Machinga; Je tunatatua Tatizo ambalo Halipo?

Machinga; Je tunatatua Tatizo ambalo Halipo?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Niliona Morogoro wanazindua vibanda vya Machinga...

WhatsApp%2BImage%2B2021-09-21%2Bat%2B6.03.41%2BPM%2B%25282%2529.jpeg

Hio ni vema na Haki... ila swali la kujiuliza tuna tatizo la mabanda au sehemu za kufanyia biashara ? Machinga Complex ilijaa au tulikosea wapi ?

Unaweza kusema ingawa frame / maduka yapo ila ni gharama Je Machinga wanashindwa kujichanga hata watano wakachangia frame (after all wamezoea kufanya kazi karibu karibu) si ni bora wakae kwenye nyumba kuliko mabanda ya mbao ?

Kuna wanaosema watafutiwe maeneo.., Je masoko yote yamejaa, Je kweli hakuna nafasi kwenye masoko au kuna masoko ambayo bado matupu..., Kila sehemu kuna mipango miji je ujenzi huu mpya unaendana na mipango miji. Na je jukumu la Serikali ambalo ni la muda mrefu ni kutafutia mabanda na kuwapanga au kuhakikisha watu wana ajira nzuri na sio kubangaiza ?, Je kila baada ya miaka mitatu mpaka mitano tutakuwa tunawapanga watu? nadhani hapa Serikali inaepuka wajibu wao wa kutengeneza Sera Mujarabu na kutumia short cut.

Kwahio naomba tujiulize, tatizo ni sehemu za kufanyia biashara ? (Sidhani sababu sehemu nyingi ni tupu): Je ni gharama ya hivi vyumba ? (nadhani hapana sababu kuna masoko yapo matupu na hawa wadau wanaweza kujichanga na kuchukua frame ambazo zipo sababu nyumba nyingi ni tupu)

Kwa hiyo huenda tatizo ni ajira za uhakika za watu kuweza kujipatia Kipato cha uhakika na kuacha Kubangaiza. Na hilo kwanini lisiwezekane kwa nchi Tajiri yenye Maliasili kama hii (Migodi, Maziwa, Bahari, Vivutio vya Watalii na Nchi Kubwa yenye Rutuba kila Kona) ?

Au tumeamua kuwa nchi ya Wachuuuzi ?
 
Hawana namna, maana ndo uwezo wa kufikiri ulipoishia hapo.....
 
Vipo wapi viwanda 400 vilivyojengwa na serikali ya ccm?
Ipo wapi serikali ya viwanda?
labda nadharia na sio uhalisia...,

Na inategemea kiwanda wanaki-define vipi sababu huenda hata fundi viatu (repair) nayeye ni kiwanda..., fundi cherehani mwenye mashine mbili nayeye ni kiwanda ila anyway so long as hivyo so called viwanda hawaviweki kwenye road reserve
 
Nchi iko kwenye uchumi wa kati halafu waziri anazindua mabanda ya mbao???
 
Nchi iko kwenye uchumi wa kati halafu waziri anazindua mabanda ya mbao???
Ukisema waziri pekee huenda mtu asikuelewe akadhani labda ni waziri wa furniture na vigoda...., tena huenda hizi mbao zikawa ni more expensive mbele ya safari.. (hatari ya moto mchwa n.k.)
 
the only solution ni kuwajengea mall yenye floor yao using the same limited space iliyopo!
Tatizo ni Nafasi ? Mbona Watu wenye Vyumba na Frame zipo Tupu ?
Au ni Gharama ? Kwani wanashindwa ku-share ?
Unaongelea Kujenga..., Si Machinga Complex ilijengwa ?

And is the space really limited hadi tuanze kwenda juu ? kwanini wasiende vertically sehemu nyingine pasipo na huduma hizo au kujaza zile spaces ambazo ni tupu (hazina wapangaji) The only thing which is limited ni wanunuzi ndio sababu kila mtu anataka apange mbele ya mwenzake ili kugombania wateja
 
Tatizo ni Nafasi ? Mbona Watu wenye Vyumba na Frame zipo Tupu ?
Au ni Gharama ? Kwani wanashindwa ku-share ?
Unaongelea Kujenga..., Si Machinga Complex ilijengwa ?
ndio Tatizo ni nafasi . pale pale penye potential ya kuuza zaidi ndipo wanapopataka,sio kweli wafanya biashara wenye maduka hawapati hela wangeshahama, machinga wanapata , wenye maduka wanapata,dawa ni kuwaweka in formal arrangement.
 
