Ni zao zuri sana kutokana na soko lake kuwa kubwa. Ukifata kanuni za kilimo utafanikiwa na kutajirika kwa muda mfupi. Nitatoa mfano, kuna rafiki yangu yeye alipandaga karibu heka moja ila alichokosea ni kwamba alipanda ktk msimu ambao sio muda wake. Yani kipindi cha masika kilifika wakati ambapo miche ya mitikiti haijakomaa shambani, hivyo mvua ilivyonyesha miche yote ilivunjika vunjika na jamaa akala hasara. Kabla hujajiingiza kwenye kilimo hiki ni vizuri ukawatembelea wazoefu wakakupa maujuzi na mbinu wanazotumia vinginevyo hasara utayopata hutoisahau maishani mwako