Mabosi waeleza kwanini wanawafukuza kazi Gen Z miezi michache baada ya kuajiriwa. Gen Z chukua notes

Shida ni kwamba Maboss wengi kwenye organizations na makampuni bado ni millennials wanashindwa kucope na kukubali kuwa dunia imebadilika kwa sababu wengi wao ni very conservative. Gen Z ni kizazi kimelelewa na kukuzwa kwenye mazingira tofauti they don't have to go through whatever their bosses went through.
Kwa mfano hapo kuchelewa kazini, mtu unaweza kuwa kuwahi kazini na usiwe productive, kwanza dunia imebadilika there is no point kuwahi kazini saa kumi na moja asubuhi wakati kazi zinaweza kufanyika remotely au online na zikaenda.
Kingine Gen Z ni kizazi ambacho wako very open minded na hawajalelewa kwenye mazingira ya uoga shida ya maboss wanataka kuogopwa na kunyenyekewa ndo maana wanaona Gen Z hawana adabu mambo ya "Yes Sir or Madam" ndo wanayataka. The world has changed and it is still changing

Sasa wawasubiri hao Gen Alpha ndo watajua hawajui πŸ˜€
 
Kaka hiki kizazi hakijui thamani ya kupewa nafasi
 
Upo sahihi, alafu mabosi wanasahau kuwa hata wao pia walikuwaga ni fresh graduates na walilelewa na kufundishwa kazi mpaka hapo walipofikia.
 
Hata wewe pia ulikuwa kama wao. Acha kujizima data.
Sema mimi swala la kuita boss ofisini ndo Sinaga Ila kwenye biashara yangu wateja wote nawaita boss Ila nikienda hata TRA nikakuta boss namsalimia kulingana na tofauti ya umri wetu brother, mama, baba, mzee Ila sitamki neno boss
 
Sema mimi swala la kuita boss ofisini ndo Sinaga Ila kwenye biashara yangu wateja wote nawaita boss Ila nikienda hata TRA nikakuta boss namsalimia kulingana na tofauti ya umri wetu brother, mama, baba, mzee Ila sitamki neno boss
Kwa TRA, wewe ndiye unayepaswa kuitwa boss
 
Kusema boss ni kupiga magoti kivipi Mkuu, sijaelewa hapo! Si kama hapa unavyoita wengine Mkuu au?
Maboss wanaojielewa alafu wapo sophisticated (degree ya kwanza na ya pili kasona Ulaya/Marekani), hawapendi kabisa kuitwa boss. Yeye kwake ukimuita boss/mkuu/chief/kiongozi, hawanaga noma hata kidogo.

Sasa ukutane na limbukeni la UDSM hahahahaa utalia
 
Pole sana mdogo wangu. Ulikutana na miungu watu, wapenda kuabudiwa.
 
Hawa watoto wanavyolaumiwa utadhani walijizaa... tulaumu wazazi wao kwa malezi ya kipumbavu. Wazazi hawafuatilii watoto wao na kuwatupia majukumu housegirl na mwalimu. Isiitoshe kwa sasa watoto wanaingia shule wakiwa wadogo sana na kumaliza wadogo tofauti na vizazi vilivyopita. Nikiwa O - level kuna watu wakati wa likizo walikuwa wanapiga vibarua vya saidia fundi au kufyatua matofali ya kuchoma ili wapate ada. Mtu kama huyu lazima awe serious na kujiamini. Hawa Gen Z kwa malezi yao wanajua tu tofauti ya Blue Band na Peanut butter. Wakiingia kazini wasaidieni wawe wafanyakazi wazuri badala ya kuwalaumu na kuwafukuza.
 
Kutumia herufi mkato. Kwa mfano akitaka kuandika "sasa", anaandika xaxa!!

Huu ujinga sivumilii, natupa kule
 
Ninapenda sana kufanya kazi na vijana wadogo. I love handling them. I hate bullying.
 
Ninapenda sana kufanya kazi na vijana wadogo. I love handling them. I hate bullying.
Mungu akubariki sana. Vijana wengi kwa sasa wanaingia kwenye soko la ajira wakiwa wadogo sana. Ni kuwapa muda na kuwajenga ili wajiamini. Wakija kujua vitu wanakuwa fasta mno kuliko wakongwe. Ukiangalia hata town kuna ongezeko kubwa la Gen Z wanaokimbiza sana kwenye biashara.
 
Hao gen Alpha watamalizana na gen Z!
 
Mkuu, mimi kunyanyasa mtu (generally speaking) huwa sipendi. Ninapenda sana mdogo wangu ajisikie huru kuniuliza maswali yoyote (ya kikazi au maisha) kama hana Pesa aseme, tunaenda wote lunch, Nikiwa na Pesa Nampa na kama sina nitamwambia tu ukweli kuwa leo sina mdogo wangu.

Siwezi kumchezea mtu faulo ya makusudi ili afukuzwe kazi au field yake. HAPANA. NEVER EVER.
 
Kuna Dogo alikuja Field...Eti Site akawa anakuja na Jeans kubwaa na mayeboyebo makubwaa kichwani kanyoa kiduku
Nikamwambia Dogo peleka Ujinga huko nisikuone na mavazi hayo.
Hakurudi asee sjui alienda kupatia wapi field.
Kwa nini usiongee nae kistaarabu na kumwelewesha mavazi anayo takiwa kuvaa?
 
Mtu analazimisha shikamoo utadhani alikuazima kakataa kukurudishia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…