Hakuna Maduka matupu ?, Hivi umezunguka miji mingi nchini na kukuta maduka hayana watu / yamefungwa ? Kutaka na kupata ni vitu viwili tofauti..., mimi ningetaka niwe na duka Mayfair huko UK ila nina uwezo wa kupamiliki ? Wewe unataka wajengewe mall (kwa hizi tozo zetu) badala ya kujenga nyingine kwanini kwanza tusiijaze ile iliyokwisha jengwa (machinga complex) Ili tupate working modal ya mfano ?

Formal arrangement ni wao kujipanga na kujichanga na kuchukua frame kwa ku-share; wala wasingojee wapewe / wajengewe malls - kwanza kujengea kila mtu wa leo na future generation haiwezekani... In reality Serikali itaanza kuwapunguza pole pole na wale watakaobaki kila mtu atakufa kivyake..., kwahio kwanini wasijiongeze na wakodi frame na kushare..., So long as watalipa Kodi hata mwenye pango atawatafuta na kuwabembeleza na sio kuwafukuza na kuwadhihaki kama wahamiaji kumbe watu wapo katika nchi yao tena nchi tajiri ya maliasili kuliko mataifa mengi ulimwenguni...

Nadhani wale watakaobaki machinga wa kweli wa kutembeza matenga sidhani kama watafukuzwa ila nao tutategemea wata-graduate kutoka kwenye kutembeza hizo bidhaa
 
Hakuna Maduka matupu ?, Hivi umezungaka miji mingi nchini na kukuta maduka hayana watu / yamefungwa ? Kutaka na kupata ni vitu viwili tofauti..., mimi ningetaka niwe na duka Mayfair huko UK ila nina uwezo wa kupamiliki ? Wewe unataka wajengewe mall (kwa hizi tozo zetu) badala ya kujenga nyingine kwanini kwanza tusiijaze ile iliyokwisha jengwa (machinga complex) Ili tupate working modal ya mfano ?

Formal arrangement ni wao kujipanga na kujichanga na kuchukua frame kwa ku-share; wala wasingojee wapewe / wajengewe malls - kwanza kujengea kila mtu wa leo na future generation haiwezekani... In reality Serikali itaanza kuwapunguza pole pole na wale watakaobaki kila mtu atakufa kivyake..., kwahio kwanini wasijiongeze na wakodi frame na kushare..., So long as watalipa Kodi hata mwenye pango atawatafuta na kuwabembeleza na sio kuwafukuza na kuwadhihaki kama wahamiaji kumbe watu wapo katika nchi yao tena nchi tajiri ya maliasili kuliko mataifa mengi ulimwenguni...

Nadhani wale watakaobaki machinga wa kweli wa kutembeza matenga sidhani kama watafukuzwa ila nao tutategemea wata-graduate kutoka kwenye kutembeza hizo bidhaa

Machinga kuwekwa Machinga complex sio jambo la investigation stage,limeshapita huko namaanisha results tunazo tayari,kwamba wanarudi pale pale mjini, na hii ni prove the current solution/modal(kusambaza machinga kwenye maeneo mbali mbali is not working!)

Halafu sijui unakataa nini, machinga kujichanga na kuchukua frame ndio kupangwa huko, hivyo hivyo kwenye mall. Kukiwa na floor yao haimaanishi watakuwa wakikaa kiholela, NO.,ni frame zinapangwa kwenye floor na wao wanachukua hizo fremu ndani ya mall na kulipia, hiki kitu nimekiona mkuu ila sijajua wanalipaje hio rent

Swala la kodi zetu kujenga mall, kwanza ni responsibility ya serikali kuhakikisha inatengeneza mazingira mazuri na safe kwa biashara, so sioni kama ni hoja mkuu besides tukishatambua nani yuko kwenye fremu gani ni rahisi kukata kodi hata kama ni kidogo.

