Machimbo ya Kariakoo yapo usiku wa manane tu, mchana hutayaona utadalaliwa tu

Halafu uzuri mimi Wala sina shida na hayo machimbo maana sio mishe zangu, ila najua kuna watu wanahitaji lakini ndo hivyo changamoto ni nyingi
 
Kuna ukweli? Nataka niende nikja dar next month
 
Huijui vizuri kariakoo, hayo machimbo yapo tangu mwaka 2007 nilipoyasikia na kuyaona. Tatizo wengi wetu tunadhani kariakoo ni mtaa wa kongo na msimbazi tu.
Pia "Kariakoo kuna zaidi ya biashara"
Bado hujatajirika tu?
 
Nataka nijitoe siku moja niingie muda huo nione
 
hata uhai huanzia gizani..mbegu inachipua gizani ndani ya udongo, mtoto anaanza kupata uhai gizani ndani ya tumbo.

Maombi yanayokubaliwa kwa haraka na Mungu ni yale ya usiku wa manane wakati watu wengi wamelala.

Adhabu nyingi za Mungu hushuka nyakati za giza nene karibu na Alfajir.

Kabla ya kuwepo kwa Nuru kulikuwa na GIZA.
 
Mwez wa nane hapo mwishon nilikua dar kufatilia chimbo la sandal wanazouza mawinga 3,500.

Ili namim nije niuze 3,500 mkoani..

Asee nilizunguka wee..
Nikaulza wa bidhaa tofaut na sandal kwan wauza sandal hawasemi wanapochukuliaga mzgo.

Nikaambiwa kuna wachina wanauza hzo sandal ila kwa box na linakua na aina moja na rangi moja.

Hyo ilikua j.pili hawafunguagi niliambiwa.

Ila nilipotezea tu mwishowe, nikarud na mawasiliano ya wauzaj wa jumla.

Na kilicho nifanya niende dar ni wale wanaojitangaza mitandaon wanaagza sandal kwa tsh 800 kutoka china.

Nikajiambia wacha nikafke ofis zao kwanza, kama ni wakweli.

Wale jamaa nilipo waambia nipo MIKOCHENI maeneo wanaposema ofisi zao zinapatikana hawakupokea sim zangu.

hadi watatu, wote vilevile nikagundua ni matapeli wanasubiri watu watume pesa kwa lipa namba, wawalize.
 
Wale waagizaji ni wezi kwani unashindwa kuagiza mwenyewe made in china mbona rahisi
 
Karikaoo mizigo hushushwa usiku na kupelekwa godauni kwaiyo iki ujue chimbo lazima ujue location za magodauni kama unavyooina ilala chimbo la mitumba ni asubuh na mapema unapata mali nzurii ukija fika saa kumi na moja kila mtu keshakusanya mali zake
 
Ni kweli miaka ya nyuma nilishusha container usiku wa manane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…