Machinga waanza kunyanyaswa rasmi hawatakiwi huu si wakati wa wanyonge

Mwendazake aliwatumia Machinga kwa faida ya kujijenga kisiasa. Kwanza aliwaita wanyonge. Mnyonge naliona kama tusi kwa Watanzania. Tafsiri yake hii hapa:

1.mtu dhaifu; mtu asiyekuwa na nguvu Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni (ms) Synonyms: mnyela
2. mtu mwenye tabia ya upole na ya kunyenyekea
3. mtu wa hali ya chini Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda (methali)

Binafsi silipendi hili neno, tupaze sauti sauti wana siasa wasituite sisi wanyonge, watumie neno wananchi au Watanzania, waache kutusanifu.

Hao machinga, kuambiwa wafuate utaratibu wa mipango miji na Halmashauri siyo manyanyaso
 
Machinga kukaa kwenye jengo ni ngumu sana! Kuna style moja niliona Moshi nafikiri ile ndio sahihi! Kunajengwa jengo kama mall kisha hao machinga wapange biashara zao humo kwa siku maalum ndani ya week!

Inajulikana kabisa ni sale!
 
Hata Sinza Palestina Hospital imezungukwa na vibanda haijulikani ni Hospital ama ni nyumba ya Wageni.
 
Ndo maana sheria zikawepo,kama waliruhusiwa kufanya biashara popote mbona hawafanyii biashara zao ikulu au kwenye kambi za jeshi? Magufuli amekua Magufuli
 
Hao machinga wenyewe wachafuzi wa mazingira.Usijifanye unampenda hayati Magufuli.Mnatandaza bidhaa zenu sehemu za wapita kwa miguu,inawabidi wapite ndani ya barabara kuu ,watoto wa shule,na wengineo wanagongwa na magari,daladala,bodaboda n.k mmetandaa kote hadi mbele ya maduka na mahoteli ya walipa kodi.Waongo nyie.Hongera manispaa zinazofuata utaratibu wa kuwaondoa hao machinga mabarabarani.watengeeni maeneo maalum.Nchi lazima iwe safi na kwa mpangilio.sio kila mtu akiambiwa ukweli anajifanya mnyonge anaonewa.Nashauri Zoezi la kuwaondoa machinga mabarabarani na maeneo mengine yaendelee.Mfano nenda kituo cha mabasi cha Magufuli Mbezi,Yaani utasema nchi yetu haina serikali.Vurugu mtindo mmoja.wamachinga,mama lishe kibao.uchafu unaletwa na hao machinga.muda wowote magonjwa ya milipuko itatokea.Wamachinga,mama lishe watengewe sehemu maalum kama wenzetu wa nchi nyingine.
 
aiseh!

unajua, siku zote, wanaopiga kura kwa wingi nchini ni watu wasio kuwa na twitter, instagram ama account kwenye forums kama hapa jamii forums.

labda wengi wao wangekua kwenye hii mitandao ya jamii, tengepata mawili matatu!

pole yao!
 
Naona wanyonge wamejikuta pekeyao katikati ya safari tuliwaambia tunahitaji mfumo imara sio mtu imara(imara kwa kauli za wanyonge)

Haya sasa sisi tusiokuwa wanyonge safari yetu bado inaendelea kuelekea kudai huo mfumo tulioutaka miaka tangu na tangu
 
Mbona umeweka picha hiyo hiyo moja mara nyingi hivyo? Naungana na serikali maana Jiwe aliwadanganya sana hawa Machinga, tunataka miji iwe safi bwana! Watu wanaangalia bidhaa mpaka mwenye maduka ya wenzao bwana, hapana hatuwezi kwenda hivyo!
Ningependa thge same ifanyike kwa miji yote nchini ikiwa ni pamoja na K/koo, Stand mpya ya mabus ya Mbezi Dar. Wamachinga waendeshe biashara zao kwa kufuata sheria zilizowekwa na mamlaka husika kwa usalama wao na muendelezo wa biashara zao.
 
Nilipita mitaa ya Posta ndani ya Dar Es Salaam, baadhi ya mitaa imeharibiwa kabisa na vibanda vya wamachinga. Yaani hakuna mpangilio wala sehemu ya wapita miguu. Ni kero kubwa sana, waondolewe na wapelekwe sehemu maalum ya kufanya biashara zao.
 
Wangeomba kwa baba hati miliki
Ila kwa kuwa zilikuwa kauli zake basi vumilieni tu wasafishe mji kwa sheria na kanuni badala ya neno la mtu mmoja
 
Wewe ni hohehahe wa akili ambaye hujui hata kuwa kuna kitu kinachoitwa mipango miji.
 
Wamachinga wangeweza kujipanga nchi nzima wawe na umoja wao,uongozi wao
Wangetisha sana

Ova
 
Hawa machinga nikiangalia kwa jiji la dar hawa ndio wanaosababisha foleni barabarani wanapanga bidhaa zao sehemu ambayo ni za watembea kwa miguu mwisho wa siku wananchi wamekuwa wanapita barabara za magari
 
Machinga hawa wanatakiwa wawe sehemu sahihi kulingana na level yao , unakuta mtu analipa frem laki Saba , mbele yake kuna machinga analipa 50000 , af anachekelea na kujiita mpambanaji... ..Fukuza kabisa hao watu waende sehemu sahihi ya umachinga
Mkuu umekosea siyo 50,000 wanalipa 20,000 wanapewa Kitambulisho cha kuvinjaro popote watakapo kufanyia Biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…