Mabraza mliooa, mnaweza tupatia ushauri gani sisi ambao tunataka kuoa?

Mabraza mliooa, mnaweza tupatia ushauri gani sisi ambao tunataka kuoa?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu habari.

Moja kwa Moja kwenye mada.

Mabraza mliotangulia kuoa, ni ushauri gani mfupi mnaweza kutupatia sisi ambao tunatazamia kuoa hivi karibuni?

Vitu kama umri wa kuoa, kushare mishahara na mke, kujenga nyumba na kuandika majina yenu wote, kuchanga na kununua gari, kurudi home mapema au kuchelewa n.k.

Ata ushahuri mdogo unaweza kua na msaada kwangu au kijana mwingine mwenye malengo kama yangu.

Natanguliza shukrani.

1621407316266.png

 
Usitoe.ukioa ni majanga yanaanzia hapa. Kwanza inabidi umnunue mke, Kwa bei inayoitwa mahari. Na wakati wa kununua lazima iambatane na tafrija ya Pete na Harusi,hela hizo zinakutoka. Si ungekula BATA na Wana Hadi nafsi ifurahi??
Shida zote za nini, USIOE!

Tuendelee, mnakua wawili, gharama za maisha zinaongezeka, jumlisha matabia mapya ya mkeo yanakuchanganya, ushazoea kulala kokote huezi tena, kukesha bar na kulala na pisi Kali Kama zamani.
Shida zote za nini, USIOE!

Mnakuja kupata watoto, gharama zinaongezeka mara dufu,chakula, pango, shule, msaidizi, kutunza wakwe na mashemeji...eh eh eh..wakwe ndio...si washakua wazazi wenu, na nduguze mkeo ni nduguzo?
Shida zote za nini, USIOE!

Bado unatakiwa upambane watoto uwaachie urithi mbili,ELIMU NA MALI....
Shida zote za nini, USIOE!
 
Kama level yako ya kufikiria na kupata muafaka ni kuanzisha uzi JF nashauri Oa mwanamke ambaye ana afya strong. Mtu ambaye hazipiti wiki mbili lazima aumwe au mkitembea mkirudi ana mafua au mgongo umekaza atakufanya ujute
 
Mwanamke wa kuoa.

1: Usimpende ila awe na vigezo vya kuwa mke ukitaka kuishi kwa raha mustarehe na hakikisha yeye ndio anakupenda na anauchungu na hiyo ndoa kuzidi wewe.

2: Mwanamke ni wa jumuiya hivyo hakikisha atakuwa balozi mzuri kwa wazazi wako na marafiki wako bila kusahau wanao yaani atakuwakirisha vyema. Achana na hawa matakataka wanao sema mke ni wakwako sijui usisikilize ya watu .... brother maisha Ni safari ndefu Kuna sehemu hutafika ukiwa na mke kero kwa watu, mwanamke Malaya , mwanke mwizi nk...... Nakwambia Tena mwanamke wa jumuiya ndio maana yakiwashinda ndani mnaanza kuita washenga,wazazi sijui wachungaji waje wawasuruishe Kama Ni wako kwa Nini usimsuruhishe mwenyewe, ndio maana wahenga walifupisha tu walikuambia mwanamke Ni tabia njema.

3: Mwanamke anae fiti viatu vyako

4: Awe mchakalikaji wa wastani
5:Awe anajua kwenye ndoa kafuata Nini.
6.....
7........
8......
9.....
10:......Awe mlevi kupindukia[emoji41]
 
Back
Top Bottom