Mada maalum kwa wachoraji, sanaa ya picha na rangi

Mada maalum kwa wachoraji, sanaa ya picha na rangi

Hapa ndo kuna tatizo,
Familia zinataka daktari, mwalimu, rubani n. K

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia nadhani hata wazazi wetu hawakua na ufahamu mkubwa juu ya taaluma hii ya uchoraji,kwa kifupi uchoraji ni sehemu ya ubunifu,mfano achilia mbali injini,lakini magari mazuri ,majengo mazuri,mavazi mazuri,fenicha nzuri mapambo mazuri na bidhaa nyingi zitengenezwazo viwandani ,wachoraji picha ndio huweka umbo la nje ama sura ya nje,sasa kwa nchi za wenzetu wachoraji huajiliwa sana,na siku hizi wachoraji wanahitajika sana kwenye mashirika ya kijasusi na idara za upelelezi za polisi (CIA,SCOTLAND YARD,FBI,FSB MOSSADnk) kwa kazi muhimu sana ,wachoraji ni taaaluma pana sana,tazama vitu kama viatu,triningi shoes,jeans, nk ni kazi za wachoraji,vyombo kama mafriji,matv,na zana mbalimbali,umbo la nje ni kazi za wachoraji,tazama madege mazuri kama boing,Air bus yanavyovutia kwa nje ni kazi za wachoraji,vitu ni vingi mno,ila wazazi wetu hawakujua vitu kama hivi,wangetuachia tufanye vitu tunavyoviweza tungefika mbali na kuiletea nchi faida.
Mdada moja mchoraji huko Sweden alimuona muuaji wa Olof Palme waziri mkuu AKACHORA PICHA YAKE na akajakamatwa lwa picha ya kuchora.
 
[emoji2]
FB_IMG_1553847113707.jpeg
FB_IMG_1553844766607.jpeg
FB_IMG_1553845094007.jpeg
FB_IMG_1553796255016.jpeg
FB_IMG_1553796355903.jpeg
FB_IMG_1553794047080.jpeg
FB_IMG_1553791413496.jpeg
FB_IMG_1553789772763.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kutokea mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya uchoraji ya watoto ya dunia.nikapata medali na vitu vingine lakini ..
Wazazi na hata walimu hawakukubali offer niliyopewa kwenda kusoma Japan miaka mitatu...
Kisa wale ni makafiri ..watanikengeusha! Jamii nzima iliungana kupiga vita...matokeo sikwenda na wala sikuendelezwa tena.Ila toka ndani ya moyo wangu napenda mno kuchora...ni basi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku maisha yakiwachapa hadi hao ndg zako ukashindwa wasaidia ndo wataona faida za imani uchwara, eti 'ukafiri' mimi kuna mipaka ya kuiamini na kuitumikia dini na kuishi katika dini ya kiislamu, mtu ukiniletea hizo stori za masheikh uchwara huwa sikuelewi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia nadhani hata wazazi wetu hawakua na ufahamu mkubwa juu ya taaluma hii ya uchoraji,kwa kifupi uchoraji ni sehemu ya ubunifu,mfano achilia mbali injini,lakini magari mazuri ,majengo mazuri,mavazi mazuri,fenicha nzuri mapambo mazuri na bidhaa nyingi zitengenezwazo viwandani ,wachoraji picha ndio huweka umbo la nje ama sura ya nje,sasa kwa nchi za wenzetu wachoraji huajiliwa sana,na siku hizi wachoraji wanahitajika sana kwenye mashirika ya kijasusi na idara za upelelezi za polisi (CIA,SCOTLAND YARD,FBI,FSB MOSSADnk) kwa kazi muhimu sana ,wachoraji ni taaaluma pana sana,tazama vitu kama viatu,triningi shoes,jeans, nk ni kazi za wachoraji,vyombo kama mafriji,matv,na zana mbalimbali,umbo la nje ni kazi za wachoraji,tazama madege mazuri kama boing,Air bus yanavyovutia kwa nje ni kazi za wachoraji,vitu ni vingi mno,ila wazazi wetu hawakujua vitu kama hivi,wangetuachia tufanye vitu tunavyoviweza tungefika mbali na kuiletea nchi faida.
Mdada moja mchoraji huko Sweden alimuona muuaji wa Olof Palme waziri mkuu AKACHORA PICHA YAKE na akajakamatwa lwa picha ya kuchora.
Hili lingetokea bongo,
Lingeleta positivity

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rafiki inaonekana unapenda sana michoro. Kumbe ningeendelea na uchoraji ungekua mteja wangu.Mimi najua kuchora aisee,wala sijisifu,lakini sikuendelea na uchoraji,niliingia fani nyingine kabisa,kuchora imo kwa damu yangu,hata sasa nikiamua kurudi sipati tabu kwani nilizaliwa mchoraji,ila wakubwa zangu hawakutaka nijikite huko.
Pole sana rafiki, hii ndiyo Afrika. Dira yenye fursa ya kumfanya mtu aendelee kimaisha na kumfanya afike mbele zaidi kwa mtu mmoja mmoja na taifa imewekezwa kwenye fani za elimu tunazochepua nazo kutokea sekondari, na Tanzania ndivyo ilivyo. Mbali na hapo mzazi hakupi fursa kwa sababu ndivyo misingi ulivyojengeka.

