Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dakika za jioni dhidi ya JKT Tanzania

Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dakika za jioni dhidi ya JKT Tanzania

Kocha aache ujinga kwani lazima Mutale acheze.
Pia anafanya sub bila kuangalia wapi panavuja.
Mavambo na Awesu waache kucheza na jukwaa na kukaa na mpira muda mrefu.
Chemalone apewe kipindi bado anarudia makosa yake.
Hamza naye aongeze umakini.
Kocha ashukuru tumeshinda Ila lawama zote zingekuea kwake.
Simlaumu sana kocha
Kuna namna anakujakuja
 
Hatuchezi kombe.

Tunacheza michuano ya ligi ya shirikisho barani Afrika.

Huku tumeshuka kuirudisha heshima ambayo mwanzo ilipotea baada ya vinabo wachache kuchafua hadhi ya mashindano.
Lipo jukwaa maalum la kujadili michuano ya shirikisho/ kombe la kina mama.
Nenda kalitafute.
 
Isingeshinda kwa ku struggle kiasi hiki
Mi nahisi wachezaji nao walikuwa wamechoka Jumamosi walikuwa Bukoba wakicheza na Kagera Sugar wasafiri kutoka Bukoba hadi Dar kwaajili ya mechi itakayochezeka Jumanne ambayo ni leo.Ina maana walikuwa na siku tatu za safari,mapumziko na mazoezi kwaajili ya mechi dhidi ya Jkt ambao hawakuwa na safari yoyote au mechi yeyote hivi karibuni.
 
Kwani lazima amuingize Mutale, Chasambi ameanza kuchezeshwa baada ya kelele za mashabiki.
Labda unisaidie ni mechi gani Mutale amesaidia baada ya kuingizwa sub.
sikatai Mutale kapotea na anazidi kupotea
Kocha anafanya vile kurudisha confidence yake, mechi iliyohitaji matokeo kama hii ingetosha kabisa kumrudisha mutale mchezoni

Ninachokataa ni mashabiki kusema mutale hana kiwango, mutale wa mechi za mwanzo alikua ni mchezaji pekee anaepress kuanzia eneo la timu pinzani, alikua analeta kashkash mpaka wanajichanganya, hudhuria mazoezi bunju utanielewa kuhusu mutale.
 
Hivi hii mechi iliishaje?
1000211276.jpg

Hesabia mwiko nyuma wenzako hao utajua ilishaje
 
sikatai Mutale kapotea na anazidi kupotea
Kocha anafanya vile kurudisha confidence yake, mechi iliyohitaji matokeo kama hii ingetosha kabisa kumrudisha mutale mchezoni

Ninachokataa ni mashabiki kusema mutale hana kiwango, mutale wa mechi za mwanzo alikua ni mchezaji pekee anaepress kuanzia eneo la timu pinzani, alikua analeta kashkash mpaka wanajichanganya, hudhuria mazoezi bunju utanielewa kuhusu mutale.
Ukweli ni kwamba Mutale hajawahi kuwa na game nzuri toka amekuja Simba. Rudi kaangalie hiyo Simba Day na sijui mechi gani nyingine mnazosema, utakuta Mutale wa mechi hizo ndiyo tunayemuona sasa.

Nimejiridhisha kuwa siyo ishu ya confidence inayomkabili. Ukweli ni kuwa siyo mchezaji mzuri maana hana misingi ya mpira. Hafikiri kabla ya kutenda jambo uwanjani na ana uwezo mdogo sana wa kuanticipate movement za wachezaji wenzake na wapinzani.
 
Simba mtumieni match analysit...ili kujua uwezo wa FADLU...
2nd half anashindaga kwa tabu...ni kama anashindwa kung'amua madhaifu ya mpinzani ili kuja na PLAN B
 
Back
Top Bottom