Formal arrangement nilikua namaanisha status sasa ya sasa hivi ni kuwa both wenye maduka na Machinga wanafanya biashara hapo hapo mjini,na WOTE wanatengeneza pesa, ni arrangement nzuri ndio inatakiwa, Machinga hawawazuii wenye maduka kutengeneza pesa,ingekua hivi ungekuta frame tupu hapo mjini,ila leo tafuta fremu kariakoo/mjini kama utapata kirahisi, mjini hapo ni kituo cha biashara kuwahamisha watu kuwe na this idea in mind.
 
Niliona Morogoro wanazindua vibanda vya Machinga...

WhatsApp%2BImage%2B2021-09-21%2Bat%2B6.03.41%2BPM%2B%25282%2529.jpeg

Hio ni vema na Haki... ila swali la kujiuliza tuna tatizo la mabanda au sehemu za kufanyia biashara ? Machinga Complex ilijaa au tulikosea wapi ?

Unaweza kusema ingawa frame / maduka yapo ila ni gharama Je Machinga wanashindwa kujichanga hata watano wakachangia frame (after all wamezoea kufanya kazi karibu karibu) si ni bora wakae kwenye nyumba kuliko mabanda ya mbao ?

Kuna wanaosema watafutiwe maeneo.., Je masoko yote yamejaa, Je kweli hakuna nafasi kwenye masoko au kuna masoko ambayo bado matupu..., Kila sehemu kuna mipango miji je ujenzi huu mpya unaendana na mipango miji. Na je jukumu la Serikali ambalo ni la muda mrefu ni kutafutia mabanda na kuwapanga au kuhakikisha watu wana ajira nzuri na sio kubangaiza ?, Je kila baada ya miaka mitatu mpaka mitano tutakuwa tunawapanga watu? nadhani hapa Serikali inaepuka wajibu wao wa kutengeneza Sera Mujarabu na kutumia short cut.

Kwahio naomba tujiulize, tatizo ni sehemu za kufanyia biashara ? (Sidhani sababu sehemu nyingi ni tupu): Je ni gharama ya hivi vyumba ? (nadhani hapana sababu kuna masoko yapo matupu na hawa wadau wanaweza kujichanga na kuchukua frame ambazo zipo sababu nyumba nyingi ni tupu)

Kwa hiyo huenda tatizo ni ajira za uhakika za watu kuweza kujipatia Kipato cha uhakika na kuacha Kubangaiza. Na hilo kwanini lisiwezekane kwa nchi Tajiri yenye Maliasili kama hii (Migodi, Maziwa, Bahari, Vivutio vya Watalii na Nchi Kubwa yenye Rutuba kila Kona) ?

Au tumeamua kuwa nchi ya Wachuuuzi ?
Shigella bwege sana ana akili za ukibwengo.
 
Machinga kuwekwa Machinga complex sio jambo la investigation stage,limeshapita huko namaanisha results tunazo tayari,kwamba wanarudi pale pale mjini, na hii ni prove the current solution/modal(kusambaza machinga kwenye maeneo mbali mbali is not working!)

Halafu sijui unakataa nini, machinga kujichanga na kuchukua frame ndio kupangwa huko, hivyo hivyo kwenye mall. Kukiwa na floor yao haimaanishi watakuwa wakikaa kiholela, NO.,ni frame zinapangwa kwenye floor na wao wanachukua hizo fremu ndani ya mall na kulipia, hiki kitu nimekiona mkuu ila sijajua wanalipaje hio rent

Swala la kodi zetu kujenga mall, kwanza ni responsibility ya serikali kuhakikisha inatengeneza mazingira mazuri na safe kwa biashara, so sioni kama ni hoja mkuu besides tukishatambua nani yuko kwenye fremu gani ni rahisi kukata kodi hata kama ni kidogo.

Formal arrangement nilikua namaanisha status sasa ya sasa hivi ni kuwa both wenye maduka na Machinga wanafanya biashara hapo hapo mjini,na WOTE wanatengeneza pesa, ni arrangement nzuri ndio inatakiwa, Machinga hawawazuii wenye maduka kutengeneza pesa,ingekua hivi ungekuta frame tupu hapo mjini,ila leo tafuta fremu kariakoo/mjini kama utapata kirahisi, mjini hapo ni kituo cha biashara kuwahamisha watu kuwe na this idea in mind.
Kwanini ujenge nyingine wakati zilizopo hazijajaa ?

