MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

MADA: Fahamu zaidi kuhusu mbinu za kilimo cha tikitimaji, faida na changamoto zake

KWELI TUNA SAFARI NDEFU KAMA JAMII.
Hivi milioni 20 nzima uweke kwenye kilimo tena cha matikiti???!!!!!
MKUU NIACHE KIDOGO
 
Habari yenu,
Nadhani hapa kuna wataalamu wa kilimo, nimepata sehem nataka nilime matikiti maji kwa kuangalia nimeona ndo biashara inayolipa haraka haraka,

Mtaji nilionao wa kuanzia ni 20,000,000 naomba ushauri wenu juu ya hatua za kufuata,
Usijaribu, kilimo cha whatsapp hicho. Ukishupaza shingo kalime uone
Kama unataka kulima kalime vitunguu swaumu uza Marekani vina soko kubwa
 
KWELI TUNA SAFARI NDEFU KAMA JAMII.
Hivi milioni 20 nzima uweke kwenye kilimo tena cha matikiti???!!!!!
MKUU NIACHE KIDOGO
kuweka sio shida ila inatakiwa uwe na xperience hapa nlipo kuna mjeda ana heka 34 analima za tikiti soko lake lipo Nairobi ndo soko la uhakika
 
kama kichwa kinavyojielezea najua wengi mmepata hasara kwenye kilimo hiki! me cjawahi pata hasara hata mara moja labda nipate faida ndogo zaidi ya nliyoiwazia.

nimelima hii ni mara ya 4 mara ya kwanza nlilima heka moja mara ya pili 2 mara ya 3 mbili sasa hiv nalima heka 3 na nusu.

kikubwa tkiti inahitaji mtaji mkubwa yaaani tikiti ni kama kumhudumia mwanamke jinsi unavyozidi kumhonga ndo anavyopendeza ntajibu maswali kwa kadri nitakavyoweza.
 
Nikihitaji kulima hiki kilimo vitu gana vya msingi natakiwa kuzingatia?
 
Nikihitaji kulima hiki kilimo vitu gana vya msingi natakiwa kuzingatia?
location ya shamba isiwe bondeni iwe na rutba iwe na maji lakini yasiyotuama mtaji usiwe wa mashaka yaani isiwe unaombwa dawa hadi usubirie mshahara uwe na uhakika unakijua au unayemuweka shamba anajua magonjwa na jinsi ya kuyakabiri
 
location ya shamba isiwe bondeni iwe na rutba iwe na maji lakini yasiyotuama mtaji usiwe wa mashaka yaani isiwe unaombwa dawa hadi usubirie mshahara uwe na uhakika unakijua au unayemuweka shamba anajua magonjwa na jinsi ya kuyakabiri
Kwa uzoefu wako ina ghalim kiasi gan kwa heka 1 mpaka hatua ya kuvuna ?
 
gharama inatokana na sehemu unayolimia ila inarange kati ya 1 m hadi 1.5

roughly iko hivi kwa nlipo
kukodi shamba 60000
kulima50000 /kupiga tuta 100000 tuta wanapiga msimu wa mvua
mbegu Sukari F1 230000
mbolea ya samadi gunia 12@15000=180000
chakula na nauli weka 200000
posho za kbarua za kuandaa hadi kumaliza 250000
mbolea 4@65000(bei zna range hii ni rough)=195000
dawa na booster 300000
Jumla 1565000

hapo bado hujanunua pump kwa maeneo kame na bomba za kupulizia dawa

ukizipanga vizuri znatoa gari 3 za tani 3.5 au 2.5 kila gari unauza 1.5-2 mill kwahiyo ukivuna hutakosa 3-5 mill sio hela ndogo

kikubwa ukianza lima usiwe mbali na shamba
 
Mimi ndo nataka nianze? Nipo dar. Sina hakika mda mzuri wa kupanda ni UPI? Naomba maelekezo hatua ya mwanzo hadi mwisho hatua kwa hatua. Nataka niwasiliane na mtu mwenye Shamba nikajifunze.
 
Jenseny,
Sawa sawa mkuu mbona kuna rafiki zangu wa kanda za juu milimani maeneo ya Marangu kule karibu na hifadhi ya mlima,wanasema wanapanda hayaoti vizuri.Jee? Kuna uwezekano wa kupata mbegu unaoweza kustahimili kanda za juu? hususani kwa wenzangu wachaga huko?
 
Je, kipindi cha masika unaweza kupanda tikitiki, coz kuna mdau flani nilimtembelea shambani kwake kipindi hiki cha mvua za vuli nikakuta tikitiki zake zinaoza akanambia tatizo ni mvua, sasa je mtu akipanda kipindi cha masika ataweza kupata kitu kweli? Je waweza kutuelezea kidogo changamoto za magonjwa na dawa zake na vipi kuhusu soko?
 
Back
Top Bottom