Angalau miaka ya hivi karibuni wenye vipaji wameanza kuthaminiwa na imefungua jicho la tatu kwa serikali kwamba, mbali na elimu kipaji kina uwezo wa kuwa ni ajira rasmi, kupata pato binafsi la uhakika na kuchangia pato la Taifa. Mpira na usanii wa mziki umetizamwa kwa jicho la nuru kwa sasa hivi.

Nina imani kadri muda unavyozidi kwenda sanaa/kipaji cha uchoraji kitapewa uwanja mpana na kufanywa ni miongoni kwa ajira rasmi na yenye kuheshimika.

Binafsi, wenye kipaji/sanaa ya uchoraji nawaheshimu, nawaona ni watu wenye akili ya ziada. Si jambo rahisi hisiya kuziwasilisha kwa njia ya mchoro tena mchoro wenye mafumbo.

Ukirudi tena kwenye fani ya uchoraji nitakuwa mteja wako wa uhakika.
 
Nadhani wazazi wetu walikua hawajagundua kuwa kuna sehemu watu wamebadilisha maisha kabisa ya familia zao hapa duniani,ni mabilionea wakubwa kwa kuchora tu,Pablo Picasso etc
Singida kuna michoro ya miaka na miaka iliyofanywa kwenye miamba, bahati mbaya inatoweka kwa sababu sisi tumejikita kwenye mlima Kilimanjaro na wanyamapori! Macho yetu hayazielewi picha za kuchora.
Tanzania tulikuwa na kina prof. Jengo (udsm) na prof. Msangi (Kenyatta University) wametoweka na kazi zao!
 
Habari za wakati huu kwenu wote!

UCHORAJI ni sanaa ya kuweka alama kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kuchorea, kama vile kalamu ya wino au ya risasi , burashi ,
penseli za rangi ya wax, crayoni, makaa, choko, pastels, aina mbalimbali za erasers, markers, styluses, metali mbalimbali (kama silverpoint) na siku hizi hata elektroniki au kitu kingine cha kuandikia au kupaka rangi katika karatasi ,
kitambaa , ubao , metali , mwamba, kadi, plastiki, ngozi, canvas, na bodi au penginepo.
Mimi kama mchoraji wa kiwango cha kawaida tu, nimeamua kuleta uzi huu kwa watu wote ndani ya jf na nje.
kwa kua na heshimu kazi za wachoraji WAKUBWA, wakawaida na hata wadogo ndani na nje ya Tanzania.

Kama wewe ni mchoraji au umeona sehemu mchoro unaweza kuleta hapa na sisi tukaona vipaji vya watu na kufurahi pamoja.

Kuna baadhi ya michoro si rahisi mtu aamini kama imechorwa na mkono wa mtu lakini ndivo ilivyo.
Baadhi ya majina ya wachoraji ni hawa

1-Da Vinci
2-picasso
3-Kipanya
4-Tingatinga
5-Olumide
6-mimi ( [emoji23])
Na picha au michoro ni hii hapo chini,

Yenye rangi ni ya mnigeria anaitwa OLUMIDE

Ongezeni michoro mingine Tafadhali View attachment 1055295View attachment 1055296View attachment 1055297View attachment 1055298View attachment 1055299View attachment 1055300View attachment 1055301View attachment 1055302

Sent using Jamii Forums mobile app
Prof. Kenneth F. Msangi, huyu alinifundisha kuchora Iyunga Mbeya mwaka 1968 na kuniwezesha kupata A (credit) mtihani wa Cambridge. Moja ya picha zake ninayoikumbuka ilikuwa na jina CALVIN (Calvin Mbowe) marehemu, huyu alikuwa mwanafunzi wake na ni kaka yake mhe. Mbowe. Picha hii aliiweka kwenye onesho lake pale makumbusho ya Taifa, ilikuwa picha nzuri sana. Baadaye K. F. Msangi alienda kufundisha chuo kikuu cha Kenyatta ( kama sijakosea) mpaka kifo kilipomkuta.
 
Back
Top Bottom