Nilishasema kitambo ujenzi mwingi wa sasa wanafanya wawekezaji / developers na wao wanajenga ili mwisho wa siku pesa yao irudi kukiwa na demand ya nafasi watu watajenga wala hakuna haja ya kuwakumbusha.., ila kama kuna majengo yamejengwa (refer Rocky City Mall) na hayajaa ni matupu Na hata affordable places (Machinga Complex, Masoko Sehemu kadhaa Frame za nyumba) zote ni tupu hazijajaa..., sasa unadhani ukimpelekea developer plan yako ya kupandisha jengo lingine kama hajakuponda na proposal yako usoni atakuwa amekuheshimu sana...

Na kuzungumzia Kariakoo wote hatuwezi kulazimisha kukaa Kariakoo...., leo mtu akijenga ghorofa Kariakoo ana option ya kupata mpangaji wa kumlipa mara tano ya pesa ambayo machinga wanaweza kumlipa..., (profit per unit area) sasa unadhani itakuwa ni busara kumkatalia huyu mwenye uwezo ili tumpe yule asiye na uwezo kutokana na Nickname yake (Machinga)..., Ndio maana nikasema kuna sehemu tofauti za viwango tofauti kama hawa wadau wanaona Kariakoo ni gharama si wanakwenda kwenye gharama walizo na uwezo nazo ?
 
Kwanini ujenge nyingine wakati zilizopo hazijajaa ?

Nilishasema kitambo ujenzi mwingi wa sasa wanafanya wawekezaji / developers na wao wanajenga ili mwisho wa siku pesa yao irudi kukiwa na demand ya nafasi watu watajenga wala hakuna haja ya kuwakumbusha.., ila kama kuna majengo yamejengwa (refer Rocky City Mall) na hayajaa ni matupu Na hata affordable places (Machinga Complex, Masoko Sehemu kadhaa Frame za nyumba) zote ni tupu hazijajaa..., sasa unadhani ukimpelekea developer plan yako ya kupandisha jengo lingine kama hajakuponda na proposal yako usoni atakuwa amekuheshimu sana...

Na kuzungumzia Kariakoo wote hatuwezi kulazimisha kukaa Kariakoo...., leo mtu akijenga ghorofa Kariakoo ana option ya kupata mpangaji wa kumlipa mara tano ya pesa ambayo machinga anaweza kulipa..., sasa unadhani itakuwa ni busara kumkatalia huyu mwenye uwezo ili tumpe yule asiye na uwezo kutokana na Nickname yake (Machinga)..., Ndio maana nikasema kuna sehemu tofauti za viwango tofauti kama hawa wadau wanaona Kariakoo ni gharama si wanakwenda kwenye gharama walizo na uwezo nazo ?
Mkuu tuache hapo mjadala baki unavyoamini ,nishaeleza why huko kwingine hapafai kupaendeleza ni wastage of time sababu tuna example tayari ( Machinga complex) kwamba watarudi hapo hapo mjini, adios.
 
Kuna ukweli mmoja ambao wataalamu wetu hawauongei...ni hivi,imefika muda population ya Tanzania ime-"burst",hii inamaanisha watu waliopo hawaendani na zao la rasilimali zilizopo.........production ni ndogo mno kuliko mahitaji halisi ya jamii.

Ukienda hospitali madaktari watakuambia kuhusu hilo suala,hadi imefika muda hata obstetrician hawataki kufanya kazi zao,sababu mabinti wadogo(chini ya miaka 20),wanazaliana sana ilihali hawana elimu basic tu ya afya na uchumi wao ni mbovu mno,si ajabu kukuta binti wa miaka 25 ana watoto sita na yeye anaishi kwenye nyumba ya mama yake ya tembe na watoto wake isiokua na umeme.......huku baba wa hao watoto ni bodaboda mwenye watoto na wanawake kama watatu aliowazalisha.......hao watoto sita wakiwa wakubwa lazima tu wawe machinga.

