Mada maalum kwa wanandoa

Mada maalum kwa wanandoa

unaiba mume wa mtu.....na kwa bahati mbaya hakuna namna ukampata mwanaume wa peke yako,endelea kujipa moyo

Na tena niko depressed nina stress niko lonely na mazagazaga yote.....

Sina moyo nina maini tuu ndo nimeambiwa hayazeeki na umri.... ila kuna homa ya ini... sijui inatibika...!!?
 
Haya yatabaki sirini kwakweli , sipendi kuwafanya ambao hawajaoa wasioe mana ni mambo ya kuumiza sana, lakini all in all NDOA INA MATATIZO SANA, Ungeona nilivyoanza na makonfi, kila mahari hunikosi na wedding ring, hehehehe kwa sasa hata asubuhi ndani unatoka unanyata mana ukitoka yuko macho basi kasheshe lake lazima ofisin wapate story kutoka kwako


Sent from my iPhone using JamiiForums
Aajaaaajaaaah sasa mbona hiyo sio furaha ni karaha?[emoji2958][emoji2958][emoji849]......kama Kuna mengine mpaka umeficha seems so serious asee!

Ila kiukweli kabisa ndoa ni ngumu sio mbaya ila ni ngumu kwelikweli inabidi ukaze si kitoto!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hujuagi kuwa ubaya ndo huwa unavuma kuliko wema? Wapo wenye ndoa njema kibao tu, sema wengi wao hawanaga muda hata wa kuandika. Na hata wakiandika kusifia ndoa zao, tunakuwa wa kwanza kuwaongelea mbovu, sijui ndoa yenu ina miaka mingapi blah blah blah. In short binadamu hatupendi habari nzuri

Ukisoma comment za humu unaweza amini ndoa ni mbaya na zina mabaya kibao.

Ukileta thread ya kukandia ndoa watu watakupa pole kibao ila leta thread ya kusifia ndoa yako utakandiwa mpaka basi.
 
Kila la kheri wenye ndoa.

Mahisiano niliyopitia nyuma yalinifanya nikafunga mlango wa ndoa, ila mahusiano ya sasa na Dadii ni paradiso na tukigombana tunaambiana ukweli waziwazi usoni bila kuoneana aibu.

Kesho yake tunakumbatiana kama kawaida, Mahaba yetu matamu sitamani ndoa tena....
Na iman kila dini inatufunza kuepuka uzinifu,uwe uislam,ukristo...na ndoa ndio njia yenyewe ya kuupuka hamna shortcut so siwezi kukunga mkono kwenye maamuzi yakoo bali maisha kila mtu anayake uwe bachelor ,uwe married we all have problems asikudangany mtu ndo nikitu kizuri saana na kumpendeza Mungu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh..! Hii ndoa ikifikiasha mwaka sijui...!!!?!

Maana naona kuna vitu navimiss ukizingatia mwanamke mwenyewe kichwa ngumu, yaani afadhari angekuwa tayari kukusikiliza, yeye nikiwa namwambia kitu kama kumwelewesha ataanza ubishi na kuleta ujuaji


Nikimwambia usifanye hivi ye atafanya

Hakuwahi kufanya kosa akaomba msamaha, yaani yeye muda wote anajiona yupo sahihi, kukiri kakosea hilo kwake halipo

Nnampaango wa kumsafirisha aende kwao ili mi nipumzike,

Maana afadhari angekuwa yupo tayari kunisikiliza, yeye nikimwambia tuongee atanijibu yupo busy

Sa sijui mwanamke wa aina hii nitaishi nae vipi...!

Kuna mdau mmoja kashauri kitu cha maana sana, tafuta furaha binafsi, waweza jikuta unaongea mwenyewe hivi hivi, mpaka namkumbuka x wangu niliyemkimbia mana I was a king to her, ila huku am just a man with a trouser


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Daah manengelo my sista, nimeumia sana kusoma ulichoandika, yaan sijui hata nikwambieje my dada, uko kwenye hard time sana, ni njiapanda hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app


asante sana mkuu...naumia...naumia sana..siumii kisa nimeamua kuondoka naumia wanangu...hawajui kitu kila siku nawadanganya nipo hosptal..!this too shall pass
 
Kwenye ndoa kuna mambo mengi sana.
Kuna wakati mkeo anakuwa rafiki yako.
Wakati mwingine anakuwa adui yako.
Wakati mwingine anakuwa boss wako vice versa is also true.

Wakati mwingine mume unakuwa polisi na mke mfungwa vice versa is also true
Wakati mwingine chumbani kunageuka ulingo wa masumbwi na watoto washangiliaji

Wakati mwingine mnakuwa majirani kila mtu hajui kinachoendelea kwa jirani yake

Wakati mwingine mnakuwa mtu mmoja indivisible being

Wakati mwingine mmoja anakuwa Mtoto na mwingine ni mzazi.

Na haya ndiyo huwa maisha yetu ya kila siku ndoani.

Asikwambie mtu hakuna Kitu kinachoongeza heshima na hadhi ya mtu kama ndoa.

Onyo. Usiulizie matumizi ya hela za mkeo jifanye huoni yanayoendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Waambie wanaokwepa majukumu ,nime penda maneno yako kabsa Mungu akubari na atubariki soote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aajaaaajaaaah sasa mbona hiyo sio furaha ni karaha?[emoji2958][emoji2958][emoji849]......kama Kuna mengine mpaka umeficha seems so serious asee!

Ila kiukweli kabisa ndoa ni ngumu sio mbaya ila ni ngumu kwelikweli inabidi ukaze si kitoto!

Sent using Jamii Forums mobile app

Uvumilivu na ujasiri kiwango cha kujifunika shuka moja na snake ndiyo unahitajika


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom