Nampongeza sana Makala na SSH kwa kuwapanga wamachinga vizuri nchi nzima.
Kiukweli wamachinga walikuwa kero sana hasa kwenye majiji makubwa...Leo hii K/kko hauwezi kwenda na gari kununua biadhaa dukani hasa matairi ,vifaa vya umeme etc maana wamachinga wamepanga bidhaa kwenye barabara.
Mitaro yote kwenye majiji juu yake wamejenga vibanda ,services road zote wamezitawala wanatandaza biashara yaani ni kero kero kero,
Wamachinga waende sehemu husika zilizotengwa kufanya bioashara ,sisi wateja wao lazima tuwafuate huko huko walipoweka bidhaa,serikali nayo itanue maeneo hayo makubwa hata kama kulipa wakazi wa huko waondoke ili kutanua masoko au waganwanye wamachinga sehemu nyingine ili wote wapate nafasi za kufanya biashara zao.
Tunaomba serikali msirudi nyuma wamachinga walikuwa kero kubwa sana kwa jinsi walivyokuwa wanafanya biashara,kitu chochote kipya lazima kiwe na changamoto lakini muda ukienda watazoea na watajilaumu kwanini hawakuamua tangu mapema kwenda kwenye maeneo husika.