ajili ya form 4 , Certificate , Diploma , and Degree.

" "The world is not flat but spiky and that creates many opportunities to everyone"
 
Au unakuta Kuna ajira ya certificate ila kwa kuwa mtu uliunga hadi degree ,basi qualifications ya certificate uwezi apply wakati ume attach certificate,dip and bachelor Ila wao Wana consider elimu ya bachelor tu ,dip.au certificate uliyo attach uwezi ku apply ,wabadilishe mfumo.kwa kweli kwa mtu alieanzia certificate hadi degree
 
Mwenye diploma ana degree mpaka afanye maombi ya kazi inayomfaa mwenye degree? Lakini mwenye degree anaweza kufanya ya mwenye diploma kwa sababu diploma ni kiwango cha chini Cha elimu kuliko Diploma.

Hii ndio itakuwa ni njia rahisi ya kufanya mtu kujiendeleza kielimu kama ataona akiwa na diploma hawezi kushindana na wenye degree kwenye mchakato wa ajira.

Umezungumzia jeshini kama mfano lakini utambue mwenye cheti Cha kidato Cha nne hawezi kufanya kazi za kitaalamu jeshini lakini diploma na degree ni level za ujuzi na utaalamu na ndio maana ajira zao kidato Cha nne hawawezi kufanya.
 
Au unakuta Kuna ajira ya certificate ila kwa kuwa mtu uliunga hadi degree ,basi qualifications ya certificate uwezi apply wakati ume attach certificate,dip and bachelor Ila wao Wana consider elimu ya bachelor tu ,dip.au certificate uliyo attach uwezi ku apply ,wabadilishe mfumo.kwa kweli kwa mtu alieanzia certificate hadi degree
Haya ndio ya kufanyika ,Kama Taifa hatutakiwi kuonyesha huruma kwenye eneo hili. Hapo wameangalia usawa lakini lazima tuangalie zaidi ufanisi
 
nimesoma Diploma, na nimesoma Degree ya Uhandisi
hii ndiyo tofauti niliyoiona, na najibu kwa upande wa kada yangu

wa Diploma yuko ki hands-on, amesomea praki (na theories) miaka yote X
wa Degree hawezi kava nafasi ya Diploma, maana yeye kule amekunywa theories tupu (tena zisizo na uhalisia kabisa kwenye mazingira ya kazi) , hata wire wa 2.5mm² hajui unafananaje
 
Kwa hiyo unataka kusema Elimu ya diploma ipo juu kuliko degree na kwenye soko la ajira aangaliwe mwenye diploma zaidi? Hii ndio nchi yangu
 
mwenye diploma ndiyo mzalishaji
nenda kiwanda chochote, angalia idadi ya wenye diploma mathalan, sekta ya uhandisi
unakuta mafundi ni 10 (diploma), engineer 1(degree) ambaye anajaza/saini logbook tu

theories kajaza ujinga ujinga wa electromagnetism , lakini kiwandani anakutana na PLCs, hata kuiprogram hajui
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
Wewe unaona ni sawa?
 
nimesoma Diploma, na nimesoma Degree ya Uhandisi
hii ndiyo tofauti niliyoiona, na najibu kwa upande wa kada yangu

wa Diploma yuko ki hands-on, amesomea praki (na theories) miaka yote X
wa Degree hawezi kava nafasi ya Diploma, maana yeye kule amekunywa theories tupu (tena zisizo na uhalisia kabisa kwenye mazingira ya kazi) , hata wire wa 2.5mm² hajui unafananaje
Na kujidai dai wakati hakuna anachojua zaidi ya design ya makaratasi
 
Hakika Rais Samia anaona na anapitia huku , kwa mabadiliko aliyofanya kwa kumuamishai waziri Simbachawene utumishi ninaamini ni kutokana na Jambo hili.

Nakuomba Mhe. Simbachawene ,wewe ni mwanasheria na unazijua sheria. Naomba kafanyie kazi suala la utumishi kuzuia wenye degree kushindwa kuomba kazi za diploma , Mungu akutangulie.
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
Degree ni Managerial level wanaowasimamia hao wa Diploma na Certificate.

Sasa ukiajiri woooote wa Degree hao wa Diploma (ambao ni wengi) watasimamiwa na wataajiriwa na nani???

Kama una degree pambana na degree yako vinginevyo irudishe chuoni wakubadilishie wakupe DIPLOMA.
 
Kitu kingine ambacho naona ni changamoto kwenye ajira portal ni utambuzi wa “post graduate diploma”. Hili nalo wakaliangalie.

Mtu mwenye hii kitu apewe nafasi sawa na yule alisoma shahada ya fani husika.

Mfano mtu mwenye shahada ya rasilimali watu akasoma post graduate ya Business administration awe na sifa ya kuomba nafasi yenye sifa inayomtaka mtu mwenye shahada utawala ktika biashara.
 
Kuna jambo gumu kidogo kuhusu sekretarieti ya ajira hususani kwenye ajira zinazowahusu diploma huku wenye 'degree' wakizuiwa kuomba wakati mwenye 'degree' anaweza kuleta matokeo na ufanisi mzuri zaidi.

Ombi langu kwa sekretarieti ya ajira na Serikali fanyeni mabadiliko ya sheria au utaratibu unaouzuia jambo hilo ili vipaji vya wenye "degree" vitumike mahali popote
Nani kakudanganya kuwa wenye degree wanaleta ufanisi mzuri zaidi?kwani kinacho leta ufanisi ni degree au ni hulka ya uwajibikaji aliyo nayo mtu? Usikalili mzee hizo PhD , Masters, degree ,diploma arrogances zinasumbua sana na kukwambisha hili taifa kwa miongo mingi sana matokeo yake nchi imejaza mavyeti
mavivu maofisini.
 
Degree ni Managerial level wanaowasimamia hao wa Diploma na Certificate.

Sasa ukiajiri woooote wa Degree hao wa Diploma (ambao ni wengi) watasimamiwa na wataajiriwa na nani???

Kama una degree pambana na degree yako vinginevyo irudishe chuoni wakubadilishie wakupe DIPLOMA.
Sijasema wote wawe ni degree ila mchakato uruhusu hata wenye degree kufanya application.

Kwa kufanya hivyo tunasaidia kundi kubwa la wasomi kutumika kwenye utumishi lakini leo tunaona kuna wasomi wa degree ambao Kimsingi ni muhimu na bora zaidi. Pengine kwa kufanya hivi tutaongeza uwajibikaji na matokeo bora zaidi
 
Back
Top Bottom