Einstein aliwahi sema"you can't fix the problem with the same reason it occur"
Issue ya machinga ni multisectorial factors.........lazima tuanze kufix elimu na uchumi wa mtu mmoja mmoja,ama clusters ndogo ndogo strategically

Hata mungu alianza kuumba kwanza vitu ndio akaumba watu,hakua mjinga.

Sasa jitu linazaa watoto 4 linamiliki chumba kimoja,hio ni zambi tayari mbele ya mungu.
Huduma za afya,hasa za uzazi lazima ziwe za kulipiwa,elimu ya bure ife,sheria za kutekeleza mtoto ziwe ngumu zaidi,.......ukizalisha na kutekeleza ukikamatwa ufungwe kwanza ama faini itakayotosha kumuhudumia mtoto kwa angalau miaka kumi,ama kukatwa mshahara kwa lazima kwa waajiriwa.

Yaani huduma zote hata maiti hospitali inalipiwa,ila kuzaa ni bure,WTF?

Hatuwezi kuwa na watoto wanaokujua kuteseka duniani hilo lazima tu-admitt,.....

Yanahitajika maamuzi magumu ili kuzuia na kupunguza machinga,maamuzi ya kisera zinazogusa sekta za Afya,Elimu,na Sheria.........

Miaka 5 ijayo tutakuwa na mamillioni ya watu wenye miaka zaidi ya 50,wenye wajukuuu,wakiwa bado machinga wasiojiweza,wakilala mabarabarani,uhalifu utaongezeka, na uovu wa jamii kama kujiuza na ushoga nao utaongezeka.

TUNAHITAJI "COMPLETE OVERHAUL" ya sheria zetu za afya na elimu.

Kwa muliobahatika kusoma jitahidi uzae watoto wachache,hata wawili tu...issue ya wa kwamba akifa mmoja atabaki mmoja hio ni psychology tu,kwani ukiwa na watoto kumi ambao hawana kazi,walevi,mateja na vibaka wasio na uwezo wowote ule wanatofauti gani na maiti?,issue kua nitazikwa na nani?,ukiishi maisha ya kumpendeza mungu, na vizuri na watu,utazikwa tu na watu wastaarabu,ila sio kuongeza population isyokua na maana itakayokuja kuteseka for cheap reasons zisizokua na mashiko...gharama za maisha zinapanda sababu ya production chache......imagine nguvu kazi yote hii ya Tanzania mafuta ya alizeti Lita 8,000/=,vijana kibao wangeweza kulima Alizeti na kuuza wapo wana chuuza chupi,charger za simu na vibanio mjini?,....Huu ujinga ni kama laana hivi,na majitu masikini hata hayashtuki yanaendelea tu kufyatuana[emoji16][emoji16]
 
Mfano machinga wa k koo....mnao sema wajichange wachukue frame hivi mnajua k koo frame bei gani au mnafikiri ni laki 1 laki2....kuhusu machinga complex lile eneo limejengwa alafu baada ya kuwapa machinga wa karume wakachukua viongozi wa juu wakawa wanawapangisha machinga kwa hela kubwa....wengi machnga kariakoo meza wengi wanapanga kwa laki moja mpaka laki na nusu kwa mwezi sasa hawa ili waweze kujichanga wawe na frem k koo lazima wawe machinga kama 10 hiv sasa hiyo itakua biashahara au uchafu....wengi wanasema machinga waondoke na wakati serikali haija watengea mazingira na kama hujui maisha wanayo pitia hawa watu wana somesha na wanaendesha maisha yao kwa hizo biashara so serikali inatakiwa kuwawekea utaratibu bila kuathir biashara zao
 
Kuna ukweli mmoja ambao wataalamu wetu hawauongei...ni hivi,imefika muda population ya Tanzania ime-"burst",hii inamaanisha watu waliopo hawaendani na zao la rasilimali zilizopo.........production ni ndogo mno kuliko mahitaji halisi ya jamii.

