Usitoe.ukioa ni majanga yanaanzia hapa. Kwanza inabidi umnunue mke, Kwa bei inayoitwa mahari. Na wakati wa kununua lazima iambatane na tafrija ya Pete na Harusi,hela hizo zinakutoka. Si ungekula BATA na Wana Hadi nafsi ifurahi??
Shida zote za nini, USIOE!
Tuendelee, mnakua wawili, gharama za maisha zinaongezeka, jumlisha matabia mapya ya mkeo yanakuchanganya, ushazoea kulala kokote huezi tena, kukesha bar na kulala na pisi Kali Kama zamani.
Shida zote za nini, USIOE!
Mnakuja kupata watoto, gharama zinaongezeka mara dufu,chakula, pango, shule, msaidizi, kutunza wakwe na mashemeji...eh eh eh..wakwe ndio...si washakua wazazi wenu, na nduguze mkeo ni nduguzo?
Shida zote za nini, USIOE!
Bado unatakiwa upambane watoto uwaachie urithi mbili,ELIMU NA MALI....
Shida zote za nini, USIOE!