Machinga wasilete siasa waondolewe haraka miji yote Tanzania

Machinga wasilete siasa waondolewe haraka miji yote Tanzania

Nadhani cha kufanya wajiunhe hata 10 ikibidi, wachukue fremu na wafanye bishara rasmi

Sawa sawa kabisa hiyo ni njia sahihi ya kuwaondoa ktk sehemu za wapitanjia na barabarani. Waanzishe viji SACCOS wakodishe vyumba / fremu kutoka nyumba, maduka , majumba, mini supermarkets, supermarkets, malls, mmachinga complex ktk nyumba zilizo pembeni mwa hizo barabara.
 
Mjini Kampala ukienda luwum street utaamini hili
Machinga wanajiunga wanne mpaka watano wanakodisha frame ila ndani ya fremu kila mtu anauza chake
Pia hapa Tanzania
ifike mahali machinga waungane wakodi fremu na sio kuhodhi brbr za watembea kwa miguu
Wapi tunafeli kuwapanga machinga kila wakati makundi ya machinga yanaongezeka
Tusitumie nguvu kubwa kuwapeleka kwenye masoko la hasha wapewe elimu ya namna ya kupanga frame kwa watu wanne watano ili nao walipe kodi
Mbona hata wauza simu kariakoo wanafanya hiv

Unakuta frem moja na watu 10 kila mtu kivyake
 
Sielewi kama vitambulisho vya wajasilia mali wadogo kuna sheria ama kanuni gani iliyoasisi kuanzisha vitambulisho hivyo.

Mi niliona tu Rip Jpm akivipromote.
Hakutumia Sheria yoyote...


Hapo ndo tatizo lilipoanzia...

Kama ipo,. anaeijua elf 20 kwa wajasiriamali kisheria atuwekee hapa..
 
Aina ya uandishi ulioutumia unaonyesha umewahi gombana na machinga kwa hiyo una bifu nao,halafu Unaonekana bado unakaa kwa dada yako halafu umetumia simu ya shemeji yako kupost huu uzi.
Fremu leo zimedoda mikoa yote, ina maana Machinga wanashindwa kujiunga hata watatu watatu wakachukua fremu wakaripa Kodi?

Nchi imekuwa ya kipuuzi sana mama ntilie wanashindwa kujiunga wakatengeneza taasisi inayolipa Kodi na wakafanya derivali ya chakula kwenye maofisi mida ya mchana?

Mpaka wakae kila Kona ya mtaa. Ebu tuache ushamba basi

Nashauri Machinga wathibitiwe Kama wanagoma vibanda vyao vyote vichomwe hatuwezi kuwa na taifa la watu wasiolipa Kodi, kufuata Sheria na katiba ya Nchi .

Mbaya zaidi kupoka haki za wengine hii haikubaliki hata kidogo lazima tuwe taifa la mfano.

Na mikoa yote ondoeni Machinga wenye mitaji mikubwa wakapange fremu wauze online bidaa zao wafanye derivali.

Wenye mitaji midogo watengewe viwanja vikubwa viwe Kama minada wafanye uko mbona kila mkoa unayo maeneo?

Makala nakushauri vunja kabisa kila kitu maana wabongo Ni wabishi Sana bila kuwavunjia hawataondoka kwa heri.

Tujenge Nchi tuache kufanya kila kitu siasa. Siasa ndio imetufikisha hapa tulipo.
 
SIASA ZA MACHINGA

Msukuma: Samia ameteua watu wa ovyo, alikubaliana na Magufuli Machinga waachwe, leo amewageuka,




Source : Bongo Sihami
 
24 September 2021
Dar es Salaam, Tanzania

KIONGOZI WA MACHINGA - TUNAAFIKI HATUA YA KUONDOA MACHINGA KATIKA BARABARA KUU



Baada ya vikao kufuatia zoezi la mwanzo ambalo limelenga kuanza kusafisha machinga toka barabara kuu na kubwa za Dar es Salaam, Kiongozi wa machinga jijini DSM wamekiri wapo tayari kutoka maeneo hayo ya mwanzo na kuomba serikali iharakishe jinsi ya kuwapanga vizuri ili Jiji lirejee katika mpangilio mzuri utakaoleta usalama na usafi na pia machinga kupata sehemu bora za kufanya biashara zao kwa kufuata kanuni za mipango miji
Source : Global TV online
 
Mkuu, hao ndio wanarudi kitaa kutafuta pesa kwa ngeta!
Hivyo tukae mkao wa kutulia, tusubiri yajayo.