Ukienda hospitali madaktari watakuambia kuhusu hilo suala,hadi imefika muda hata obstetrician hawataki kufanya kazi zao,sababu mabinti wadogo(chini ya miaka 20),wanazaliana sana ilihali hawana elimu basic tu ya afya na uchumi wao ni mbovu mno,si ajabu kukuta binti wa miaka 25 ana watoto sita na yeye anaishi kwenye nyumba ya mama yake ya tembe na watoto wake isiokua na umeme.......huku baba wa hao watoto ni bodaboda mwenye watoto na wanawake kama watatu aliowazalisha.......hao watoto sita wakiwa wakubwa lazima tu wawe machinga.
Jambo la maana ni sustainability enzi za mababu zetu za kilimo ilikuwa kuzaa sana ni utajiri sababu hao watoto watalima na ukiwa na wake wengi hence ardhi nyingi na wafanyakazi wengi (watoto ) huo ni utajiri. Mambo yamebadilika dunia nzima nguvu kazi sio issue tena.., na Kwa Tanzania ingawa hali ni ngumu kesho itakuwa ngumu zaidi..., sababu bado maeneo ni matupu ila tukiendelea na kuwa na Taifa la Wachuuzi wasio na uwezo wa kujigharamikia na kujipatia mahitaji, the future is scary....

Hapa Serikali na yenyewe haifanyi kazi yake sababu hata hao wanaomaliza shule unawaambia waingie mtaani kubangaiza..., uzeeni hawana pension (watakuwa wazee mzigo wa taifa) wakiugua siku moja hawana savings yoyote ni kwamba wamefilisika. Cha kutisha kesho yetu haitakuwa ngumu kwao tu hata wanajiona wanavyo watakuwa hatarini sababu ukiwa na watu wengi with nothing to loose..., soon or later watakuja kuchukua what's yours....
Einstein aliwahi sema"you can't fix the problem with the same reason it occur"
Issue ya machinga ni multisectorial factors.........lazima tuanze kufix elimu na uchumi wa mtu mmoja mmoja,ama clusters ndogo ndogo strategically
Naam tunahitaji kuwa na watu with buying power..., hapo wala hatutasumbuka kutafuta masoko nje sababu hata watu wa ndani watakuwa na pesa za kununua.... (kwahio tutaweza kuuziana na kununuliana)
Hata mungu alianza kuumba kwanza vitu ndio akaumba watu,hakua mjinga.

Sasa jitu linazaa watoto 4 linamiliki chumba kimoja,hio ni zambi tayari mbele ya mungu.
Huduma za afya,hasa za uzazi lazima ziwe za kulipiwa,elimu ya bure ife,sheria za kutekeleza mtoto ziwe ngumu zaidi,.......ukizalisha na kutekeleza ukikamatwa ufungwe kwanza ama faini itakayotosha kumuhudumia mtoto kwa angalau miaka kumi,ama kukatwa mshahara kwa lazima kwa waajiriwa.
Watu lazima wawe responsible..., ingawa hata hizo so called bure sio bure na quality yake ni mediocre..., cha maana watu wepewe nyenzo za kuweza kujilisha, unaweza kumlaumu mtu kwanini halimi na kupata chakula akala kumbe kosa ni la kwako badala ya kumpa jembe umempa koleo..., kwahio kwa kuwa na utamaduni wa kuwapa watu skills za maisha za kufanya kile kinachohitajika..., mkulima akifanya kazi yake ya kulima apate masoko (sio tena unataka awe marketing expert) akilima chakula kikiwa kingi unamsahau kikiwa kidogo unamwambia hakuna kuuza nje (hio ni kuwafanya wengine waone kule hakulipi)
Yaani huduma zote hata maiti hospitali inalipiwa,ila kuzaa ni bure,WTF?

Hatuwezi kuwa na watoto wanaokujua kuteseka duniani hilo lazima tu-admitt,.....

Yanahitajika maamuzi magumu ili kuzuia na kupunguza machinga,maamuzi ya kisera zinazogusa sekta za Afya,Elimu,na Sheria.........

Miaka 5 ijayo tutakuwa na mamillioni ya watu wenye miaka zaidi ya 50,wenye wajukuuu,wakiwa bado machinga wasiojiweza,wakilala mabarabarani,uhalifu uatongezeka, na uovu wa jamii kama kujiuza na ushoga nao utaongezeka.

