Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
1. Ukitaka chimbo la bidhaa zote acha usingizi, nenda Kariakoo muda kama huu saa 8 za usiku

2. Machimbo ya bei nafuu sio Siri, yapo wazi usiku tu kuanzia saa 7,8,9 ndo utayaona

3. Usije Kariakoo saa 5 asubuhi 😂 eti oooh naulizia chimbo la vifaa vya simu, chimbo la abaya, Chimbo la Raba hutapata ng'ooo

4.Machimbo hayana connection wala sijui groups za Whatsapp, we jitoe nenda Kariakoo usiku matajiri wanashusha mizigo unabeba Kwa bei cheee

5. Hizo Abaya mnazouziwa bei ya jumla 35,000 ili mkauze 60,000 hapa usiku huu watu wanazoa Kwa 13,000

6. Sandles mnazonunua 3500 jumla hapa zinauzwa 1200

7. Kipindi usiku umelala unazagamua ili kesho uamkie Kariakoo kuchukua mzigo ujue wenzako wamelala nao wa bei ya chimbo

8 Narudia tena mchana hutaona Chimbo lolote

9. Nimegundua wafanyabiasha wakubwa hawalali, wale watu wanao deal na fashion tuko nao hapa wanapambania mzigo kama watoto wa shule wanavopigania wali


10. Usiku ndo muda wa kusaka utajiri.

Muwe na usiku mwema wana jf
 
Usiku una siri gani?
1. Ukitaka mafanikio makubwa (plan au ndoto halisi hufanyika usiku).
2. Watoto wengi huzaliwa usiku, nadhan hata mwamzisha uzi huu ulizaliwa usiku.
3. Vifo vingi pia hutokea usiku.
4. Usiku unabeba nini lakini?

Kwa hoja hizo naweza kukubalia yamkin uzi wako una ukweli
 
Miaka yote hii unataka kusema watu hawaijui hii plan?

Ukipita Kariakoo mida hii 9 alfajiri naamini utaona maduka mengi yamefungwa, sasa hayo machimbo yapo underground au?

Usije kufanya watu waende Kariakoo mida mibaya waishie kukabwa na kuibiwa pesa zao, warudi nyumbani na damu badala ya hizo Abaya za bei rahisi.
 
Miaka yote hii unataka kusema watu hawaijui hii plan?

Ukipita Kariakoo mida hii 9 alfajiri naamini utaona maduka mengi yamefungwa, sasa hayo machimbo yapo underground au?

Usije kufanya watu waende Kariakoo mida mibaya waishie kukabwa na kuibiwa pesa zao warudi nyumbani na damu badala ya hizo Abaya za bei rahisi.
Huijui vizuri kariakoo, hayo machimbo yapo tangu mwaka 2007 nilipoyasikia na kuyaona. Tatizo wengi wetu tunadhani kariakoo ni mtaa wa kongo na msimbazi tu.
Pia "Kariakoo kuna zaidi ya biashara"
 
Hii mida 9 alfajiri kuambia watoto wa kike wakimbilie Kariakoo kuafuta Abaya za bei rahisi unataka wabakwe tu.
Wengi wenye maduka sio watoto wa kike jamaa anachosema yupo sahihi Kariakoo usiku ndio wanapokea mzigo na kuuuza muda huo huo inategemeana na duka lililopata mzigo kama hana mzigo siku hiyo afungui ila vijana wa kazi wanajua waliopokea mzigo mchana..
Ukipata taarifa kama hauna uhakika na hauwezi kufanya usibishe wapo wanaofanya na wakimaliza kununua mizigo yao wanachukua Lodge za hapo hapo analala Wazambia wengi na watu wa mikoani wametembea na hii pin number..
 
Kwa wale mnaoiishi maporini, hii ndio Kariaako

1780881313319.png

1780881502819.png
 
Hiyo ni ukweli mtupu usiku vitu huwa vinashuka bei, nahisi kunawauzaji wengine ndo huwa wanapata nafasi ya kufanya biashara . Au asubuhi sana yaani saa kumi na Moja asubuhi. Muhimu nikuwa makini kwenye kuchagua usijepata lonya au reject
 
1. Ukitaka chimbo la bidhaa zote acha usingizi, nenda Kariakoo muda kama huu saa 8 za usiku

2. Machimbo ya bei nafuu sio Siri, yapo wazi usiku tu kuanzia saa 7,8,9 ndo utayaona

3. Usije Kariakoo saa 5 asubuhi 😂 eti oooh naulizia chimbo la vifaa vya simu, chimbo la abaya, Chimbo la Raba hutapata ng'ooo

4.Machimbo hayana connection wala sijui groups za Whatsapp, we jitoe nenda Kariakoo usiku matajiri wanashusha mizigo unabeba Kwa bei cheee

5. Hizo Abaya mnazouziwa bei ya jumla 35,000 ili mkauze 60,000 hapa usiku huu watu wanazoa Kwa 13,000

6. Sandles mnazonunua 3500 jumla hapa zinauzwa 1200

7. Kipindi usiku umelala unazagamua ili kesho uamkie Kariakoo kuchukua mzigo ujue wenzako wamelala nao wa bei ya chimbo

8 Narudia tena mchana hutaona Chimbo lolote

9. Nimegundua wafanyabiasha wakubwa hawalali, wale watu wanao deal na fashion tuko nao hapa wanapambania mzigo kama watoto wa shule wanavopigania wali


10. Usiku ndo muda wa kusaka utajiri.

Muwe na usiku mwema wana jf
Duh sasa sisi wa Mkoani tunafanyeje
 
Back
Top Bottom