Mada maalum kwa wachoraji, sanaa ya picha na rangi

Hapa ndo kuna tatizo,
Familia zinataka daktari, mwalimu, rubani n. K

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia nadhani hata wazazi wetu hawakua na ufahamu mkubwa juu ya taaluma hii ya uchoraji,kwa kifupi uchoraji ni sehemu ya ubunifu,mfano achilia mbali injini,lakini magari mazuri ,majengo mazuri,mavazi mazuri,fenicha nzuri mapambo mazuri na bidhaa nyingi zitengenezwazo viwandani ,wachoraji picha ndio huweka umbo la nje ama sura ya nje,sasa kwa nchi za wenzetu wachoraji huajiliwa sana,na siku hizi wachoraji wanahitajika sana kwenye mashirika ya kijasusi na idara za upelelezi za polisi (CIA,SCOTLAND YARD,FBI,FSB MOSSADnk) kwa kazi muhimu sana ,wachoraji ni taaaluma pana sana,tazama vitu kama viatu,triningi shoes,jeans, nk ni kazi za wachoraji,vyombo kama mafriji,matv,na zana mbalimbali,umbo la nje ni kazi za wachoraji,tazama madege mazuri kama boing,Air bus yanavyovutia kwa nje ni kazi za wachoraji,vitu ni vingi mno,ila wazazi wetu hawakujua vitu kama hivi,wangetuachia tufanye vitu tunavyoviweza tungefika mbali na kuiletea nchi faida.
Mdada moja mchoraji huko Sweden alimuona muuaji wa Olof Palme waziri mkuu AKACHORA PICHA YAKE na akajakamatwa lwa picha ya kuchora.
 
Siku maisha yakiwachapa hadi hao ndg zako ukashindwa wasaidia ndo wataona faida za imani uchwara, eti 'ukafiri' mimi kuna mipaka ya kuiamini na kuitumikia dini na kuishi katika dini ya kiislamu, mtu ukiniletea hizo stori za masheikh uchwara huwa sikuelewi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili lingetokea bongo,
Lingeleta positivity

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana rafiki, hii ndiyo Afrika. Dira yenye fursa ya kumfanya mtu aendelee kimaisha na kumfanya afike mbele zaidi kwa mtu mmoja mmoja na taifa imewekezwa kwenye fani za elimu tunazochepua nazo kutokea sekondari, na Tanzania ndivyo ilivyo. Mbali na hapo mzazi hakupi fursa kwa sababu ndivyo misingi ulivyojengeka.

Angalau miaka ya hivi karibuni wenye vipaji wameanza kuthaminiwa na imefungua jicho la tatu kwa serikali kwamba, mbali na elimu kipaji kina uwezo wa kuwa ni ajira rasmi, kupata pato binafsi la uhakika na kuchangia pato la Taifa. Mpira na usanii wa mziki umetizamwa kwa jicho la nuru kwa sasa hivi.

Nina imani kadri muda unavyozidi kwenda sanaa/kipaji cha uchoraji kitapewa uwanja mpana na kufanywa ni miongoni kwa ajira rasmi na yenye kuheshimika.

Binafsi, wenye kipaji/sanaa ya uchoraji nawaheshimu, nawaona ni watu wenye akili ya ziada. Si jambo rahisi hisiya kuziwasilisha kwa njia ya mchoro tena mchoro wenye mafumbo.

Ukirudi tena kwenye fani ya uchoraji nitakuwa mteja wako wa uhakika.
 
Nadhani wazazi wetu walikua hawajagundua kuwa kuna sehemu watu wamebadilisha maisha kabisa ya familia zao hapa duniani,ni mabilionea wakubwa kwa kuchora tu,Pablo Picasso etc
Singida kuna michoro ya miaka na miaka iliyofanywa kwenye miamba, bahati mbaya inatoweka kwa sababu sisi tumejikita kwenye mlima Kilimanjaro na wanyamapori! Macho yetu hayazielewi picha za kuchora.
Tanzania tulikuwa na kina prof. Jengo (udsm) na prof. Msangi (Kenyatta University) wametoweka na kazi zao!
 
Prof. Kenneth F. Msangi, huyu alinifundisha kuchora Iyunga Mbeya mwaka 1968 na kuniwezesha kupata A (credit) mtihani wa Cambridge. Moja ya picha zake ninayoikumbuka ilikuwa na jina CALVIN (Calvin Mbowe) marehemu, huyu alikuwa mwanafunzi wake na ni kaka yake mhe. Mbowe. Picha hii aliiweka kwenye onesho lake pale makumbusho ya Taifa, ilikuwa picha nzuri sana. Baadaye K. F. Msangi alienda kufundisha chuo kikuu cha Kenyatta ( kama sijakosea) mpaka kifo kilipomkuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…