Machache yaliyoonekana Simba ikiibuka na ushindi dakika za jioni dhidi ya JKT Tanzania

Hatuwezi bishana sijui mnacheza kombe gani huko kimataifa mpo kundi gani ili tubishane!
Hatuchezi kombe.

Tunacheza michuano ya ligi ya shirikisho barani Afrika.

Huku tumeshuka kuirudisha heshima ambayo mwanzo ilipotea baada ya vinabo wachache kuchafua hadhi ya mashindano.
 
Simlaumu sana kocha
Kuna namna anakujakuja
 
Hatuchezi kombe.

Tunacheza michuano ya ligi ya shirikisho barani Afrika.

Huku tumeshuka kuirudisha heshima ambayo mwanzo ilipotea baada ya vinabo wachache kuchafua hadhi ya mashindano.
Lipo jukwaa maalum la kujadili michuano ya shirikisho/ kombe la kina mama.
Nenda kalitafute.
 
Isingeshinda kwa ku struggle kiasi hiki
Mi nahisi wachezaji nao walikuwa wamechoka Jumamosi walikuwa Bukoba wakicheza na Kagera Sugar wasafiri kutoka Bukoba hadi Dar kwaajili ya mechi itakayochezeka Jumanne ambayo ni leo.Ina maana walikuwa na siku tatu za safari,mapumziko na mazoezi kwaajili ya mechi dhidi ya Jkt ambao hawakuwa na safari yoyote au mechi yeyote hivi karibuni.
 
Kwani lazima amuingize Mutale, Chasambi ameanza kuchezeshwa baada ya kelele za mashabiki.
Labda unisaidie ni mechi gani Mutale amesaidia baada ya kuingizwa sub.
sikatai Mutale kapotea na anazidi kupotea
Kocha anafanya vile kurudisha confidence yake, mechi iliyohitaji matokeo kama hii ingetosha kabisa kumrudisha mutale mchezoni

Ninachokataa ni mashabiki kusema mutale hana kiwango, mutale wa mechi za mwanzo alikua ni mchezaji pekee anaepress kuanzia eneo la timu pinzani, alikua analeta kashkash mpaka wanajichanganya, hudhuria mazoezi bunju utanielewa kuhusu mutale.
 
Ukweli ni kwamba Mutale hajawahi kuwa na game nzuri toka amekuja Simba. Rudi kaangalie hiyo Simba Day na sijui mechi gani nyingine mnazosema, utakuta Mutale wa mechi hizo ndiyo tunayemuona sasa.

Nimejiridhisha kuwa siyo ishu ya confidence inayomkabili. Ukweli ni kuwa siyo mchezaji mzuri maana hana misingi ya mpira. Hafikiri kabla ya kutenda jambo uwanjani na ana uwezo mdogo sana wa kuanticipate movement za wachezaji wenzake na wapinzani.
 
Simba mtumieni match analysit...ili kujua uwezo wa FADLU...
2nd half anashindaga kwa tabu...ni kama anashindwa kung'amua madhaifu ya mpinzani ili kuja na PLAN B
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…