Machinga waanza kunyanyaswa rasmi hawatakiwi huu si wakati wa wanyonge

Hao watu wengi hawajasoma hivyo hawaelewi mambo ya mfumo.
Naona wanyonge wamejikuta pekeyao katikati ya safari tuliwaambia tunahitaji mfumo imara sio mtu imara(imara kwa kauli za wanyonge)

Haya sasa sisi tusiokuwa wanyonge safari yetu bado inaendelea kuelekea kudai huo mfumo tulioutaka miaka tangu na tangu
 
..Meko sijui alitubu kuwaibia wamachinga buku 20 na kuwapa vitambulisho feki?
 
Wananyanyaswaa au wafuate utaratibu, watu wanafunga njia sasa kulikua na haja gani ya kutumia pesa za walipakodi kuzijenga? Duniani kote machinga wapo ila sio hawa wakufunga njia, ni mjinga tu anaweza kuona watu wananyanyaswa kutakiwa wafiate utaratibu
 
Yaani miji imekua kama ya wajinga
Nilipita mitaa ya Posta ndani ya Dar Es Salaam, baadhi ya mitaa imeharibiwa kabisa na vibanda vya wamachinga. Yaani hakuna mpangilio wala sehemu ya wapita miguu. Ni kero kubwa sana, waondolewe na wapelekwe sehemu maalum ya kufanya biashara zao.
 
Watu wanaharibu kingo za barabara, wanafanyia biashara maeneo hatarishi, wapo kingo za barabara na mimeza yao, wadadiriki hata kujenga vibanda vya kudumu! Jamani hata sio mapenzi tena tuwe na utaratibu!! Tunajenga barabara na kugeuza soko!? Kwa nini sasa tusijenge masoko kwanza?
 
Watu magonjwa ya kisukari yanaongezeka kwa kukosa pa ketembelea huku mjini mtuonee huruma
 
Wamachinga wafuate sheria za nchi watafanya biashara zao kwa raha zao vinginevyo watakereka kama wanavyowakera wengine sasa.
 
Mnadeka sanaa
 
Unawezaje kujenga strong institution mkuu??
Hii myth sijawahi kuilewa... Institution ipo ila willingness ya wahusika/viongozi wa kila ngazi ndio shida..

Nipe shule mkuu
We need strong Institutions and not strong Persons!!!!

Na haya ndo madhara yake!!!!!
 
Ndo maana sheria zikawepo,kama waliruhusiwa kufanya biashara popote mbona hawafanyii biashara zao ikulu au kwenye kambi za jeshi? Magufuli amekua Magufuli
Mimi kwa kweli ninakerwa sana na wanavyojenga juu ya mifereji ya maji kwa kuweka mabanzi na kujenga vibanda. Huu ni uharibifu wa miundombinu.
 
Binafsi silipendi hili la kuitwa mnyonge
Kuna mtu nishawahi mtukana kisa kaniita mnyonge
 
Hao mgambo waende na Dar...

Kuna mahali hao wamavhinga wamejenga mabanda yao hadi barabarani kiasi kwamba sehemu ya njia mbili imekuwa moja...
 
Wazee wa legasi kutetea upuuzi ,sasa wamachinga wanafanya biashara barabarani unafikiri mtu anayejielewa anaweza kusupport? Wajengewe sehemu huzika za kuuza biadhaa zao na sio kuzuia barabara.
 
Mwendazake aliwatumia machinga kwa maslahi yake binafsi, acha waone uhalisia
 
Mnatetea kitu ambacho si endelevu.
Machinga si sekta rasmi ambayo hairatibiwi popote.
Tujikite katika sekta endelevu ambazo zina uzalishaji kama kilimo, biashara rasmi, uzalishaji kiviwanda vidogo n.k.

Hao machinga wametumika muda mrefu kama mtaji wa kisiasa, wapumzike sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…