Machinga waanza kunyanyaswa rasmi hawatakiwi huu si wakati wa wanyonge

Binafsi sifagilii machinga kufanya biashara holela kiasi hiki na hii altendo iliyoanzia huko iendelee nchi nzima, waelekezwe kwenye maeneo ramsi.
 
Nchi /nyumba isiyokuwa na mpangilio ni jalala.
Kuna tatizo gani ukiwaita na kuwaelekeza njia nzuri ya kufanya biashara zao kuliko kuwawinda na kuvunja meza na kupora mali zao
 
Tanzania SIO taifa la Wanyonge na Wamachinga.
 
Tuulizeni tuanokaa huku sio mnakurupuka tu...before hujajaji tambua kwamba mkurugenzi alipitisha tangazo la kuwataka hao machinga kuhamia soko la dodoma na pia walipewa wiki nzima ya kujiandaa kuondoka na hata mkuu wa wilaya mwenyewe najua alisikia ila aliziba masikio wakakaidi ndipo usiku wa kuamkia jumapili mgambo wakafanya yao..kwa tunaoishi huku tunaelewa kwamba mkuu wa wilaya na mkurugenzi hawapatani wew imagine mwenye mji anajaribu kuushape mji wake ukae kwenye muonekano wa kimjini mkuu wa wilaya analeta siasa na hata sasa hawa machinga wamerudi kwa amri ya mkuu wa wilaya.. Endapo tutaendelea kuwa na huyu mama wilaya ya njombe isahau kabisa hata kuendelea na kupata hata kamanispaa tu🥱. Mji wa njombe haupo kabisa kwenye mpangilio uko rafu utadhani haina maafisa mipango miji kumbe siasa ndo inaturudisha nyuma.. Kama mama na mkuu wa mkoa wataona andiko hili wamuache mkurugenzi aushepu mji wake sio kuleta siasa hata kwenye vitu vya maendeleo.. Nyie ni wateule tu waacheni watendaji wafanye kazi zao.

NB: uhuru bila mipaka ni vurugu[emoji3061]
 
Kuna tatizo gani ukiwaita na kuwaelekeza njia nzuri ya kufanya biashara zao kuliko kuwawinda na kuvunja meza na kupora mali zao
Yah!! Ili wakome na wasirudi tena maamae!! Ngoja nikafue zile kombati zangu za mgambo sasa, hazijafuliwa miaka 7 maanina zake!!
 
Kuna tatizo gani ukiwaita na kuwaelekeza njia nzuri ya kufanya biashara zao kuliko kuwawinda na kuvunja meza na kupora mali zao
Ni wa korofi!! Wajue kuna taratibu na sheria!! Huwezi weka vitu vyote sebuleni
 
Machinga si wa kuendekeza hata kidogo, na viongozi wenye mamlaka waache mara moja kutoa matamko ili kupata kura za watu wasiolewa taratibu za miji.
 
Yaani picha 9 kwa moja, kuna nyakati inakupasa mtu kuchumpa baadhi ya maandiko
 
Tujifunze kuishi kwa kufuata sheria, kuwa machinga hakukupi haki ya kufanya biashara popote bila kufata utaratibu. Bado wale wa Kariakoo na stendi ya mbezi.
 
kama wanasababisha uchafu, fukuza kabisa ili wajifunze. kuna mambo usipokuwa mkatili kidogo hayatakuja yawe mazuri. Tz ukitoka nje ukishuka tu hadi harufu ni tofauti uchafu all over. watengenezewe mazingira maalumu, ila mtu kuamua kutenga sufuria la wali pembeni mwa barabara, hakuna choo, hakuna sehemu ya kutupa taka, mara anaosha mavyombo, utakuta mwingine ameamua kupanga matunda chini barabarani, mwingine amepanga nguo sijui nini, hakuna utaratibu. tutaishije bila utaratibu?
 
Kumbe ndo maana wamachinga walilia sana siku, ila basi jamani rudini tu maeneo yenu ya kazi maana wamachinga hao hao pia walikuwa wakilia kuwa wamabenwa nadhani sasa na wakati wa kuachiwa, hakuna kubanwa banwa tena.
 
Lazima tubadilike tuwe na majawabu ya kudumu
 
Hakika ni mambo ya ajabu sn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…