Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dakika za jioni dhidi ya JKT Tanzania

Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dakika za jioni dhidi ya JKT Tanzania

sikatai Mutale kapotea na anazidi kupotea
Kocha anafanya vile kurudisha confidence yake, mechi iliyohitaji matokeo kama hii ingetosha kabisa kumrudisha mutale mchezoni

Ninachokataa ni mashabiki kusema mutale hana kiwango, mutale wa mechi za mwanzo alikua ni mchezaji pekee anaepress kuanzia eneo la timu pinzani, alikua analeta kashkash mpaka wanajichanganya, hudhuria mazoezi bunju utanielewa kuhusu mutale.
Amempa nafasi Mara nyingi Sana, Karabaka Yuko wapi, Manura mbona hapewi nafasi, Kama timu imeshinda ni muhimu apewe nafasi na sio kucheza kamari
 
Kwa Mutale imetosha sasa. Inaonekana aliyemleta Mutale pale Simba ni kigogo mkubwa sana. Haiwezekeni mechi kama ya leo timu inahitaji pointi tatu kwa machozi, jasho na damu halafu benchi la ufundi linafanya upuuzi wa kumuingiza Mutale ambaye toka amefika mechi aliyocheza vizuri ni ile ya Simba day tu. Vinginevyo viongozi waseme tu labda Mutale ana mkataba kama aliokuwa na Saidoo wa kucheza kila mechi.

Tuzungumuze ukweli ulio wazi Karabaka ni bora mara mia kuliko Mutale na amethibitsha hilo kwenye michezo michache aliyocheza. Lakini kwa upuuzi unaofanywa na bechi la ufundi la Simba eti leo Karabaka anataka kutolewa kwa mkopo halafu Mutale kila mechi yupo lazima acheze atatafutiwa hata dakika kumi kwa lazima.

Simba ni timu kubwa inayohitaji matokeo muda wate inatakiwa ifanye mambo yake kitaalamu kwa kumtafutia Mutale mtaalam wa saikolojia wamalizane wenyewe huko kambini na mazoezini na siku akiwa sawa ndio arudishwe aanze kucheza. Hivi inavyofanyika kulazimisha acheze ili arudishe saikolojia yake ndio kwanza anazidi kuwa kituko uwanjani na inageuka aibu kwa benchi la ufundi, kamati ya usajili na viongozi wote kwa ujumla. Na sijui kwa nini Simba wanahangaika na Mutale kwa kiasi hicho wakati Mutale mwenyewe ukimtazama tu usoni ni kama amechanganyikiwa hivi na hata akiingia uwanjani akipata mpira hajui afanye nini matokeo muda wote awapo uwanjani anaikaba Simba na anasababisha wenzake wacheze pungufu japo wametimia.

Ni mtizamo tu
 
Kwa nilivyoona mimi jaribu ku reflect mechi na Mashujaa na hii ya JKT. Ushindi wa aina hii unakuja kuku cost siku timu unayocheza nayo ikaamua kukaza na kuepuka kufanya makosa ya kijinga kama yale. Kama ubingwa unahitajika ipo haja hizi timu ziingie sokoni kusaka wafumania nyavu haswa kuliko kubaki na hawa wachezaji wapate nafasi 7 wafunge 1.

Angalia miaka mingine timu zinazobeba ubingwa wafumania nyavu wao au wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha matokeo. John Bocco, Kagere, Mayele, Aziz Ki, Msuva n.k ni nadra sana kupata ubingwa bila kuwa na main man anayeweza kukunyanyua mechi inapokua imekuelemea kama hii dhidi ya Mashujaa au JKT
 
Mi
Kwa Mutale imetosha sasa. Inaonekana aliyemleta Mutale pale Simba ni kigogo mkubwa sana. Haiwezekeni mechi kama ya leo timu inahitaji pointi tatu kwa machozi, jasho na damu halafu benchi la ufundi linafanya upuuzi wa kumuingiza Mutale ambaye toka amefika mechi aliyocheza vizuri ni ile ya Simba day tu. Vinginevyo viongozi waseme tu labda Mutale ana mkataba kama aliokuwa na Saidoo wa kucheza kila mechi.

Tuzungumuze ukweli ulio wazi Karabaka ni bora mara mia kuliko Mutale na amethibitsha hilo kwenye michezo michache aliyocheza. Lakini kwa upuuzi unaofanywa na bechi la ufundi la Simba eti leo Karabaka anataka kutolewa kwa mkopo halafu Mutale kila mechi yupo lazima acheze atatafutiwa hata dakika kumi kwa lazima.

Simba ni timu kubwa inayohitaji matokeo muda wate inatakiwa ifanye mambo yake kitaalamu kwa kumtafutia Mutale mtaalam wa saikolojia wamalizane wenyewe huko kambini na mazoezini na siku akiwa sawa ndio arudishwe aanze kucheza. Hivi inavyofanyika kulazimisha acheze ili arudishe saikolojia yake ndio kwanza anazidi kuwa kituko uwanjani na inageuka aibu kwa benchi la ufundi, kamati ya usajili na viongozi wote kwa ujumla. Na sijui kwa nini Simba wanahangaika na Mutale kwa kiasi hicho wakati Mutale mwenyewe ukimtazama tu usoni ni kama amechanganyikiwa hivi na hata akiingia uwanjani akipata mpira hajui afanye nini matokeo muda wote awapo uwanjani anaikaba Simba na anasababisha wenzake wacheze pungufu japo wametimia.

Ni mtizamo tu
Mi mwenyewe nashangaa wanaosema eti mutale ni mzuri apewe muda mnataka apewe muda Mara ngapi mtu kacheza mechi karibu 10 performance yake ile ile ambayo inagharimu timu basi tuleteeni takwimu zake huko Zambia hawana

Yani winga kwa saivi kwamba anatakiwa kusifiwa kukimbia kimbia uwanjani na kuwasumbua mabeki sijui wengine wanaonaje mpira yani huyu mutale hajafikia hata kiwango alichorudi nacho miquessone kutoka Egypt

Wakina karabaka wapo nje halafu anapewa muda mtu ambaye anavurunda kila mechi na hapo unapambania ubingwa na yanga na umemwacha kwa point kiduchu mno simba saivi inahitaji wachezaji walio tayari na sio mtu anafika aanze kupewa muda yani mpaka dirisha dogo aendelee kupewa muda ili iweje na bora hata angekua anakaa benchi labda tungesema benchi linamuathiri karibu kila mechi anapangwa ila anayofanya ni kituko
 
Jifunze kuanzisha topic fikilivu na ngumu si kila siku eti,"machache yalioonekana mechi kati ya simba na......" wewe si mchambuzi bali ni shabiki wa makolo,mechi ya juzi ya yanga mbona haukuleta uzi kuzungumzia machache?
 
Back
Top Bottom