Mada: Fahamu mambo mbalimbali kuhusu gari aina ya Subaru Forester

Hi

Watu wamekua wananunua sana subaru forester.. nimeshawishika kununua moja nimeiona ya mwaka 2011.. anayefahamu undani wake anaweza ku share uzoefu hasa katika matatizo yake na namna ya ku fix

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera kwa uamuzi aisee,
Ila siku nyingine kamwe usifanye manunuzi ya kitu kwasababu unaona 'wengi' wananunua.

Huwezi kujua, hao wengi huwenda hawana taarifa sahihi za wanachonunua.

Miaka fulani ya nyuma huko, kabla ya Toyota Noah kuwa maarufu, watu wengi walinunua gari zinaitwa Toyota Lucida. Na wengine wakanunua magari fulani ya kikorea yanaitwa Ssangyong.

Little did they knew, magari yale yalikua ni tatizo ... hayakuweza kumudu hali za huku.

Niseme kwa bahati nzuri, chaguo ulilofanya ni zuri.
Ni gari inayohimili sana, hali nyingi za barabara hata kwenye vumbi.
 
Inategema na matumizi yako.

Ukiitumia kwa adabu, utafurahi. Haina shida, ground clearance ya kutosha, All Wheel Drive, well balanced barabarani. Wengi wanapata tabu wanapotaka kuzifanya za mashindano, usiingie kwenye mtego wa kuongeza power (tuning) tumia kama ulivyolikuta (stock).

Mafuta haina tofauti sana na Xtrail au Rav 4 Kili Time. Angalizo kama umetokea kwenye magari madogo ya Toyota (IST, Vitz etc), gharama ya parts na service itakustua kidogo 😁😁😁
 
Ha ha ha

Hii mambo, imetesa sana raia.
Matokeo yake, gari leo iko barabarani, kesho iko garage .. ushauri mzuri sana asiifanyie tunings. Though kuna sport zake ambazo zinakuja zikiwa tuned, moja kwa moja from japan,
 
Inategema na matumizi yako.

Ukiitumia kwa adabu, utafurahi. Haina shida, ground clearance ya kutosha, All Wheel Drive, well balanced barabarani. Wengi wanapata tabu wanapotaka kuzifanya za mashindano, usiingie kwenye mtego wa kuongeza power (tuning) tumia kama ulivyolikuta (stock).

Mafuta haina tofauti sana na Xtrail au Rav 4 Kili Time. Angalizo kama umetokea kwenye magari madogo ya Toyota (IST, Vitz etc), gharama ya parts na service itakustua kidogo 😁😁😁
Kuna kifaa kinafungwa Kwenye Subaru zenye turbo charge kinaitwa DUMP VALVE,wengi wanafunga kwasabb ya ule mzuka wa valve zinapofungua Ila madhara yake baadae ni makubwa Kwenye engine
 
ukweli ni kwamba subaru ni gari nzuri sana natumaini ukinunua autajuta kwani
1. aina magonjwa
2.kama ni mtu wa kusafiri itakupa utulivu kwa barabaa
3.mafuta inakula kawaida kabisa
4.kwenye barabara za vumbi linapiga bila shida

hasara ya subaru
jamii inamtazamo wanaomiliki na kuendesha subaru ni vijana wahuni

ila nunua tu autojuta
Mkuu kuna tofauti gani kati ya Subaru Forester 2.0XS na 2.0 XT?.. na ipi ni chaguo bora?
 
Best choice btn the two?...turbo ndo dubwana gani?...toa shule kidogp mkuu...
Naomba nijaribu kidogo kumsaidia kujibu ;
Turbo, ni 'dubwana" ambalo linalazimisha hewa nyingi iingie kwenye cylinder, ambapo hewa hiyo huisidia engine kuzalisha nguvu zaidi (gari kuwa na speed/kuchanganya haraka)

I stand to be corrected

Ahsante,

P. Oligarchy.
 
Best choice btn the two?...turbo ndo dubwana gani?...toa shule kidogp mkuu...
Tofauti kubwa ni namna engine inapumua, bila turbo engine inapumua bila usaidizi. Ikiwa na turbo, hewa inagandamizwa na kuwa na pressure kubwa zaidi (boost).

XT ni turbo na XS ni ya kawaida.

XT ina power zaidi, wenyewe subaru wanasema XS ni 140hp na XT ni 220hp. Kwa sababu XS engine yake ni simple haina vitu vingi, ni more durable na inakula mafuta kidogo zaidi, ila haitembei sana. XT ni moto mwingine, chaguo ni lako. On a personal point, tushatoka na XT saa 12.30 jioni Himo Moshi, by saa 5 usiku tulikuwa Tegeta. Chaguo ni lako.
 
Nimekupata boss,shukrani.
 
Hongera kwa uamuzi aisee,
Ila siku nyingine kamwe usifanye manunuzi ya kitu kwasababu unaona 'wengi' wananunua.

Huwezi kujua, hao wengi huwenda hawana taarifa sahihi za wanachonunua.

Miaka fulani ya nyuma huko, kabla ya Toyota Noah kuwa maarufu, watu wengi walinunua gari zinaitwa Toyota Lucida. Na wengine wakanunua magari fulani ya kikorea yanaitwa Ssangyong.

Little did they knew, magari yale yalikua ni tatizo ... hayakuweza kumudu hali za huku.

Niseme kwa bahati nzuri, chaguo ulilofanya ni zuri.
Ni gari inayohimili sana, hali nyingi za barabara hata kwenye vumbi.
Hahahah Enzi hizo Ssangyong inaitwa "Musso" zilikuwa gari za ushuani sana. Prado akaja kuifuta sokoni.
 
ukweli ni kwamba subaru ni gari nzuri sana natumaini ukinunua autajuta kwani
1. aina magonjwa
2.kama ni mtu wa kusafiri itakupa utulivu kwa barabaa
3.mafuta inakula kawaida kabisa
4.kwenye barabara za vumbi linapiga bila shida

hasara ya subaru
jamii inamtazamo wanaomiliki na kuendesha subaru ni vijana wahuni

ila nunua tu autojuta

Kuna suala hapa kuna mtu alinidokeza nikaona ni busara kuuliza kwa wazoefu. Subaru Forester zisizo na Turbo za kuanzia mwaka 2008 au 2009 - 2011 zinatumia electric steering wheel (au za bush wengine wanaita). Wakati zile zenye turbo zinatumia hydraulic. Je, hizi zisizo na turbo hiyo steering system inasumbua kiasi gani?? Ni kitu cha kuepeuka ikiwezekana? Najua vanguard zina shida hiyo pia kwamba na hizi barabara zetu baada ya muda lazima ianze kugonga. Ushauri tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii gari ina miaka sita naitumia tangu ilipoiagiza kutoka Japan. Hii ina turbo (chips mayai) zingine model kama hii hazina turbo (chips kavu). Engine haijawahi kuguswa, zaidi ya kubadilisha plagi, petrol filter na oil filter. Nyepesi sana kuondoka. Ukisafiri mwendo mrefu ndio utaona utamu wa subaru. Shida ya subaru spare zake zinapatikana kwa shida na bei yake imechangamka. Siyo kila sehemu unaweza kupata spare yake kama toyota
IMG_20200425_153125_5.jpeg

kp app
 
Back
Top Bottom