Macho yangu yananidanganya?

Macho yangu yananidanganya?

Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.

Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!

Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.

Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.

Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
 
Mimi mwenyewe nilienda Uhuru jana kumuangalia ili nijiridhishe akifa anafananaje? Kwa kule kujimwambafai naachaje kwenda kumuona. Yani nilitaka tu nijue akifumba macho anakuwaje mwamba yule!
Judas Iscariot...
 
Yaani mnafurahia Rais kuzungushwa mitaani kama sanamu ya mapambo huku akiwa tayari ni marehemu!! Eti mpime ni kwa namna gani anapendwa!!

Inasaidia nini? I wish akapumzishwe mapema iwezekanavyo, na kama ilivyo mila na desturi zetu kama Watamzania/Waafrika.
Coment yako imeka kidini zaidi sio, kama imekaa kidini naomba unijibu nikuulize swali moja tu
 
Leo baada ya askari kusumbua watu na hata kuwapoga makofi wakati watu wakifosi kuingia walianza sema magufuli hakua anatufanyia hivyo, askari alikua mpole sana.
Nampenda Mama Samia. Namuunga mkono. Namtakia kila la kheri.

Ila sina uhakika kama atayadhibiti mafisi ya CCM.

Halafu tuwe wakweli: bila Magufuli tungempata Samia?

Mimi najivunia kuwa na Rais mwanamama.

Lakini tusisahau kuwa Rais Magufuli kahusika kwa kiwango kikubwa sana kwa uwepo wake mama Samia.
 
Hivi ni kwa nini wachukua picha za video hawachukui sehemu ambayo na sisi tunaoomboleza tukiwa nyumbani tunaweza kuona sura ya Mh. Kwa dakika za mwisho? Au wanakatazwa? Au ndio maadili ya kazi yanawataka hivyo!? Ningetamani waonyeshe kama ilivyokuwaga kwa Hayati Baba Wa Taifa!
 
Dodoma siendi. Mie sio kada, ni raia wa kawaida sana hata mtaani kwangu mtendaji mkuu wa serikali ya mtaani kwetu hatujuani, ni mitazamo yenu nyie bavicha ndio mnadhani mie ni kada....
Kwisha kabisa MATAGA, mlizoea kusambaza siasa za chuki kwa watawala ili muendelee kupewa buku 7 za lumumba.


Sasa huyu mama hana mpango wa kuwa na wafanya propaganda za majungu.
 
Walianza ujinga jana kwamba kuna gari zinasomba watu.

walipoona haiwezekani huo wimbo kuingia kwenye maskio ya watu timamu wa akili,wakaona wakaushe.

kwa sasa wanasema watu walikwenda kuhakikisha[emoji23][emoji23][emoji23].
watu wanasema ukiukataa ukweli,utakufata kama kivuli chako na kukuzomea.
 
Mkuu,
Hili ni pigo kubwa sana kwa taifa na Africa kwa ujumla, huyu ndugu ntamkumbuka daima, hofu yangu ni kurudi kwa ccm asilia makamba et al,. Hakuna kitu watu wanakichukia kama ufisadi, na uporaji wa maliasili za nchi, Magu alidhibiti mno. Watu waliona kazi zake ndiyo hiyo nyomi mkuu, I will miss him a lot. Rip Magufuli.

Best,
Kejuu
Kwa taifa labda, Africa how?
 
Dodoma siendi. Mie sio kada, ni raia wa kawaida sana hata mtaani kwangu mtendaji mkuu wa serikali ya mtaani kwetu hatujuani, ni mitazamo yenu nyie bavicha ndio mnadhani mie ni kada....
Nashukuru umejibu kistaarabu mama yangu hakukuuliza swali pia ameshatangulia mbele za haki. Mimi siwezi kumuhususha mama yako kwenye huu upuuzi WA mitandao.
 
Back
Top Bottom