Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Niliona Morogoro wanazindua vibanda vya Machinga...
Hio ni vema na Haki... ila swali la kujiuliza tuna tatizo la mabanda au sehemu za kufanyia biashara ? Machinga Complex ilijaa au tulikosea wapi ?
Unaweza kusema ingawa frame / maduka yapo ila ni gharama Je Machinga wanashindwa kujichanga hata watano wakachangia frame (after all wamezoea kufanya kazi karibu karibu) si ni bora wakae kwenye nyumba kuliko mabanda ya mbao ?
Kuna wanaosema watafutiwe maeneo.., Je masoko yote yamejaa, Je kweli hakuna nafasi kwenye masoko au kuna masoko ambayo bado matupu..., Kila sehemu kuna mipango miji je ujenzi huu mpya unaendana na mipango miji. Na je jukumu la Serikali ambalo ni la muda mrefu ni kutafutia mabanda na kuwapanga au kuhakikisha watu wana ajira nzuri na sio kubangaiza ?, Je kila baada ya miaka mitatu mpaka mitano tutakuwa tunawapanga watu? nadhani hapa Serikali inaepuka wajibu wao wa kutengeneza Sera Mujarabu na kutumia short cut.
Kwahio naomba tujiulize, tatizo ni sehemu za kufanyia biashara ? (Sidhani sababu sehemu nyingi ni tupu): Je ni gharama ya hivi vyumba ? (nadhani hapana sababu kuna masoko yapo matupu na hawa wadau wanaweza kujichanga na kuchukua frame ambazo zipo sababu nyumba nyingi ni tupu)
Kwa hiyo huenda tatizo ni ajira za uhakika za watu kuweza kujipatia Kipato cha uhakika na kuacha Kubangaiza. Na hilo kwanini lisiwezekane kwa nchi Tajiri yenye Maliasili kama hii (Migodi, Maziwa, Bahari, Vivutio vya Watalii na Nchi Kubwa yenye Rutuba kila Kona) ?
Au tumeamua kuwa nchi ya Wachuuuzi ?