Hii haihitaji degree kuielezea,
Magufuli hakubana watu wa hali chini kama chinga,bodaboda na wengineo kama mama ntilie na hawa ndio zao la hilo nyomi mnaloliona.
Msisahau kwa tz watu wa hali ya chini ni zaidi ya 70% ya population na mifumo mingi kandamizi hawa imewaweka kando kupitia 20,000/= ya kitambulisho cha chinga.
Chinga karikoo anapanga bidhaa barabarani kwa siku anauza 300,000 lakini hana makadirio yoyote TRA zaidi 20,000/= kwa mwaka ,wakati wewe ukiwa na fremu mauzo 100,000/= kwa siku makadirio TRA 3000,000/= kwa mwaka,sasa kwanini wasizimie msibani?Kabla ya utawala wa magu chinga aliishi kama digidigi kama ambavyo wafanya biashara wa kati na wakubwa wanavyoishi sasa.
Ukweli ni kwamba kama Magufuli angeweza kuwafanya wafanya biashara wa Kati na wakubwa kufanya biashara kwa uhuru,kama angeweza kutominya vyama vingine vya siasa,kama kungekuwa na uhuru wa vyombo vya habari,angelikuwa ni kiongozi bora Sana ila kwakukosa sifa tajwa hapo juu kwangu ndie raisi wa mwisho kabisa.
Huo ndio uhalisia wa mambo nchi imepasuka vipandevipande,hivi ni muhitimu gani atazimia kwa msiba huu?ajira hakuna na ukiipata mshahara unakatwa pesa za mkopo + ma fee mengine ya hovyohovyo.
Hii ilikua ni technique na alifanikiwa sana kwenye hili.
Yote kwa yote RIP