Machinga wasilete siasa waondolewe haraka miji yote Tanzania

Hii hata Kariakoo ipo kwa wale wauza Simu,utaina duka moja lina vikabati vingi ujue hapo kila Mtu na kikabati chake anafanya biashara. Sasa nashangaa hawa ndugu zetu wanaopanga biashara zao barabarani na kwenye mitaro.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kariakoo mbona wauza simu wanaungana watu zaidi ya watatu wanakodi fremu na biashara wanafanya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pale barabara ya kutoka Karume kwenda Kariakoo, shule ya msingi mchanganyiko njoa ya kwenda kwa miguu imezibwa kabisa na vimesa, watembea kwa miguu wanapishana na magari na pikipiki barabarani na kuwa katika hatari kubwa ya kigongwa na vyombo vya moto.
 
Mliwapelekea kodi wakagoma kulipa?

Endeleeni kuwahamasisha kinyume
 
Mkuu, hao ndio wanarudi kitaa kutafuta pesa kwa ngeta!
Hivyo tukae mkao wa kutulia, tusubiri yajayo.

Nadhani kungekuwa na smooth transitiin ya maeneo wanayopaswa kufanyia biashara zao, na si kibabe kama ilivyokuwa leo vingunguti.
Maeneo kuyapata ni mtihani maana ni wengi sana. Serikali iboreshe tu miundombinu ya kilimo ili influx ya vijana kurlekea mijini ipungue.

Ushirika na kufanya kazi kwa vikundi kuhamasishwe ili wapatiwe mikopo ya kuwawezesha kufanya shughuli rasmi.

Mtu ana jiko la moto anachoma mishikaki au mihogo katikati ya brbr, ni hatari na siyo stahaa
 
We Chief vp? Kwa nini isiwezekane? Lakini je, lazima iwe Kkoo?
 
Usitete ujinga mkuu, nyeupe iwe nyeupe na nyeusi sema nyeusi. No matter machinga ana mtaji wa aina gani, lazma tuzingatie madhari na usafi wa miji yetu. Huwezi kufanya biashara popote pale utakapojiskia. Iyo haikubaliki.

Na nikukumbushe tu, si wajibu wa serikali kuwekeza kwenye kilimo, sera ya kilimo ya 97 iliweka bayana kwamba serikali imejitoa rasmi kwenye shughuli za kilimo na kubaki kama msimamizi na mtunga sera. Private sector ndio injini ya kilimo kwa sasa, na hao machinga hawajazuiwa kwenda kuwekeza kwenye kilimo.

Tusiilalamikie serikali kwa kila jambo.
 
Watanzania wanapenda kuishi kwa ujanja ujanja tu.

Sio machinga wote ni wamachinga kweli, kuna matajiri kibao wamekodisha watu kuwauzia biashara zao nje ili wakwepe kodi, wanawanunulia vitambulisho vya machinga, kifupi hoja inayokwepwa ni kulipa kodi.
Machinga imekuwa ni kichaka cha watu kujificha wasilipe kodi, ukiangalia kwa haraka haraka huwezi kuelewa utaona wote ni wamachinga kweli kumbe janja janja tu
 
Wameshindwa kuungana wakiwa barabarani wataweza kuungana wakati wa kuondolewa barabarani kwa fedheha?
 
Watafutiwe maeneo ya kufanya biashara
Masoko na minada ipo kila Mkoa/Wilaya/ mpaka ngazi ya kata. Haya ndio maeneo yanapofanyika biashara za namna hiyo, Ukisema watafutiwe na nani tena wakati Maeneo yapo tangu enzi na enzi.
 
Watu wanalalamika kuhusu wamachinga lakini kiukweli hii ishu ni funzo kwetu sote. Vijana tumekosa ubunifu wenzetu machinga wapo lakn si sana kama huku kwasababu watu wamafanya biashara nyingi online. Huku ukitaja online wanakwambia changamoto kubwa ni uaminifu kuna biashara isiyo na changamoto? Solve hyo changamoto na tunaishi kwa mazoea na kuwaamini wana siasa haijalish ni chama gani ila wanasiasa si sakuwaamini......
 
Umezuunguka Sana,Hawa waliruhusiwa kwenye utawala uliopita,utawala uliopita ulikuwa haujali Mambo madogo madogo
 
U
Uvunjwaji wa Sheria na Katiba unafanywa na machinga tu? Polisi, Bunge na Serikali huoni wanachofanya kwa raia na makundi mbali mbali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…