Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

Hizi taasisi za umma ziko corrupt and inefficient tunapoelekea hata TRA itakuja kubinafsishwa maana hawana ubunifu, hawana ufanisi kazi kuomba rushwa tu na kuongeza tozo!!
Ninawaelewa sana wenye mawazo kama haya uliyowasilisha hapa, ila huwa nashindwa kabisa huwa hamuendi mbele zaidi na kutaja tatizo la haya yote hasa ni nini?

Hivi serikali zetu hizi na viongozi wao, wao hufanya kazi zao vizuri sana kiasi kwamba huko hatuwezi kuhimiza wawepo wawekezaji ili tupate ufanisi mkubwa huko pia?

Ninavyojua mimi, matatizo yote ya akina TPA, TRA na wengineo chimbuko lake ni huko huko serikalini, kama ulivyogusia mwenyewe.

Mimi nashindwa kabisa kuelewa, inakuwaje mwekezaji afanye kwa ufanisi, kwa msukumo wa kupata faida; lakini mtu wetu mwenyewe, mzalendo wa nchi hii yeye awe ni mtu wa kuharibu tu?
Kwa kweli somo hili hapa huwa silielewi kabisa.
Labda siku moja italazimu nitafute msaada wa 'brain transplant" toka kwa magwiji kama nyinyi, ili nami nipate kulielewa hili jambo vizuri zaidi.

Kwa mwendo huu mnaotupeleka sasa ni kwamba hakuna jambo hata moja tunaloweza kufanya kwa ufanisi sisi wenyewe, bila ya kuwategemea wawekezaji, na hasa hao toka nje!

Ni ajabu sana.
 
Well said kiongozi
 
Hujasikia chuo Cha polcs kgambon kinahamishwa kupisha DP,

Hili dude wamedhamiria, tuongeze nguvu, la sivyo itaenda.
Usitie shaka, acha lituondolee uchafu huu ulioganda siku nyingi, nikiwa na maana ya CCM na serikali yake.

DPWorld haitawaacha salama wakiendelea kuvimbisha vichwa.

Kama hawalioni hilo, watakuwa wamelewa madaraka vibaya sana.
 
Usitie shaka, acha lituondolee uchafu huu ulioganda siku nyingi, nikiwa na maana ya CCM na serikali yake.

DPWorld haitawaacha salama wakiendelea kuvimbisha vichwa.

Kama hawalioni hilo, watakuwa wamelewa madaraka vibaya sana.
HAPANA, 2025 mbali ,watakuwa wameuza Kila ki2,

Tuungane na Nabii Mwabukusi kupeleka mashtaka mahakama ya umma iliyo juu ya zote, mabarabarani na Viwanjani Ili waovu watokomee!!
 
JPM hakufanikiwa lolote huko bandari, ufisadi haukuwahi kuisha TPA na ufanisi Bado ulikua chini sana.

Sijui why mnamuona JPM alikua perfect, hivi si ndio NIDA alitumbua weee mbona bado vitambulisho havitoki?

Wote Yale Yale tu
Nidhamu ilikuwepo mkuu.

Siku magufuli anatangazwa Kuwa amefariki watu walihamishia matrioni majumbani mwao .
Alipoingia Samia akakuta hazina ni nyeupe wakamdamganya Kuwa JPM hakufanya Kitu.
Yule MTU aliifanya kazi kubwa sana .

Nilitofautiana Naye aliposhindwa kuzuga Hata kumpa pole Tundu Lisu. Na kuvuruga uchaguzi na kuibeba CCM . Kuibeba CCM Ilikua ni Kama kumlaza mtoto mchanga kwenye Chumba chenye Siafu.

Lakini mambo Mengi JPM alikua Yuko Sahihi sana.
Nchi hii haihitaji mjomba kuja kuendeleza zaidi ya kupata Rais mwenye ujasiri na roho ngumu ya kuiua CCM na kuwaacha Wezi wapambane na Hali zao.

Bandari na miundombinu mingi Ilikua inawekwa Vizuri Ili uanze kukusanya pesa Kwa Kasi.

Hivi umewahi kujiuliza pesa zinazokusanywa kwenye mizani Kila MAHALI, masoko, Stendi Kila Halmashauri, vituo vya mafuta, Nyumba Asilimia kubwa katikati ya miji ni za NHC. Pesa karibu asilimia 60 mpaka 70 zinaishia mifukoni Kwa watu . Hivi Soko kama la kariakoo linapataje hasara. Stendi Kama ya Mbezi inapataje hasara? Shirika la Nyumba linapataje hasara, bandari inapataje hasara?
Watu wanajiunganishia bomba la mafuta kuelekea majumbani mwao halafu wanabembelezwa Badala ya kuzsmishwa kwenye kisima cha mafuta na kutiwa kiberiti.

Watanzania watapataje ajira Kwa Mwarabu wakati wametangaziwa Kwa Wazi Kuwa sio waaminifu ,ni Wezi na wasiojituma!! ?
Watu Kama Hao Kwa nini wasinyooshwe kwanza Kwa miaka 20 Ili wabadikike kwanza ndipo waendane na Kasi ya utendaji Wa Dunia unaohitaji watu waadilifu. CCM mpaka Karne hii Bado Wanaweka watu Wa kuchota pesa za kampeni kwenye mashirika ya umma na Kisha Kurudi madarakani kuiba Tena.
Mfano tu Yule Aliyeiba pesa za Benki ya Walimu alipata uteuzi Badala ya kufungwa halafu utegemee banki ile iweze kuwanufaisha walimu?

