Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

Wengi wenye maduka sio watoto wa kike jamaa anachosema yupo sahihi Kariakoo usiku ndio wanapokea mzigo na kuuuza muda huo huo inategemeana na duka lililopata mzigo kama hana mzigo siku hiyo afungui ila vijana wa kazi wanajua waliopokea mzigo mchana..
Ukipata taarifa kama hauna uhakika na hauwezi kufanya usibishe wapo wanaofanya na wakimaliza kununua mizigo yao wanachukua Lodge za hapo hapo analala Wazambia wengi na watu wa mikoani wametembea na hii pin number..
Hata mwanaume huo usiku usalama upoje? Miaka ya 2001-2002 kuna kijana wa kidato cha 5 alishuka na begi lake saa 5-7 akakabwa maeneo hayo ya Kariakoo tena siyo uchochoroni.
 
Hiyo ni ukweli mtupu usiku vitu huwa vinashuka bei, nahisi kunawauzaji wengine ndo huwa wanapata nafasi ya kufanya biashara . Au asubuhi sana yaani saa kumi na Moja asubuhi. Muhimu nikuwa makini kwenye kuchagua usijepata lonya au reject
Chimbo limedifainiwa vip hapo? Mana ni ngum kupata bidhaa kwa bei nafuu kama sio kwenye dazen au carton. Hata ukienda sa 4 jua kali
 
Hata mwanaume huo usiku usalama upoje? Miaka ya 2001-2002 kuna kijana wa kidato cha 5 alishuka na begi lake saa 5-7 akakabwa maeneo hayo ya Kariakoo tena siyo uchochoroni.
Mkuu usalama kariakoo unazungumzia leo yupo IGP mmoja aliibiwa simu hapo na akasema kama mimi wahuni wamekimbia na simu je ninyi wao wametangaza biashara kama unaona ina risk kubwa endelea kulala tu mazee wala haujalazimishwa kwenda.
 
1. Ukitaka chimbo la bidhaa zote acha usingizi, nenda Kariakoo muda kama huu saa 8 za usiku

2. Machimbo ya bei nafuu sio Siri, yapo wazi usiku tu kuanzia saa 7,8,9 ndo utayaona

3. Usije Kariakoo saa 5 asubuhi šŸ˜‚ eti oooh naulizia chimbo la vifaa vya simu, chimbo la abaya, Chimbo la Raba hutapata ng'ooo

4.Machimbo hayana connection wala sijui groups za Whatsapp, we jitoe nenda Kariakoo usiku matajiri wanashusha mizigo unabeba Kwa bei cheee

5. Hizo Abaya mnazouziwa bei ya jumla 35,000 ili mkauze 60,000 hapa usiku huu watu wanazoa Kwa 13,000

6. Sandles mnazonunua 3500 jumla hapa zinauzwa 1200

7. Kipindi usiku umelala unazagamua ili kesho uamkie Kariakoo kuchukua mzigo ujue wenzako wamelala nao wa bei ya chimbo

8 Narudia tena mchana hutaona Chimbo lolote

9. Nimegundua wafanyabiasha wakubwa hawalali, wale watu wanao deal na fashion tuko nao hapa wanapambania mzigo kama watoto wa shule wanavopigania wali


10. Usiku ndo muda wa kusaka utajiri.

Muwe na usiku mwema wana jf
Utakuwa mkabaji wa usiku wewe.
 
Mkuu usalama kariakoo unazungumzia leo yupo IGP mmoja aliibiwa simu hapo na akasema kama mimi wahuni wamekimbia na simu je ninyi wao wametangaza biashara kama unaona ina risk kubwa endelea kulala tu mazee wala haujalazimishwa kwenda.
Mkuu natmani sana kwenda hiyo alfajiri. Ila nikiwaza mambo ya roho mkononi pesa mfukoni nasita kidogo.
Nitaend karibuni.
Wanaserma "Get rich or die trying".
 
Back
Top Bottom