Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

Mkuu natmani sana kwenda hiyo alfajiri. Ila nikiwaza mambo ya roho mkononi pesa mfukoni nasita kidogo.
Nitaend karibuni.
Wanaserma "Get rich or die trying".
Nipo Johannesburg kuchukua magari lakini habari za mtandaoni huku wanafukuza wageni kilichopo hapa sio kinachoongelewa labda tarehe za mbele bila risk haupati pesa bwashee.
 
1. Ukitaka chimbo la bidhaa zote acha usingizi, nenda Kariakoo muda kama huu saa 8 za usiku

2. Machimbo ya bei nafuu sio Siri, yapo wazi usiku tu kuanzia saa 7,8,9 ndo utayaona

3. Usije Kariakoo saa 5 asubuhi 😂 eti oooh naulizia chimbo la vifaa vya simu, chimbo la abaya, Chimbo la Raba hutapata ng'ooo

4.Machimbo hayana connection wala sijui groups za Whatsapp, we jitoe nenda Kariakoo usiku matajiri wanashusha mizigo unabeba Kwa bei cheee

5. Hizo Abaya mnazouziwa bei ya jumla 35,000 ili mkauze 60,000 hapa usiku huu watu wanazoa Kwa 13,000

6. Sandles mnazonunua 3500 jumla hapa zinauzwa 1200

7. Kipindi usiku umelala unazagamua ili kesho uamkie Kariakoo kuchukua mzigo ujue wenzako wamelala nao wa bei ya chimbo

8 Narudia tena mchana hutaona Chimbo lolote

9. Nimegundua wafanyabiasha wakubwa hawalali, wale watu wanao deal na fashion tuko nao hapa wanapambania mzigo kama watoto wa shule wanavopigania wali


10. Usiku ndo muda wa kusaka utajiri.

Muwe na usiku mwema wana jf
Chai
 
Wengi wenye maduka sio watoto wa kike jamaa anachosema yupo sahihi Kariakoo usiku ndio wanapokea mzigo na kuuuza muda huo huo inategemeana na duka lililopata mzigo kama hana mzigo siku hiyo afungui ila vijana wa kazi wanajua waliopokea mzigo mchana..
Ukipata taarifa kama hauna uhakika na hauwezi kufanya usibishe wapo wanaofanya na wakimaliza kununua mizigo yao wanachukua Lodge za hapo hapo analala Wazambia wengi na watu wa mikoani wametembea na hii pin number..
Uliwahi kupata Mali usiku? Una uzoefu kariakoo?
 
Simu za bei chee eti zinauzwa usiku 😹😹
Watu wanachekesha hapa.
Bidhaa yoyote wakiambiwa chimbo wao wanajua unaipata moja hawajui hiyo chee inauzwa kwa dozen..!!
Hii concept inawachanganya watu sana wanaoanza biashara. The more you become in, the more you see how complex it is.. kuna makosa mengi ya kiufundi yamebebwa kwenye dhana ya machimbo
 
Simu za bei chee eti zinauzwa usiku 😹😹
Watu wanachekesha hapa.
Bidhaa yoyote wakiambiwa chimbo wao wanajua unaipata moja hawajui hiyo chee inauzwa kwa dozen..!!
Kuna namna unaangalia watu wanaandika nini unashindwa hata namna ya kumuelekeza, anyway ngoja tuone masoko ya usiku😂
 
Usiku una siri gani?
1. Ukitaka mafanikio makubwa (plan au ndoto halisi hufanyika usiku).
2. Watoto wengi huzaliwa usiku, nadhan hata mwamzisha uzi huu ulizaliwa usiku.
3. Vifo vingi pia hutokea usiku.
4. Usiku unabeba nini lakini?

Kwa hoja hizo naweza kukubalia yamkin uzi wako una ukweli
Mkuu Mshana Jr hoja hii kama nimeielewa naomba ufafanuzi kama ndgu yetu alicomment
 
Back
Top Bottom