Mada maalum kwa wanandoa

Watoto Wana umri gani?
Kuna mmoja wa kiume ana miaka miwili na miezi mitatu, wa kike ana miezi mitatu (huyu hakutaka nijihusishe kumpa jina kabisa jina katoa yeye na ndugu zake jina nililotoa mimi yeye halitaki anataka mtoto aitwe jina la Bibi yake mzaa mama wakati huyu mtoto wa kiume aliniambia nisitoe jina la babu yaani la Baba yangu ila yeye sasa kampa jina la mama yake)
 
Yani rafiki yake MTU wa form four, na mshonaji hapo nimepata kujua uelewa wa mkeo jinsi ulivo mdogo, mda wote alificha makucha baada ya ndoa kayatoa
Mwenyewe hapa mpaka sasa najiuliza, kaficha makucha miaka minne ya uchumba, kashindwa kuyaficha japo miaka miwili ya ndoa?!!!
 
Huyu mkeo ni mwanamke mpumbavu mno hasa number 4 ka kubuhu au ulioa mwanamke wauswahilini maana duh ana akili za kushikiwa huyo mambo ya ndoa na majirani wapi na wapi
Huyu kalelewa na shangazi yake, baada ya kumshirikisha Dada yangu ( baada ya kumpa taarifa ajenda ya kikao ) akaniambia huyo hata shangazi yake aliyemlea na kumsomesha alikua akigombana nae, nikamuuliza kwa nini hukuniambia mapema kabla sijaoa, ye akanijibu kuwa aliona katulia na alishampa kitchen party kama mke mtarajiwa wa kaka yake
 
Hapo kwenye akili za kushikiwa hapo upo sahihi
Maana yeye akiona fulani anamfanyia mme wake hivi na yeye atataka kufanya, pia Bongo movie zimemuharibu sana, hajui kama wenzake wanaigiza na nia yao ni kufundisha kwamba wanayoigiza yanatokea katika jamii na hayafai kumfanyia mwenzi wako, hili yeye halijui
 
Hahaaa Heheee mngekubaliana kuneutralize muweke like 1 day per week, as outing tamu Sana beans na Ina imarisha mahusiano
 
Mmh Mama Terry umo humu? Ni yule tunayemjua ama?
Hahaa yule yule, leten matatizo yenu yote niwape uzoefu, ndoa tamu Sana Kama kweli mlipendana tangu day one, sio ulipenda pesa ukifika ndan unazizoea unaanza kutafuta mambo yako.
Afu mjifunze kuneutralize interest zenu kwa kujali furaha pande zote, ongeen pamoja kwa kila Jambo na kubwa zaidi mkiweza kujua maisha yenu Ni yenu tu hayamhusu yeyote nje itakua poa Sana.
Na ndoa zenye furaha zaidi Ni watu wanaojua kipato Cha mwenzie, ujue ukificha anakufikiria unapata nyingi kumbe huna hata kumi.
Mjifunze pia kuwa na budget like % Fulani ya maendeleo, nyingine ya kula Bata na nyingine kila mtu atume kwao na other personal needs.
 
Duuh pole Sana, huyo sio mke Ni shidaa Kama uloandika Ni kweli
 
Y: Una malengo, ndoto, mipango, matamanio yako ambayo unatamani uyatimize katika uhai wako.
Tabia, makuzi na malezi tofauti.

X: Vilevile na huyu ana malengo, ndoto, mipango, matamanio yake ambayo anatamani ayatimize au ayafikie katika uhai wake.
Tabia, makuzi na malezi tofauti.

SASA MNAKUTANA UKUBWANI ILU MUWE KITU KIMOJA, HAPA NDIYO MTIHANI ULIPO.
 
Hayo yote ni ya kweli hakuna hata moja nililomsingizia, ukipitia na comment zangu zilizotangulia zipo tabia zake nyingine ambazo hapo sikuziandika

Wakati nipo kwenye harakati za maandalizi ya ndoa nilijiambia huyu mwanamke sitamuacha mpaka nijue anachepuka

Lakini baada ya kukutana na tabia hizo ikabidi ninyooshe mikono juu maana nimefikiria mengi sana na kugundua kwamba nisipomuacha mwisho wangu utakua mbaya

Duuh pole Sana, huyo sio mke Ni shidaa Kama uloandika Ni kweli
 
Huyo hajielewi aisee shida huwa mnavutiwa na uziri wa nje na kusahau uzuri wa roho, tabia na kujielewa
 
Mkeo aliishia lasaba nini au ni slay quern anaweza kulea watoto vzuri?
 
Mkeo aliishia lasaba nini au ni slay quern anaweza kulea watoto vzuri?
Kaishia kidato cha pili

Kulea anaweza ila sasa huyu nna wasi wasi kichwani hazimtoshi, huyu mtoto wa miezi mitatu kaanza kumnywesha uji akiwa na miezi miwili,
Nikamuuliza kwa nini, akanijibu maziwa ya kunyonya hashibi ndo maana anasumbua analia mara kwa mara ( mtoto ni kibonge )
Nikamwambia kwa nini hukuniambia nitenge bajeti ya maziwa? Jibu hana

Kubwa kuliko mtoto akawa anamsumbua kunywa uji akataka kumpiga kibao...mtoto wa miezi miwili apigwe kweli, siku hiyo nilimuangalia tu na angempiga ningemrukia kichwa hicho sijui ingekuaje
 
Duh [emoji26] watoto wadogo sana
 
Kwanini ulioa mtu aliyeishia form two maana uelewa wake mdogo au ndo ile dhana huwa mna assume humu Jf kuoa asiye na shule ila akutii sasa madhara yake ndo haya, hapo nakupa pole umejifunga kitanzi kitakachokutesa the rest of ur life, yani anampa mtoto uji hajafikisha six month's the big problem ninayo ioana hapo mumepishana uelewa na vipaumbele mmoja mtu mzima mwingine hafikirii mbele hapo assume siku haupo duniani watoto wataishije, mumepeleke elimu ya watu wazima bila hivo atakuua Kwa pressure ikiwezekana usizae karibuni tena
 
Mama Terry niruhusu niweka mada maalum kwa ajili yako ujibu maswali ya wengi... Am sure kuna wengi wangetaka kujua mengi kuhusiana nawe... Waiting useme SU...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…