Na tunachozozana ni Mkataba wa Mahusiano ya kinchi sio Mkataba wenye Biasharaa yenyewe kwamba huyu mtu ataweka kiasi gani na maslahi yetu yatakuaje, kwa muda mfupi lilipoanza hili jambo nilichukua time kujifunza why DPW, nilichogundua Approach ya DPW kibiashara iko far ahead kuliko sisi, Sisi bandari yetu tunasubiri wateja wenye mzigo ndo waje watumie, kitu kinachotuoka ni eneo letu kijiografia. DP yeye ana wa approach wenye mizigo na watu wenye masoko ili kuwaunganisha, mnunuzi hana haja ya kuhangaika na mzigo wake akishanunua tu DP wataufikisha hadi nyumbani kwake, Wana zaidi ya meli 400 za mizigo zinazunguka bandari tofauti so DP anao mzigo tayari ambao ni muhimu sana kwaajili ya biashara ya port. Mimi kwa kweli huu mjadala nilitamani sana wataalamu waliobobea uwekezaji, uchumi, biashara ya usafirishaji wa majini, wataalamu wa sheria za Biashara za Kimataifa ndo wawe wazungumzaji na wachangiaji ili taifa linufaike