Machinga wasilete siasa waondolewe haraka miji yote Tanzania

Nadhani cha kufanya wajiunhe hata 10 ikibidi, wachukue fremu na wafanye bishara rasmi
 
Big NO! Si wewe uliyekuwa mwanafunzi wa university mojawapo nchini uliyesomeshwa na wazazi wako kupitia huo umachinga!
Tz ni taifa pekee katika sayari hii kwa kukamua ng'ombe bila kumlisha vizuri,wekeni mazingira wezeshi kisha watakeni kulipa hiyo kodi.
 
Machinga ni wale wanaozunguka na bidhaa mkononi wale ndio wapewe vitambulisho vya ujasiriamali lakini wale wanaojenga vibanda ni wakwepa kodi tu, wengi wana mitaji mikubwa wanastahili kulipa kodi haiwezekani wenye viduka uchwara na cafe mitaani walipe kodi eti kwa kuwa wamepanga fremu lakini wenye vibanda mabarabarani wao wapewe vitambulisho hiyo siyo haki.
 
Anayestahili kupewa kitambulisho ni mfanyabiashara mdogo yoyote aliye na mtaji wa -4000,000/=. Mengine hayo ni tafsiri yako.
 
Wakati mnawaruhusu kipindi cha kampeni zenu za majitaka hamkuyajua haya, hovyo kabisa.....
 
Mkuu, hao ndio wanarudi kitaa kutafuta pesa kwa ngeta!
Hivyo tukae mkao wa kutulia, tusubiri yajayo.

Nadhani kungekuwa na smooth transitiin ya maeneo wanayopaswa kufanyia biashara zao, na si kibabe kama ilivyokuwa leo vingunguti.
Wa wao wakae standby kupigwa viberiti na petroli without hesitation huku mtaani..hatutacheka na mwizi.
 
Yaani Samia inabidi akomae watu waondoke huko mabarabarani..kuna mmoja leo nimemsikia anasema amekopa 15m lakini biashara anafanya katikati barabarani kwenye kibanda cha maturubai..kama sio ujuha kuendelea kuwaacha hawa watu ni nini?..
 
Hata hili la kujiunga ili wapate nguvu ya kuchuka fremu na walipe kodi unataka kubisha?
HAIWEZEKANI watu wa kaliba tofauti muungane mkodishe fremu Kariakoo ya 1,000,000 muuze sidiria mwingine madera, haya mawigi nk hamtaelewana chumba kimoja, km mama ntilie tu kuuza chapati mwingine mihogo au maharage mtaa mmoja hawapatani sembuse Machinga
Dawa ni kuwatoa wakatafute mbali na maduka ya wenzao wanauza vifaa vya electronics, au vya umeme huwezi weka Wamachinga
 
Yaani Samia inabidi akomae watu waondoke huko mabarabarani..kuna mmoja leo nimemsikia anasema amekopa 15m lakini biashara anafanya katikati barabarani kwenye kibanda cha maturubai..kama sio ujuha kuendelea kuwaacha hawa watu ni nini?..
Huyo ni mkwepaji Kodi mzuri unawezaje kuchukua mkopo wa million 15 alafu unafanya biashara kwenye kibanda Cha maturubai
 
Vingunguti Scania
Kata Kiwalani Dar es Salaam
Tanzania


WAMACHINGA WAANZA KUTII AMRI, WAPANGWE UPYA


Sasa wapita kwa miguu wanatembea katika maeneo yao bila hatari ya kugongwa na magari. Kuvunjwa kwa vibanda mji unaanza kurudisha sura yake na pia usalama waongezeka. Shukrani ziuwendee uongozi wa mkoa chini ya RC Amos Makala na timu yake kwa uthubutu.

Machinga walia kwa kulaani hatua hiyo, lakini hawajali hali na haki za wakaazi wengine wa jiji hili maarufu la Dar es Salaam.
 
WAMACHINGA WAPANGIWA MFUMO MZURI WA KUWAPANGA, JIJI LIENDELEE KUWA SAFI NA SALAMA


Machinga kuondolewa Dar, Uongozi wa jiji watoa TAMKO la jinsi machinga wajipange ili kuwezesha usalama wa wapita njia pia ukusanyaji taka ktk barabara kuu kuu kufanyika bila vikwazo
 
MACHINGA COMPLEX DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo amekutana na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex na kusikiliza kero zao, wapate mazingira salama ya shughuli zao na wateja wao huku jiji letu likiendelea kurudisha hadhi yake ya usafi , usalama kwa watu bidhaa na kanuni kufuatwa za jinsi ya kuendesha biashara ndogo a.k.a umachinga, mamantilie, gereji n.k

 
September 2021
Soko la Tegeta
Dar es Salaam

Mfano wa masoko yanayofuata kanuni za kujipanga

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…