TUNAHITAJI "COMPLETE OVERHAUL" ya sheria zetu za afya na elimu.
We need an optimum productive population...., Kama hao watoto watakuja kuwa productive, wazalishaji ni fair game (and we need more of them) ila kama watakuja kuwa omba omba ndio hivyo tena...., Tunahitaji watu responsible na ni ukweli usiopingika Duniani hakuna cha Bure hata kama utakipata kuna mtu Anakilipia....
 
Mfano machinga wa k koo....mnao sema wajichange wachukue frame hivi mnajua k koo frame bei gani au mnafikiri ni laki 1 laki2....kuhusu
Kwani lazima kila mtu akae Kariakoo ? Kariakoo ni moja ya Prime areas Tanzania na hio haikuja kwa bahati mbaya...
machinga complex lile eneo limejengwa alafu baada ya kuwapa machinga wa karume wakachukua viongozi wa juu wakawa wanawapangisha machinga kwa hela kubwa....
Kwahio solution ni kuwaondoa hao viongozi wabadhirifu na sio kujenga mabanda mengine huku na kule..., na kama hao machinga wanapangishwa kwa pesa kubwa na walikuwa wanapanga nadhani ni wakati muafaka kurudia definition ya Machinga..., (Huenda kila mfanyabiashara wa Kati Tanzania ni Machinga.
wengi machnga kariakoo meza wengi wanapanga kwa laki moja mpaka laki na nusu kwa mwezi
Na hao tunawaita Machinga ?, Basi Tanzania ni nchi Tajiri sana. Na hao ujue mpaka waweze kulipa hizo basi Biashara hapo ipo, ila kuwa kwao kwenye meza huenda TRA wasiwapate hivyo overheads (gharama za uendeshaji kwao zikawa ndogo tofauti na wengine)
sasa hawa ili waweze kujichanga wawe na frem k koo lazima wawe machinga kama 10 hiv sasa hiyo itakua biashahara au uchafu...
Naam wajichange hata ishirini kama biashara ipo na wanaweka mizigo kidogo kidogo mingine stoo na hapo wanaweza kupeana shift badala ya wote kukaa hapo wakafanya mengine, au kutengeneza ajira kwa kuweka muuzaji na wao kusimamia chain nyingine. By the way kwanini wote wakae Kariakoo, kama hatuna uwezo wa Kariakoo si pengine kupo ?
.wengi wanasema machinga waondoke na wakati serikali haija watengea mazingira na kama hujui maisha wanayo pitia hawa watu wana somesha na wanaendesha maisha yao kwa hizo biashara so serikali inatakiwa kuwawekea utaratibu bila kuathir biashara zao
Machinga kuendelea kufanya kazi kwao sehemu hatarishi ni hatari kwao / kwetu hawa ni ndugu zetu na sisi na maisha haya huenda ni potential machinga kesho tukawa tunabangaiza..., sasa suluhisho sio muendelezo wa kubangaiza bali ni kutafuta shughuli endelevu za uzalishaji zitakazohakikisha tunaweka pesa ya mafao ya uzeeni na tukiugua hatumalizi akiba yote ya pesa. Na kwa nchi yenye maliasili haitakuwa mazingaombwe kubadilika kutoka kwenye taifa la wabangaizaji / wachuuzi kwenda kwenye taifa ya wazalishalishaji wanunuzi....
 
Kkoo frame mpaka laki 3 sema kupata frame ndo shida..
wao wanataka pale barabarn katikati ndo kuna pesa.

Me nina rafik yangu wanapangisha frame zile ndogo laki 3 na laki 4 ila pameja
 
Kkoo frame mpaka laki 3 sema kupata frame ndo shida..
wao wanataka pale barabarn katikati ndo kuna pesa.

Me nina rafik yangu wanapangisha frame zile ndogo laki 3 na laki 4 ila pameja
Nadhani tungeruhusu biashara kila mahali bila utaratibu hata mimi ningependa niweke Biashara yangu ya maji pale Bungeni karibu na Meza ya Spika ila ndio hivyo tena tunachokitaka na kilichopo ni tofauti..., au pale kwenye Bustani ya Ikulu ningeweka vinyago vyangu siku wageni kutoka nje wakija lazima ningeuza
 
Back
Top Bottom