Nadhani kungekuwa na smooth transitiin ya maeneo wanayopaswa kufanyia biashara zao, na si kibabe kama ilivyokuwa leo vingunguti.
Magereza yapo yanawasubilia kwa watakaobahatika kufikishwa polisi, nadhani wengi wao ule wimbo palapanda litalia, utawahusu!!yaani waachwe tu kwa wanayofanya eti kisa watakuwa wezi?!!hao ukitumia siasa sana hawataenda, huko wao wanataka sehemu wanayopenda wao na sio sehemu inayowaruhusu kufanya biashara, sehemu ambapo watu wanapita pita na sio sehemu ambayo mtu itabidi kuwafuata!!hao wa vingunguti usione serikali imekaa kimya, ni kuwa kwa chini chini imebariki kutendo hicho, na zamu hii hutamsikia Mh.rais anawapiga mkwara watendaji!!kwani hujasikia huko songwe eti maeneo waliyoonyeshwa ni nje ya mji, hawaendi, wanataka serikali inunue nyumba hapo hapo mjini ndio wawekwe, watu hawa ndio utumie siasa??zamu hii hata kama ni makomandoo wa JWTZ, watatakiwa kutumika watatumika tu!!ndio kilio cha kumlilia mwendazake kisikike vizuri.
 
yestahili kupewa kitambulisho ni mfanyabiashara mdogo yoyote aliye na mtaji wa -4000,000/=. Mengine hayo ni tafsiri yako.
Kumbe hata wewe hujui unachokitetea, yaani mtu mwenye mtaji wa milioni 4, huyo ni machinga?kitambulisho hicho hakihusiani na mtaji wa biashara bali mapato(turnover)ya mwaka.ki uhalisia ukitaka kutenda haki hata muuza kahawa, mama lishe, muuza machungwa, genge hastahili kuwa na hicho kitambulisho bali anatakiwa kwenda TRA, na kukadiliwa kodi ya mapato.ilikuwa ni siasa tu kuona hawa lazima nao wachangie kodi serikalini kutokana na nature ya biashara zao, ni ngumu kuwasimamia.
 
Huna njaa! Huna shida wewe. Ukijaribu kuchangia jaribu kujiweka kwenye nafasi za hao majamaa.

Siyo kweli, tumekua watu wa kuendekeza uholela. Visingizio vya njaa ni uongo mtupu ili kujigichia kama kichaka. Hali ilivyo Mbagala, Mbezi, Gongolamboto, Kariakoo na Karume, Posta kwa kweli ni uholela ambao haukupaswa kuachwa. Machinga Complex iko tupu. Ila watu wamepanga barabarani hii haikubaliki popote duniani
 
Hayo ni maisha ya watu na ni wapi huko frem hazina watu kama kkoo mbona frem zimejaa tatizo mnataka watu wahangaike wakati wamejiajiri kutafuta riziki.Kama serikali ingekua imewekeza kwenywe viwanda na kilimo vijana wengi wangekua wako kwenye ajira.Hili ni bomu kubwa sana linaandaliwa

Mkuu siyo kwa hali ile, yaani imekua ni kero kero kubwa. Pa kupita hakuna, uchafu kila mahali. Ukienda posta ni vibanda kama shambani moshi wa kuni utafikiri kwenye machimbo au site za ujenzi, mimoshi ya ajabu ajabu. Lazima watu watengewe eneo kama ilivyo Karume, Machinga Complex nk lakini watu wasizibe njia, mitaro nk. Haikubaliki!
 
Mji unaonekana mchafu kutokana na wamachinga kuingia adi barabarani. Inakuwa ngumu kama mnapishana na magari mzehe. Kwangu mimi ingependeza wakatafutiwa uwanja. Nchi zilizoendelea uwezi kuta haya.

Mkuu, siyo zilizoendelea, sema nchi za waliostaarabika, huwez kukuta huo upuuzi
 
Back
Top Bottom