Pesa za Tasaff ni wizi mtupu lakini ndio bajeti yake inaongezwa baadala ya kunyoosha kwanza wezi na kuwafunga gerezani Ili anayeingia upya awe muoga na Kuwa mwadilifu .
Tabia zinatengwa na jamii kulingana na mazingira . Wizi ukizidi Lazima pawe na hatua Kali na SIO kubembelezana Kama Yule Mkurugenzi Wa maje alivochukizwa na Mafisadi wanaoletea vimemo mezani halafu waziri anawalamba Miguu . Ingekua Mimi ningempiga Chini waziri nimpe yule Dada kazi mana anaonekana kukerwa na Uovu unaorudisha Nyuma maendeleo ya watu.
 
We Msanii acha Usanii. Bajeti ya bandari inakataje?

Huyo jamaa yako anakumbuka jinsi ya kupata tija leo, muda wote alikuwa wapi?

October mbona mbali, DP world atakuja tu.
 
Acha kuzua taharuki. Huyo mfanyakazi naye ana mrija wake bandarini. Bandari inaingiza hela nyingi ila zinaishia kwenye mifuko ya wachache. Vijana wadogo wanaofanya kazi TPA wana utajiri wa kufuru. JPM alikamata kamata ila hakuweza kufaulu. Mama kuleta DPW itakuwa komesha ya wezi wote ndo maana tunasikia vilio kila kona.
 
Yote hayo yanasababishwa na haohao viongozi.
 
Kwa nn tusitafute kampuni ya kitaalamu kama deloitte ya management tuu na sio kuleta watu wenye migogoro na bandar djibout.sudan etc
 
DPp world Si wawekezaji ni wakoloni, wanatulazimisha tubadili KATIBA Ili wamiliki ardhi bila UKOMO.

Hii kitu tutapambana Hadi mwisho.
 
DPW inayokuja ina share za wezi na mafisadi wa CCM wa zile royal families.

Kuona Ticts ilipewa ukomo wao wameona watoe kabisa masharti ya ukomo ili wajimilikishe bandari milele. Kwa maana hio watoto wao watakula pesa, wajukuu watakula pesa, vitukuu vyao vitazikuta shares vitaendelea kula maisha huku watanzania wengine wakitopea kwenye lindi la umasikini kwa kukosa huduma bora za kijamii milele.

Lazma tuipinge hii DP World kwa nguvu zote hata ikibidi kuifurusha CCM madarakani kwa vurugu. Tunahitaji serikali makini inayojali na kuboresha maslahi ya wananchi na sio wezi na mafisadi wanaojali matumbo yao na kujilimbikizia mali za umma.
 
Bodi ya bandari iundwe na Majenerali Wa Jeshi la Wananchi Badala ya makada Wa CCM waliotumikia wizi Kwa miaka mingi na wanaendelea kuwaza pesa za Rushwa zipatikane wapate Mgao .
Mkuu '1000digits', kwa mara nyingine tena (kuna mara kadhaa huko nyuma nilishafanya hivyo) nimekusoma kwa makini sana andiko lako lote refu.
Hakuna sehemu ninayotofautiana nawe kimtazamo kuhusu nchi yetu hii; ila labda hapo kwenye vyama hivi vya upinzani tulivyonAVYO SASA.(hususani CHADEMA).

Msimamo wangu juu ya hili ni kwamba, ni mara mia bora kabisa kuwaondoa CCM madarakkani na kuwa pa hawa pamoja na mambo yao mengi yasiyojulikana.
Tuwape, angalau kwa miaka mitano.
Kazi yao kuu kwa sasa kwetu ni huko tu kuwaondoa CCM madarakani, mengine yatafuata huko baadae.

Ningependa sana kuchambua andiko lako hatua kwa hatua, sitafanya hivyo kwa sasa kutochosha wasomaji.

Ila nimalizie tu kwa haya machache: Wachina, kama tunavyowajua sasa kwa kuishi nao miaka hii ya karibuni, ni watu wezi/wadokozi sana. Ukifumba macho tu, unaliwa.

Sasa enda kule kwao chini ya serikali yao ya kikomunisti uulizie wizi huko ndani ya mashirika na serikalini ukoje.

Hapa kwetu tunao watu waoga sana, ndiyo maana CCM imetufikisha hapa.
Tunachotaka hapa ni 'regime' isiyocheka na mpumbavu yeyote anayekwapua mali za wananchi. Sina shaka hata kidogo hapa kwetu wizi utakoma haraka sana.
Magufuli alijaribu, lakini alijaribu kwa njia mbovu, hakuwa 'systematic', huku wakti mwingine akionekana kama yeye mwenyewe ni mshiriki katika hujuma za jitihada zake.
 
HAPANA, 2025 mbali ,watakuwa wameuza Kila ki2,

Tuungane na Nabii Mwabukusi kupeleka mashtaka mahakama ya umma iliyo juu ya zote, mabarabarani na Viwanjani Ili waovu watokomee!!
Shida kubwa kwa Tanzania ni kuwapata hao wa kwenda barabarani.

Isingekuwa hivyo, nami ningesema tuanze kesho.

Lakini kwa 2024/2025, nasema kama CCM itabaki kuendelea madarakani kwa njia yoyote ile, huo utakuwa ni muujiza wa kipekee sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…