INAENDELEA....!!!!!
Nimefika kwa azizi ally ikabidi niunge kule chini relini maskani kwa wanangu kutuliza akili.....nikatoa sigara pori zote nikawapa
Nikaingia pub moja hv pale barabarani afu nikaingia chooni na kutoa zile soksi nilizochomeka hela na kuanza kuangalia kilichomo....noti mpya mpya za elfu kumi na elfu tano....nikaona hapa nikihesabu nitachukua mda...nikapangapanga mabunda ya noti vizuri nikatia mfukoni nikarudi maskani...sasa hiyo ni saa kumi jioni.
Nipo pale masikani akili inawaza mbali sana....huu mpunga sio wangu ni wa mabraza hata iweje siwezi kuutumia...na hii siri nitamuambia tu braza muzungu ila braza mubanda nitamficha sababu nahisi ana hasira na braza mubanda.
Sasa tatizo pale masikani sio salama afu ikifika jioni wahuni wote wa kwa azizi ally wanakuja pale masikani relini....nikaamua nisepe mdogo mdogo nirudi zangu magetoni kawe ila sipitii masikani magomeni na kisimu changu cha buton nimekizima...enzi hizo hakuna mambo ya kusajili line.
Nilifika magetoni kawe saa mbili usiku...ile kufika wanangu watoto wa maghorofani kelele kibao za utani""BOSI KARUDI LEO KUKU TENA 🤣🤣🤣😂""" Mimi nikawajibu leo nguna tu,,huko nilikotoka kidogo nidakwe na manjagu kkoo.
Sasa pale magetoni hakuna kitanda tumetandika magodoro mawili chini tunalilia sababu ni geto la kulala tu ila kila mtu atakula kwao....PALE NI OFISI YA MIPANGO..!!
HELA SHETANI...SI NIKAMKUMBUKA DEMU WANGU WA MSIMU NANCY*
** NAPOSEMA DEMU WA MSIMU NAMAANISHA MDADA WA MJINI***
Huyo Nancy mwenyewe anakaa mitaa ya kule chini rose garden kapanga huko....akili ikawa kama?ó inanituma niende,ila akili nyingine inaniambia kaa nyumbani utulie.
Kutokana na uchovu nikajikuta nashituka saa nane ucku na hata kwa Nancy sikwenda na vihela vyangu vilipona 😂🤣🤣🤣🤣
Nakuja kushituka tena asubuhi kumekucha wana hawapo kila mmoja kakimbilia kibaruani kwake.
Ndipo kwa uhuru naanza kuhesabu zile hela nilizotoa kwa braza muzungu kwenye kiatu na soksi..Sasa nikaanza kuhesabu hela...noti nyingi nyingi za elfu kumi na elfu tano taratiibu.
Jumla nikapata sh laki saba na elfu themanini ndio nilifanikiwa kuondoka nazo chumbani kwa braza yangu muzungu kule kariakoo kwa bibi yake.
Jumla nikawa na laki saba na elfu ishirini ya kwangu niliyoiacha kwa bi mkubwa mikocheni""A""na kule magomeni nilipewa elfu tisini na braza Mubanda.....na pale kwa braza Muzungu nimepata laki saba na elfu themanini...ila hii sio yangu siwezi kutoa hata sh kumi.
Nikaamua na hizi nazipeleka home kwa bi mkubwa kuziifadhi na sitokei maskani magomeni na kariakoo mpaka msala utulie...na kama kuna lolote nitajua tu kupitia washikaji wetu wauza vitu used kkoo.
Nikawa najiuliza mimi mwenyewe...hv nina siku mbili tu na majanga kama haya ya mabraza...nikaona hii hatari na nikianza kua na mawazo mapya hasa kuhusu njia za kutafuta kipato....hizi harakati za watoto wa mjini jela ni nje nje au kufa.
Nimekaa sana mwenyewe najiuliza kuhusu kilichotokea ndani ya siku mbili hizi za hekaheka.
Hii noma sio maisha haya......ndio ni kweli nimeingiza karibia milioni kwa siku moja ila hizi deal hazifai......
Nikawa najiuliza hv ningedakwa kule kkoo ingekuaje mda huu....kama sio msimbazi kwa manjagu?
Nikawa nawaza mengi kweli ila na utamu wa pesa unanichanganya....
Mara mawazo yakarudi kwa mabraza ila nikajizuia kabisa kutokea masikani za kkoo na magomeni....!!!
Nikaondoka magetoni mdogo mdogo mpaka kwa bi mkubwa kuweka mambo yangu sawa na kutulia kidogo coz nyumbani ni nyumbani.
Mpaka mda huo sijawasiliana na watu wa karibu wa mabraza na sitaki kuwasikiana nao kwa lolote lile,maana nikiogopa kuunganishwa kwenye tela la watuhumiwa nikaharibu mipango yangu endelevu.
Ikabidi nije na mawazo mapya ambayo nilipanga kama mabraza wakimaliza salama huu msala wao basi nawapanga,tupige mitikasi ila safari hii tupige dili nyeupe hasa za kununua vitu vilivyotumika na kuviuza kwa bei ya cha juu.
Mambo ya KUWAPIGA WATU KIJERUMANI YANAWEZA KULETA MATOKEO HASI MBELE YA SAFARI...
Ila nikawa nawaza hawa mabraza zangu watoto wa downtown watanielewa kweli dogo janja.
*KUNA KITU NILIJIFUNZA MAISHANI KUA PESA HAZITOSHI NA HELA NI TAMU SANA NA UKIENDEKEZA TAMAA YA HELA UNAWEZA HATA KUUA WATU UPATE HELA AU KUVUNJA SHERIA ZA NCHI KIMAKUSUDI ILI UPATE HELA
ITAENDELEA.....!!!!!
Muendelezo soma
Mabraza wa Kariakoo na dili zao